Connect with us

Cellebz

Abert Mangwea Mkali wa Free-style aliye ondoka na Kipaji chake..

Published

on

Historia yake Kwa ufupi..
Alizaliwa na jina la Albert Keneth Mangwair mnamo tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo.
Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) – na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair aliacha mtoto mmoja.
Kazi na Muziki..
Ngwair alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikokutana na mtayarishaji mahiri wa mziki P. Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2003 ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho ‘Ghetto Langu,’ wimbo uliompatia umaarufu mkubwa sana.
Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatokea kwa wimbo wa kimya kimya akiwa na wana chemba. Katika Kimya Kimya anapagawisha.Zipo nyimbo nyingi ambazo Mangwea alitisha nazo kama Vile Gheto langu, Mikasi, CNN, she got gwan, Dakika moja, Mungu Nisamehe, na pia alipata colabo zilizo hit kama ile ya May Baby yake Quick Raka, na nyingine kibao.
Kifo na mauti…
Albert Mangwair alifariki tarehe 28/5/2013 akiwa huko Afrika ya Kusini. Taarifa zinasema alifariki baada ya kutumia madawa ya kulevya lakini kuna utata kuhusu kilichosababisha kifo cha marehemu, licha ya baadhi ya mitandao mbali mbali kuandika chanzo cha kifo cha mkali huyu ila baadae iligundulika kwamba alilewa kupindukia ilhali hakua amekula.(Rest in peace Mangwea).
Pengo la mangwea katika Bongo Flava/Jamii…
Hakika itachukua Muda mrefu kwa pengo lake kuzibika ama hata Pengo lake kutozibika daima maana kipaji chake na mtazamo wake ulikuwa ni wa hali ya juu mno. Mashairi yake yaliburudisha, Kuelimisha jamii. Mchango wako utakumbukwa na wengi wakubwa ama wadogo, Muziki wa bongo Flava utakukumbuka kwa mchango wako mkubwa uliokua ukiutoa ili mradi tuu uone muziki huo ukisonga mbele na kukua.
Tizama Moja kati ya Video ambayo mimi naipenda kutoka kwa Mkali huyu wa free style( Kimya kimya)

Utakumbukwa na wana kibao, washkaji zako wakina J-Moe, Wana Chemba, T.I.D, Bongo Records na wengine kibao ambao walikuepo kipindi ukiwa china na hata kipindi ukiwa nazo(Marafiki wa dam dam). Mashabiki zako Tutakukumbuka kwa ngoma zako za kinyamwezi na Flow zenye mautam na zaidi ya yote tutazikumbuka zile shows zako.
Naamini ngoma zako zikipigwa club yeyote bado mzuka utakua ule ule daima.
PUMZIKA KWA AMAN MANGWEA, MBELE YAKO NYUMA YAKO.

 

But I must explain to you how all this mistaken idea of denouncing pleasure and praising pain was born and I will give you a complete account of the system, and expound the explorer of the truth, the master-builder of human happiness. No one rejects, dislikes, or avoids pleasure itself, because it is pleasure, but because those who do not know how to pursue pleasure rationally encounter consequences that are extremely painful.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Cellebz

Fahamu historia ya Kundi la UB40

Published

on

Ninapoongelea UB40 hapana shaka kwa wewe mpenzi wa burudani ya Muziki utakua unajua anwaongelea wakina nani.  Kwa namna moja ama nyingine utakua umekwisha kusikia kibao kama vile “Red Red Wine, I got the Cup” na ule wa Falling in Love with You. Sasa pata kujua nyimbo zote hizo ni kazi za kundi hili la muziki kutoka huko Kusini mwa Birmingham, England. Kundi hili lilikua na vichwa kama vile Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan

Mwanzo wa kundi hili….
Wana kikundi hicho walikua marafiki tangu wakiwa shuleni na Ugumu wa maisha walio kua nao ndio uliosababisha kuunanisha vipaji vyao na kutengeneza kikundi hicho ili kufanya muziki na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini waliokua nao.

Jina la Ub40 lilikuja kutokana  na wananchi wa Uingereza kutoa waraka wenye kurasa 40 uliohusu mafao yao ya afya na ajira . hivyo basi kundi hili likaamua lijiite Ub40.

Brian Travers alijiunga na kundi hilo akiwa na zana yake ya Saxophone huku wengine wakija na magitaa. Na mara walianza kubandika mabango katika mitaa ya Uingereza wakitangaza bendi yao.

Wimbo wao wa kwanza  ulisikika  katika Ukumbi wa The Hare na Hounds Pub Februari 1979 katika shereh za kuzaliwa rafiki yao.  Chrissie Hynde ndiye aliye waona vijana hao wakiimba katika ukumbi mmoja ndipo alipoamua kuwafadhili na kuwapa nafasi ya kurekodi wimbo wao wa kwanza “King/Food for Thought” wimbo  ambao ulishika  nafasi ya 4 katika chati za muziki nchini humo.

Albamu yao ya kwanza iliitwa “Signing Off” wakimaanisha wanayamaliza malalamiko yao ya ukosefu wa ajira  na mafao ya afya. Albamu hii ilizinduliwa rasmi Agosti 1980.
Ikumbukwe kua mnamo mwaka 2010 mahakama ya Uingereza ilitangaza kuwa UB40 imefilisika. Kufilisika kwao kumekuja baada ya wanamuziki wane kina Jimmy Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan kushindwa kulipa madeni yao ya kodi. Kundi hili ndilo kundi linalotajwa kuwahi kuuza nakala nyingi duniani katika nyanja ya Muziki.

Japo kwa ufupi nmeweza kukupatia historia ya Kundi  hili amabalo liliwika mno miaka ya nyuma.

Continue Reading

Cellebz

Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica

Published

on

Linapotajwa jina la wimbo wa “Neria” basi kila mmoja wetu atakua na mawazo mawili tofauti ambayo yote humuongelea Nguli wa muziki wa Kiafrica na sio mwingine ni Oliver Mtukudzi kutoka kule Zimbabwe kwa mbabe Robert Mugabe.
Jina la utani huwa wanamuita “TUKU” ambapo jina hilo limetokana na jina Mtukudzi hivyo akaamua kufupisha jina lake hilo na kupata hiyo a..ka. amezaliwa mnamo 22 Septemba 1952 mjini Highfield, Harare) ni mwanamuziki wa Kizimbabwe. Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.

Nyimbo ya kwanza ilikuwa “Dzandimomotera” iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki. Anafurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. Oliver ametoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata zingine hawezi kuzikumbuka.

Filamu alizoshiriki:

Jit (mwong. Michael Raeburn , 1990)
Neria (mwong. Goodwin Mawuru, imetungwa na Tsitsi Dangarembga, 1993). Mtukudzi ndiyo alikuwa nyota wa filamu na yeye ndiye aliotengeneza nyimbo ya filamu.
Shanda (mwong. John na Louise Riber, 2002, rev. 2004)

Tuzo alizowahi kushiriki na kushinda.

Tuzo ya KORA kwa ajili ya matayarisho mazuri ya nyimbo yake ya Ndakuwara mnamo mwaka wa 2002
Tuzo ya National Arts Merit (NAMA) mnamo mwaka wa 2002 na 2004 kama kundi bora la muziki/ mwanamuziki bora wa kiume
Tuzo ya KORA kama mwanamuziki bora wa kiume wa Africa na tuzo ya Lifetime Achievement mnamo mwezi Agosti wa mwaka wa 2003
Tuzo ya Reel kama lugha bora ya Kiafrica mnamo wamaka wa 2003
An honorary degree from the University of Zimbabwe in Desemba 2003
Tuzo za M-Net Best kama nyimbo bora ya filamu mnamo 1992, kwa ajili ya filamu ya Neria.

Continue Reading

Cellebz

Lucky Dube, Mkali wa Raggea ambaye aliwahi kuishi.

Published

on

Ninapo litaja jina la Lucky Dube ni wazi kwamba utakua unafahamu moja kwa moja namzungumzia nani. Ni moja kati ya wana harakati walio tetea haki za wanadamu hasa watu weusi walio kuwa wakibaguliwa na kuonewa kila siku kupitia sanaa ya Muziki. Kupigania Uhuru wa Africa kutoka mikononi mwa makaburu. Leo nitakupatia Historia kamili ya Mkali Huyo ikiwa ni pamoja na Historia ya maisha yake tangu kuzaliwa, safari yake ya Muziki, harakati za kupambana na Ubaguzi ulimwenguni….
Maisha yake ya Awali.
Jina lake kamili ni Lucky Philip Dude, na alizaliwa mnamo 3 August 1994 huko nchini Africa ya kusini katika eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama Mpumalanga, awali eneo hilo lilijulikana kama Eemelo. Wazazi wake walitengana kabla ya Luck Dube Kuzaliwa, hivyo Lucky alilelewa na mama yake. Mama yake alimuita jina la LUCKY baada ya kuteseka muda mrefu bila kupata ujauzito hivyo akampatia mwanae huyo jina la LUCK(Bahati).
Akiwa na ndugu zake Thand na Patricky, Dube alikua akiishi na Bibi yake ambae ni mzaa mama kipindi chote cha udogo wake wakati mama yake akiwa kazini. Moja kati ya interview aliyo fanyiwa mnamo mwaka 1999, alieleza kwamba bibi yake ndie Kipenzsi chake, ambae alipigania yeye kuwa yeye leo hii.
safari yake ya muziki ikaanza.
Akiwa bado mdogo, Lucky alikua akifanya kazi kama gardener ila alipo kuwa mkubwa aligundua kuwa kazi ile haikuwa ya kumpatia kipato ambacho kingewezsa kutosha kuilisha familia yake, na ndipo akaamua kuanza shule ambapo shuleni huko alijinga na Kwaya na kuanza kuimba katika kwaya.
Wakati akiwa shuleni huko pia alikutana na marafiki zake ambao kwa pamoja waliamua kuunda kundi lao la muziki ambalo waliliita skyway Band. Akiwa na umri wa miaka 18, alijiunga na Band ya Binamu zake iliyo julikana kwa jina la The Love Brothers ambalo lilikua likipiga muziki aina ya Zulu Pop music wakati huo wakifanya kazi katika machimbo ya Dhahabu huko Midrand wakiwa kama walinzi na wapishi wa eneo lile.
Kundi lile lilipata deal la kusign katika Record label ya “Teal Record Company” na hapo walipewa nafasi ya kurekodi ngoma zao ingawaje Lucky yeye bado alikua bado yupo shule ila alikua akiingia studio kipindi alipo pata likizo. Walifanikiwa kutoa Album yao ya kwanza iliyopewa jina la “Lucky Dube and the supersoul”. Na ikumbukwe kwamba wakati ule ule ndio mda ambao Luck Dube alianza kujifunza Kiingereza.
Lucky ana hamia kwenye Reggea.
Kipindi Album yake ya Tano ikitoka(Mbaqunga), Dave Saga ambaye badae alikuja kuwa sound Engineer wa lucky Dube alimshauri Luck Dube kuacha zile Element alizo toka nazo kule kwenye band aliyo kuwako na Kuanza kurekodi Album zake zote zilizo fuata kwa Jina la Lucky Dube. Wakati huo Dube aligundua kwamba mashabiki wake walikua wakionyesha muitikio pale alipo kuwa akiimba nyimbo za rege katika matamasha yake. Ambapo alikua akivutiwa sana na Wasanii kama vile Peter Tosh pamoja na Jimmy Cliff wote walikua wakicheza rege. Aliona kwamba zile socio-political messages zilizo kuwa zsikkimbwa katika Jamaican Rege zingefaa kabisa katika jamii ya kibaguzi aliyo kuwa akiishi yeye Lucky Dube.
Aliamua kuazisha aina nyingine ya muziki(Rege) na alifanikiwa kutoa album iliyopewa jina la Rasters Never Die na album hiyo haikuuza sana kama ilivyo tarajiwa kwani iliuza kopi 4000 ukilinganisha na ile ya Mbaqunga iliyo ulaza Kopi 30,000. Album hiyo ilifungiwa mnamo mwaka 1985 enzi za Ubaguzi kutokana na mashairi ya Nyimbo za Album(hasa katika ule wimbo ulio julikana kwa jina la “War and Crime”) hiyo kuchoma vikali serekali ya Makaburu walio kuwa wakiongoza Africa Kusini kwa kipindi kile.
Ingawaje hakukata tamaa ila aliendelea kutengeza ngoma za rege na baadae aliachilia Album ya pili iliyo pewa jina la “Think About the Childrean”, album iliyo vunja Rekodi ya mauzo na kumfanya Lucy Dube kuwa mwana muziki maarufu wa Rege Africa na Ulimwenguni kote.
Biashara na mafanikio katika muziki.
Lucky Dube aliendelea kutoa album kali zilizo uza kwa wingi, na mno mwaka 1989 alifanikiwa kushinda Tuzo Nne(4) tuzo zilizo julikana kwa jina La “OKTV awards” kupitia wimbo wake wa Prisoner na baadae tena kuchukua tena tuzo nyingine kupitia Cuptured life mwaka ulio fuatia na baadae kuchukua tena tuzo mbili kupitia ngoma yake ya House of Exile. Album yake ya Victims iliuzsa zaidi ya kopi milion moja ulimwenguni kote na mnamo mwaka 1995 alipata dili la kurekodi akiwa na Motown Records.
Mnamo mwaka 1996 aliachia Albu yake iliyo mfanya kuwa juu zaidi album iliyo pewa jina la “Serius Reggae Busness”, Album iliyo mfanya kujulikana kama Mwanamuziki aliyefanya mauzo Mengi ya Juu na msanii bora wa kimataifa. Album zake zote tatu zilizo fuatia zilifanikiwa kuchukua tuzo Huko Bondeni kwa Mzee Madiba.
Kifo na Mauti.
Mnamo tarehe 18,October-2007, Lucky Dube ali uawa kwa kupigwa Risasi akiwa njiani kuwapeleka wanawe wawili kwa mjomba wao. Taarifa zilizo toka kuhusiana na Kifo chake ni kwamba,, majambazi walikuwa wakitaka kumpora gari lake hilo la Kifari aina ya Chrysler 300C. Watu watano walikamatwa kwa kuhusishwa na kifo cha Dube na watatu kati yao walipatikana na hatia na Kuhukumiwa Kifungo cha maisha Gerezani.

Na huo ndio mwisho wa Makala yangu kwa leo tafadhali nitaomba unipatie maoni amba ushauri wako kupitia anwani yangu ya mtokambali2015@gmail.com ama namba yangu +255767322193(WhatsApp only).Pia nitoe shukrani zangu kwa WIKIPEDIA kwa kufanikisha kuandika Makala hii

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 mtokambali.com