Tangazo

Crime of passion ni pale mtu anapofanya kosa kutokana na hisia kali (hasira, maumivu, uchungu, aibu n.k) haswa katika mahusiano ya kimapenzi.

Kila siku wanaume kwa wanawake wanatoka nje ya mahusiano yao bila kujua au hata kujali sana kitakachotokea ikiwa watafumaniwa/gunduliwa na wenzi wao. Kama baadhi yetu tunavyoimba kila siku kwamba “Cheating is BAD” ndivyo nao wanavyoimba kwamba “Cheating is NECESSARY/INEVITABLE”. Wanatoka nje ya mahusiano yao bila kufikiria wala kujali matokeo yake kwao binafsi, watoto kama wanao na wenzi wao kwa visingizio vya “nature haikubali niwe na mwanamke mmoja, mume/mke wangu haniridhishi/ mwenzangu hanijali “n.k.

Matokeo mabaya ya kucheat ni pamoja na kumuumiza mwenzi, kupeleka magonjwa (ya moyo/kiakili na kimwili kwa ujumla) kwa aliyetulia nyumbani, kuzaa mtoto ambae anaweza asikubaliwe na mwenzi hata kuishia kunyanyaswa, kuwakosesha watoto malezi wanayostahili, mahusiano/ndoa kuvunjika na kubwa zaidi ambalo sidhani kama watu hua wanalifikiria sana. . . nalo ni kuuwawa au hata kuumizwa sana  pale atakapokamatwa.

Hizi kesi ambazo mtuhumiwa anakua amefanya kosa (laweza kuwa ni la kuua, kubaka au kumpiga hata kumuumiza mwenzake) kutokana na hisia kali sana za mapenzi au hasira  baada ya kufumania  huitwa Crimes of passion. Je na wewe uko tayari kuwa victim wa hili baada ya kumfanya mwenzio victim wa kudanganywa?

Mwaka juzi tu tulisikia  hapa kwetu mwanaume alichomwa kisu na mwanamke wake wa nje baada ya kugundua kwamba kuna mchepuko mwingine zaidi yake, kuna mama wa kiMarekani (Clara Harris ukipenda kumgoogle) yeye alimgonga mume wake kwa gari mara kadhaa baada ya kumkuta hotelini na mwanamke mwingine, Zimbabwe kuna mwanaume alimchoma mkewe kisu. . akachinja mtoto mwenye umri wa siku mbili ambae alikua wa mwanaume mwingine kabla nae hajajitundika. Na hivi majuzi tu kulikuwa na kesi ya mwanamke kuuwawa kama mnyama na kuwekwa kwenye diaba/jaba hapa Dar alafu ikaja kugundulika kuwa aliyemuua ni mume wake baada ya kugundua kwamba mkewe alikuwa akitoka nje ya ndoa yao na mwanaume mwingine.

Haya ni madhara makubwa zaidi tofauti ya yale tuliyozea/wahusika wanayotegemea kama ndoa kuvunjika, kupigwa, kuzalilishwa n.k kwasababu yanahusu kuondoa maisha ya mtu au hata mtu zaidi ya mmoja. Je wewe kama ni mmoja wa wanaotoka nje ya ndoa/mahusiano yake unadhani hicho unachopata huko nje ya ndoa/mahusiano yako kina thamani sawa na maisha yako wewe au ya mtu mwingine yeyote yule? Kama kina thamani kiasi hicho kwanini usiachane na maisha uliyonayo ukaenda kuanza upya huko unakopata hicho/hayo yaliyo muhimu zaidi?

Binafsi napinga sana kitendo cha mtu kutoka nje ya mahusiano yake kwa sababu yoyote ile. . tena baada ya kushuhudia mtu ambae alijitahidi kuwa mke mtulivu akiletewa UKIMWI nyumbani kwake, ugonjwa ambao unaweza ukafupisha maisha yake iwapo muhusika akishindwa kukubali hali hiyo na kuzidiwa na msongo wa mawazo. Ofcourse, napinga sana kitendo cha watu wanaojichukulia sheria mkononi na kutoa uhai wa binadamu mwingine kwasababu ya mapenzi lakini wote tunapaswa kujiheshimu na kuheshimu wenzi wetu pale tunapokuwa tumeamua kuwa kwenye mahusiano. Tunapaswa tujionee huruma, tuwaonee wake/waume/wapenzi/watoto na ndugu zetu huruma. Badala ya kutaka kuendelea kuwepo huku na bado uwepo kule, ukiona mambo yamekufika shingoni, nyumbani hakukaliki, huna mapenzi na uliye nae tena jiweke huru ili umuweke na mwenzio huru pia.

JALI, CHUKUA HATUA!

 

 

AdvertisementMtokambali 728x90