Tangazo

Kila  siku tunasikia jinsi mwanamke alivyo na nafasi kubwa katika kuharibu ama kujenga nyumba yake , NDOA.

Ni kweli kwamba mwanamke anaweza kubomoa nyumba yake mwenyewe ikiwa hatoweka juhudi za kutosha katika kuiboresha na kuiimiarisha. Ila tukiangalia hili swala bila upendeleo, ukweli ni kwamba mwanaume ana nafasi kubwa sana ya kumuwezesha mkewe kuwa mjenzi au mharibifu wa nyumba yao!!!

Kwa kina baba mnaodhani small house ndio suluhisho la matatizo yaliyopo majumbani mwenu hua mnakosea sana kwasababu hamtatui tatizo bali mnaongeza matatizo juu ya matatizo.

Visingizio vikuu kwa wale wanaoamua kutafuta ‘FURAHA’, ‘AMANI’ na ‘FARAJA’ ya mpito ni kwamba small house  yeye hanuni.. mapokezi anayotoa ni mazuri….anapendeza wakati wote…mapenzi anatoa yote…heshima na maelewano vinakuwepo  wakati wote (n.k), kinyume na maisha yalivyo nyumbani.

Hivi unajua kwanini kunakuwa na tofauti kati ya nyumbani kwako, mke na mchepuko? Kwasababu hata mnayofanya huko kwa mchepuko ni tofauti na mnayowafanyia wake zenu!

Unakuta mtu nyumbani kwake akiombwa pesa ya ada, matumizi  ya nyumbani ama ya matumizi binafsi ya mkewe anafoka kwamba hana pesa ilhali kwa nyumba ndogo analipa kodi…gari yake anaweka mafuta ….shopping anamfanyia teza kwa gharama kubwa tu  na matatizo yake mengineyo anamtatulia!

Small house unaenda kwake ukiwa mpole. Hufiki na kuanza  kumkemea, kugomba  au kumkaripia.  Hapo bado kila anachotaka unampatia bila utata, sasa akasirike kwa kitu gani? Ukifika huko unaita sweety…baby sijui darling na majina mengine matamu tamu kwa kubembeleza, anune nini??? Ukifika kwako ni ‘we mama nanii kuja hapa”….mara sijui fanya hivi fanye vile kwa ukali kama vile unamuamrisha mtoto, tena mtoto mwenyewe wa kambo na wewe  baba mkorofi wa kambo.

Small house hakulelei watoto wala hakuaangalizii nyumba kila uchao na kujali familia yako kuanzia mama mpaka wadogo zako, na wala hana mawazo yanayohusiana na maendeleo yenu ya kifamilia kwasababu in the long run wewe nae lazima mpishane njia kwahiyo anakuwa relaxed  na anapata muda zaidi wa kujijali yeye mwenyewe ndio maana kila saa kapendeza. Tena usisahau wewe unavyompendezesha kwa kumpeleka shopping bila kusahau pesa za saloon zisizoisha kuombwa! Mara ya mwisho mke wako umemnunulia hata underpants ni lini??? Kitambo sana I bet!!

Anyway, point yangu ni hivi, BADILIKA.

Huwezi kulalamika mtu ananuna tu muda wote kama hujampa kitu cha kufurahia unapokuwa karibu, au hakupokei vizuri ikiwa mwenyewe ukifika getini tu unageuka simba. Upole, utaratibu, na upendo wako wote unakuwa kwaajili ya watu wengine na sio mke. Hapo  lazima nae atakua katika hali ya woga na kukosa amani!! Kucheka atacheka pindi haupo au akiwa na kampani ya watu wengine.

Kuwa mzuri kwa mke wako, acha kurudi nyumbani na magadhabu maana hayo ndio yanayotengeneza tension kati yenu. Kuwa mpole na mkarimu kwa mkeo.

Acha kumkaripia na kumgombeza kama mtoto. Ikiwa amekosea zungumza  nae kama mtu mzima mwenzako.

Muonyeshe upendo kama unaodhamiria kuuonyesha au tayari unauonyesha huko kwa small house.

Mjali ….kama unaona hajijali sana mshawishi kufanya hivyo….mpeleke shopping mwenyewe..msukume ajiweke safi na katika hali ya kuvutia.

Kwa wakina mama/dada na sisi tusijisahau jamani!! Mpe mwenzio sababu ya kuwahi nyumbani na kutaka kuwa karibu na wewe. Sio mtu akiona muda wa kazi umeisha anahema kama katwishwa mzigo hata hamu ya kurudi nyumbani hana!

 

AdvertisementMtokambali 728x90