About

Karibu Mtokambali, nafurahi kukuona hapa,
Naitwa Francis Paul Mawere, Ni mmiliki na mwandishi wa Blog hii mtokambali.com.Kiasili nimetokea katika ardhi ya Mlima kilimanjaro(Najivunia kwetu) ni MTANZANIA halisi mwenye umri wa miaka Kadhaa. Nimekua nikifanya Full time blogging tangu nilipo hitimu chuo Miaka kadhaa huko nyuma..

Je mtokambali.com ni kwa ajili ya Nani?

Dhamira kuu ya kuanzisha blog hii ni kuijenga jamii inayo nizunguka na hasa vijana wenzangu ambao mara nyingi wameonekana wakipotea katika mambo yasiyo na tija.
Nilipo kua chuonio niliweza kuyaona matatizo mengi yanayoikumba jamii iliyo kuwa ikinizunguka kwa wakati ule hasa vijana wengi walio kuwa na matatizo mbali mbali kama vile ULEVI, ZINAA, UVIVU na mambo mengi lukuki na tangu hapo ndipo nilipo amua kuifungua blog hii ya MTOKAMBALI kwa ajili ya vijana wenzangu. Naamini kabisa tutaburudika na tutaelimika kama utakubali kubadili mtazamo wako mbovu na fikra zako potofu juu ya maisha haya kupitia blog hii.

Kwa nini nakuambia chagua MTOKAMBALI.

1. Kwanza kabisa utahabarika na kuelimika
2.Utapata kufahamu yale mambo ambayo hukuyajua toka mwanzoni.
3.Uta hamasika
4. Fikra chanya na mchanganuo wa mambo.
5.Hakuna Upendeleo.

Kuna nini cha Muhimu mtokambali.com?

Kama nilivyo eleza hapo juu, kwamba Blog hii ni kwa ajili ya mambo yahusuyo maisha ya jamii zetu zinazo tuzunguka na kama tunavyo fahamu idadi ya watu walio wengi katika jamii zetu ni Vijana, hivyo tumejikita zaidi kwa vijana.
Mambo yazungumzwayo hapa ni yale Mambo yahusuyo, MAISHA kwa ujumla wake(Yaani, Afya&Chakula, Mapenzi&Jinsia, Burudani, Ujasiriamali na Tecknolojia).

Haya ndio baadhi ya Machapisho yetu hapa mtokambali.com

Hayo ni baadhi tuu ya machapisho yaliyopo Humu ndani mtokambali.com. Kwa taarifa yako tuna zaidi ya machapisho 600 humu ndani hivyo ni wewe tuu ushindwe kdadavua mambo.

Naamini!

Kufanikiwa katika maisha siyo kuota tuu ndoto kila siku yakua iko siku utapata, laa hasha… Muda ulio nao wewe ni mchache mmno, hivyo unapata picha kwamba, ule Muda wa kuishi maisha ya ndoto zako ni leo na sio kesho tena maana hakuna anaye ijua kesho.