Calisah hafai kuwa model - Daxx Cruz
Tangazo

Mwanamitindo maarufu wa Tanzania ambaye shughuli zake kwa sasa anazifanyia nchini Afrika Kusini, Daxx Cruz amefunguka na kutaja vigezo vya mtu anayestahili kuwa mwanamitindo ‘model’, na kutaja baadhi ya ‘models’ wa Bongo wasiokuwa na vigezo

Daxx aliyekuwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa kituo cha EATV kila Jumatano, amemtaja model anayefahamika kwa jina la Calisah ambaye siku za karibuni alijipatia umaarufu baada ya kutangaza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo Wema Sepetu, kuwa hastahili kabisa kufanya kazi hiyo kwa kuwa hana vigezo.

Kuhusu models wa kiume amesema  “Upande wa models wa kiume, siwajui, mi nawaonaona tu, mtu pekee nayemkubali anaitwa Abel, saizi yuko South Afrika, lakini wengine wapowapo tu….”

Alipotajiwa majina ya models watatu (Rota, Calisah na Mario, haya ndiyo yalikuwa majibu yake…

“Rota Molel ana muonekano mzuri lakini ana attitude, kile ndicho kinachomuangusha, ni model mzuri lakini atitude…

Calisah NO, ni mfupi, for me No, labda kw Tanzania, unajua model siyo kuwa na six packs, akija South hapati kazi…..

Mario (ambaye amewahi kuwa Mr. Tanzania, kwangu No”

Mario – Mr. Tanzania 2010

Mwingine ambaye hana vigezo, Daxx amemtaja mwanadada Hamisa Mobeto kuwa hastahili kuwa ‘model’ kwa kuwa amekaa kiurembo zaidi na kwamba anafaa kwa kazi ya kuonekana kwenye video za miziki (Video Vixing) hivyo kutokidhi vigezo vya kimataifa vya kuwa ‘model’ labda kwa Tanzania.

Hamisa
Hamisa

Amewataja baadhi ya watu ambao anadhani kuwa ni ‘models’ wazuri na ambao endapo watakaza, watafika mbali kuwa ni pamoja na Nelly Kamwelu kama mtu anayemkubali huku akitaja kasoro kubwa inayowakwamisha wadada wengi Tanzania

Wadada wengi wako freshi, tatizo wanajiachia wanafanya maisha ya uanamitindo kuwa kitega uchumi”

Baada ya kutajiwa baadhi ya majina, Daxx amewachambua kama ifuatavyo

“Nelly ni mzuri nampa 80%….. Eligiva for now NO, zamani alikuwa okay, saizi yuko na familia yake, maisha yamebadilika….. Hamisa Mobeto kwa Tanzania Yes, but nje ya Tanzania NO, labda kwa video vixing sababu ya muonekano na height yake, amejikita sana kwenye urembo, modeling siyo urembo ……

Nelly

Pia Daxx ametaja model watatu wa kike ambao anawakubali zaidi Bongo na anaona ni pesa sehemu yoyote watakapokwenda kuwa ni pamoja na Alexia, Zuhua Goa na Batuli

Akitaja baadhi ya vigezo anavyotakiwa kuwa navyo ‘model’ amesema ni pamoja na muonekano wa mwili ambao haujalishi sura nzuri, urefu wala wembamba, pia tabia nzuri ni kitu muhimu sana.

“Kuwa model siyo lazima uwe mwembamba, licha ya kuwa ni kigezo kimojawapo, hata mimi siyo mwembamba lakin uhalisia katika muonekano ndilo suala la msingi, pia urefu siyo kigezo sana maana unaweza kuwa mrefu lakini hauna mvuto wa kibiashara, Unaweza kuwa mtanashati lakini kazi inakuja inataka mtu mwenye sura kama analia, utafanyaje, kila kiungo cha mwanadamu ni biashara, models wengi Bongo wanajiweka vizuri juu lakini kwa chini hakuna kitu… tabia nzuri na nidhamu pia ni muhimu, model lazima pia uwe na tabia nzuri isiwe tu muonekano” Amesema Daxx

Pia ametoa ushauri kwa wabunifu (ma-designer) ambao ndiyo mara nyingi huwatumia mamodel katika kazi zao kufanya mambo matatu muhimu ili kuinua sekta wa wanamitindo nchini.

Mambo hayo ni pamoja na kuwalipa vizuri ‘models’, kupunguza kutoa kazi kwa kuuana pamoja na kuongeza ukaribu kati yao na ‘models’

 

Credits To EATV.TV
AdvertisementMtokambali 728x90