Connect with us

Health

Fahamu kuhusiana na Ugonjwa wa Kipindupindu, Dalili zake na jinsi ya kujikinga

Published

on

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “Vibrio cholera”.

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “Vibrio cholera”.

CHANZO CHA UGONJWA

Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu.
Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi cha mtu bila yeye binafsi kuonyesha dalili zozote za ugonjwa.

DALILI ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.
Mgonjwa wa Kipindupindu huwa na dalili zifuatazo:

Kuharisha mfululizo au mara kwa mara bila tumbo kuuma ambako kunaweza kuambatana na kutapika.
Kinyesi au matapishi huwa ya maji maji yasiyo na harufu, yanayofanana na maji yaliyooshewa mchele.
Kusikia kiu sana, macho kudidimia na ngozi kusinyaa ambavyo hutokana na upungufu wa maji mwilini.
Kuishiwa nguvu, kuhema haraka haraka na kulegea. Hali hii hutokana na upungufu wa maji na madini mwilini.

KIPINDUPINDU KINAVYOENEA.

Kula chakula au kunywa kinywaji chochote kilicho na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa mfano:-

Kunywa maji yasiyochemshwa.
Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira ambayo siyo safi.
Kula matunda yasiyooshwa kwa maji safi na salama.
Kunywa pombe za kienyeji zilizoandaliwa katika mazingira machafu au kunywea katika vyombo vichafu.
Kula mboga za majani, kachumbari na saladi bila kupikwa au kuziosha kwa maji safi na salama.

Kula chakula au kumlisha mtoto bila kunawa mikono kwa sabuni na maji safi na salama yanayo tiririka.
Kuosha au kuhudumia mwili wa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa kipindupindu bila kujikinga.
Kunawa mikono kwenye chombo kimoja kwa mfano ndani ya bakuli au beseni kabla ya kula chakula.
Kutotumia choo au utupaji ovyo wa kinyesi.
Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni.
Kuweka mazingira katika hali ya uchafu mfano kutupa taka ovyo bila kuzingatia kanuni za afya..
Kula vyakula vilivyopoa na visivyofunikwa.
Kutiririsha maji ya chooni ardhini na hivyo kusababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji na chakula.

Inzi huchangia kueneza ugonjwa wa kipindupindu kwa tabia zake za kutua chooni kwenye kinyesi, uchafu na hata vyakula na vinywaji.

MADHARA YA KIPINDUPINDU

Hofu miongoni mwa jamii katika sehemu yenye mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Kifo kutokana na ukosefu wa maji na madini mwilini baada ya kuharisha na kutapika sana.
Kushuka kwa uchumi kutokana na familia/jamii kuacha shughuli za uzalishaji mali ili kumuhudumia mgonjwa na kushiriki katika misiba.
Serikali hutumia fedha nyingi kwa ajili ya dawa, posho kwa watumishi katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

JINSI YA KUJIKINGA NA KIPINDUPINDU

Kujenga choo bora na kukitumia Ipasavyo
Kufunika tundu la choo na kufunga mlango baada ya matumizi yake.
Kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni baada ya:.

– kutumia choo.
– kumtawaza mtoto na kabla ya kula au kumlisha motto.

Kula chakula kikiwa bado moto na kufunika chakula kilichoandaliwa tayari kwa kuliwa.
Kunywa maji yaliyochemshwa na kuhifadhiwa katika chombo kisafi na salama.
Kusafisha vyakula vinavyoliwa vibichi (kama vile matunda na mboga) kwa kutumia maji safi na salama yanayotiririka.
Kuhakikisha usafi wa mazingira ya vilabu/baa, wahudumu na vyombo vitumikavyo. Pombe za kienyeji ziandaliwe kwa maji yaliyochemshwa.
Weka mazingira katika hali ya usafi.
Kumbuka, kuchuja maji yaliyochemshwa kunaweza kuchafua maji kwa kuingiza vimelea.Hivyo, chuja maji kabla ya kuyachemsha.

KUHUDUMIA MGONJWA
Mgonjwa wa kipindupindu hupoteza maji mengi na madini muhimu mwilini anapoharisha na kutapika. Ili kuokoa maisha ya mgonjwa ni muhimu kuchukua hatua zifuatazo:

Mpe mgonjwa dawa ya mchanganyiko wa sukari na chumvi(ORS), maji, uji mwepesi, supu nk. mara kwa mara.
Mpeleke mgonjwa haraka iwezekanavyo katika kituo cha afya/zahanati/ hospitali au kituo cha kutibu kipindupindu kilicho karibu nawe.
Matapishi na kinyesi cha mgonjwa ni hatari kwa afya yako. Kwa hiyo nguo na vitu vingine vilivyochafuliwa na mgonjwa vilowekwe kwenye kemikali maalumu (mfano Jik) au vichemshwe ili kuua vimelea vya kipindupindu na kasha visafishwe kwa sabuni.
Ndugu waliokuwa wakiishi na mgonjwa au wale wanaomhudumia wahakikishe wanapata dawa za kinga dhidi ya kipindupindu.

Angalizo:
Ni lazima wakati wote kuwa msafi ili kuzuia vimelea vya ugonjwa visiingie kinywani kwako kwa njia zilizotajwa hapo juu.

Tahadhari:
Maiti ya mgonjwa wa kipindupindu ni hatari, usijishughulishe na kuosha maiti hiyo bali izikwe haraka kwa kufuatwa ushauri wa wataalam wa afya.

But I must explain to you how all this mistaken idea of denouncing pleasure and praising pain was born and I will give you a complete account of the system, and expound the explorer of the truth, the master-builder of human happiness. No one rejects, dislikes, or avoids pleasure itself, because it is pleasure, but because those who do not know how to pursue pleasure rationally encounter consequences that are extremely painful.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Health

Fahamu kuhusu njia Uzazi wa mpango, Faida na Madhara yake

Published

on

Sura hii inajadili njia mbalimbali za kuzuia mimba au kupanga muda wa kupata mimba nyingine. Njia zote ambazo zimeelezewa katika sura hii hutumika sehemu zote duniani.

Kwa nini uzazi wa mpango?

Kuna njia nyingi salama na zenye uhakika za kuzuia mimba, au kukusaidia kuchagua lini upate mtoto na idadi ya watoto ungependa kuzaa. Unaweza kupata njia za kuzuia mimba zenye gharama nafuu au zisizo na malipo kabisa kutoka kliniki za uzazi wa mpango katika mazingira yako ya kawaida. 

Uzazi wa mpango hujulikana pia kama kama njia ya kudhibiti uzazi. Haijalishi maneno gani ambayo yanatumika, uzazi wa mpango una manufaa mengi:

 • Kuzaa idadi ndogo ya watoto ni bora zaidi kwa afya ya mwanamke kuliko kuzaa watoto wengi. Kwa kutumia njia ya uzazi wa mpango, unaweza kuamua lini mwili wako uko katika hali nzuri kiafya kubeba mimba.
 • Kuvuta subira katika uzazi na kuacha muda wa kutosha kati ya mtoto mmoja na mtoto mwingine hukuwezesha kuwaandalia watoto utakaowazaa maisha ya uhakika, na kukupa muda zaidi, nguvu, na fedha kwa ajili ya kuwahudumia watoto ambao tayari unao.
 • Kuamua kama unataka kupata watoto na lini, bila watu au mtu mwingine kukuamrisha kupata mimba au usipate mimba: kuchukua hatamu ya maisha yako.
 • Kufurahia tendo la kukutana kimwili bila kuwa na wasiwasi wa kupata mimba kama wewe na mwenzako hamtaki au hamjawa tayari kupata mtoto.
 • Uzazi wa mpango huwasaidia wanawake kuepuka utoaji mimba usiyo salama, tatizo ambalo husababisha vifo vya maelfu ya wanawake kila mwaka.

Uzazi wa mpango, tendo la ngono, mimba — wakati mwingine ni mambo magumu kuyazungumzia. Kitabu cha Hesperian kijulikanacho kama Juhudi za afya kwa wanawake (Health Actions for Women) kimependekeza njia za kuwawezesha wanaume na wanawake kuuzungumzia uzazi wa mpango na masuala mengine ya afya ya wanawake.

Baadhi ya watu hupenda kuzaa watoto wengi-hasa watu wa kawaida na mara nyingi wenye hali duni (baadhi ya watoto kufariki wakiwa wadogo) kwa sababu watoto husaidia kufanya kazi na kuwatunza wazazi wao wanapozeeka.

Hali ni tofauti katika nchi zenye mgawanyo mzuri wa rasilimali na manufaa yatokanayo. Mahali ambapo ajira, makazi, na huduma za afya vinapatikana kwa urahisi zaidi, na mahali ambapo wanawake wana fursa sawa na wanaume kielimu, ajira, na katika kuendesha maisha yao, watu mara nyingi huchagua kuwa na familia ndogo. Sababu ni kwamba, kwa kiasi fulani, hawahitaji kuwa tegemezi kwa watoto wao kiuchumi, na wana imani kubwa zaidi kuwa watoto wao wataishi maisha bora kiafya, kijamii na kiuchumi.

Watu hutumia njia za uzazi wa mpango ikiwa:

 • Inatolewa kwa gharama nafuu au bila malipo.
 • kuna njia za uzazi wa mpango tofauti ili watu waweze kuchagua njia ipi inayowafaa.
 • hakuna mtu anayeshinikizwa au kulaghaiwa kutumia njia hiyo ya uzazi wa mpango.
 • wanaume wanaelewa na kuamini manufaa ya uzazi wa mpango, na kuwasikiliza wanawake wanachotaka.
 • mtu yeyote ambaye anataka kutumia uzazi wa mpango anaweza kuipata huduma hiyo kwa urahisi, wakiwemo vijana au watu wazima, ambao wameolewa na hawajaoa au kuolewa, na watu wenye ulemavu.

Uzazi wa mpango ni kwa ajili ya nani ?

Baadhi ya watu hufikiri kuwa uzazi wa mpango ni kwa ajili ya wanawake walioolewa tu. Lakini wanawake wengi ambao wameoolewa na hawajaolewa hufanya tendo la ngono, na wengi wanataka kufurahia tendo hilo bila kuwa na wasiwasi au uoga wa kupata mimba. Vilevile, wanawake mara nyingi huwa hawana maamuzi ya mwisho juu ya tendo la ngono. Baadhi hushinikizwa au kulazimishwa. Hata hivyo, bila uzazi wa mpango, mwanamke yeyote, aliyeolewa au hajaolewa, mwenye umri mdogo au mkubwa, anaweza kupata mimba. Ukiwa mfanyakazi wa afya au katika nafasi yotote ya uelimishaji, ni muhimu kueneza elimu ya uzazi wa mpango kwa wanawake wote.

Unapaswa pia kutafuta njia za kuwapa elimu wanaume juu ya uzazi wa mpango. Baadhi ya njia za uzazi wa mpango, mfano kondomu, huhitaji azma ya wanaume. Na mara nyingi mwanaume hutarajiwa kuchangia uamuzi juu ya njia ya uzazi mwenzi wake atakayoitumia. Kuwasiadia wanaume kuelewa manufaa au faida za uzazi wa mpango huwasaidia kuondokana na wasiwasi wao juu ya njia husika na kuelewa jinsi uzazi wa mpango unavyowasaida pia.

Kuwapa elimu wanaume juu ya uzazi wa mpango pia humrahihishia mwanamke kuongea na mume au mwenzi wake juu ya uzazi wa mpango na na kuamua njia ipi watumie. Kama mwanaume bado hataki kutumia uzazi wa mpango hata baada ya kujifunza na kuelewa faida zake, mwanamke atahitaji kuamua iwapo anapaswa kuendelea kuitumia katika hali kama hiyo. Kuna njia ambazo mwanamke anaweza kutumia bila mwanaume kujua.

Elimisha jinsi njia za uzazi wa mpango zinavyofanya kazi na nini cha kutarajia

Elezea jinsi ya kutumia njia mbalimbali za uzazi wa mpango kwa usahihi na kuwa mkweli juu ya madhara yake ya pembeni. Sababu kuu ya wanawake kuacha kutumia njia ya uzazi wa mpango ni kutokana na kero ya madhara yake ya pembeni. Lakini kama atajua mapema juu ya madhara hayo, anaweza kuwa tayari kuendelea na njia hiyo hadi madhara yatakapopungua au kuachagua njia nyingine inayomfaa zaidi.

Kuwasaidia vijana

Vijana wanaweza kuanza mahusiano ya kimapenzi au hata kingono kabla hawajajua jinsi ya kuzuia kupata mimba. Jamii zinaweza kuwasaidia vijana kupata taarifa ambazo wanahitaji ili kufanya maamuzi sahihi. Shule zinaweza kuwapatia vijana elimu ya afya ambayo inajumuisha suala la mimba. Vijana pia wanaweza kufundishwa kuwa walelimishaji rika na muda maalum unaweza kupangwa kwenye kliniki na sehemu zingine ili kuwapatia vijana unasihi na nyenzo za kuzuia mimba.

Mwanaume anapofikia kilele na kuachia shahawa ndani au karibu na uke, shahawa kutoka kwenye ume huingia kwenye mji wa mimba au kizazi cha mwanamke na kwenye njia za kusafirisha mayai ya kike ya uzazi. Kama ni wakati wa kipindi cha rutuba(kipindi cha mwanamke kushika mimba), mbegu ya kiume inaweza kuungana na yai la kike lililopevuka. Kama mbegu ya kiume itarutubisha yai hilo, basi hujibanza kwenye ukuta wa mji wa mimba(kizazi). Hapo mimba itakuwa imetunga. Njia za uzazi wa mpango huzuia mimba kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye uke, au kusimamisha mwili wa mwanamke usiachie mayai ya uzazi, au kuzuia mbegu za kiume kukutana na yai.

Njia za uzazi wa mpango

Sura hii inaelezea njia tofauti za uzazi wa mpango. Kwa ajili ya taarifa juu ya njia zingine za uzazi wa mpango, na zile ambazo hazitumiki sana

Jinsi ya kuchagua njia ya uzazi wa mpango

Njia zote tofauti za uzazi wa mpango zina manufaa na mapungufu. Ni muhimu kuongea na mwenzi wako, wanawake wengine, au mfanyakazi wa afya juu ya njia tofauti kukusaidia kuchangua njia inayokufaa. Baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuzingatia katika kuchagua njia ya uzazi wa mpango ni pamoja na:

Ina ufanisi kiasi gani katika kuzuia mimba?.
>Ina ufanisi kiasi gani katika kukinga dhidi ya magonjwa ya ngono?.
>Kama mwenzi wako anaafiki matumizi ya njia hiyo ya uzazi wa mpango, au kama unapaswa kuficha asijue.
>Kama njia hiyo inapatikana kwa urahisi, na mara ngapi unatakiwa kiutumia katika muda fulani.
>Inagharimu kiasi gani ?.
>Kama ina madhara ya pembeni.
>Kama una mahitaji na wasi-wasi mwingine. Kwa mfano: unanyonyesha? Bado unahitaji watoto zaidi ?

1.Kondomu

Kondomu ni kimfuko laini chembamba ambacho mwanaume huvaa kwenye uume wake wakati wa kufanya tendo la ngono. Shahawa za mwanaume hubaki ndani ya kondomu, na hivyo haziwezi kuingia ukeni na kusababisha mimba. Kondomu ni salama na hazina madhara ya pembeni..CONDOM uzazi wa mpango

Kondomu ni njia yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngono, ukiwemo VVU. Hata kama unatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango, unaweza wakati huohuo kutumia kondomu kwa ajili ya kujikinga wewe na mwenzi wako dhidi ya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono.

Kondomu ndiyo njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo inaweza, kwa kiwango kikubwa, kuzuia mimba na kukinga dhidi ya maambukizi kupitia ngono kwa wakati mmoja. Lakini mwanaume lazima awe tayari kutumia kondomu kila mara atakapofanya ngono.

Minya ncha ya kondomu na kuivalisha kwa kuviringisha juu ya uume uliosimama. Ncha ya chini yenye nafasi hupokea shahawa za mwanaume baada ya kuachiwa. (Kama hutaacha nafasi kwa ajili ya shahawa, kondomu inaweza kupasuka.)

Baada ya kufikia kileleni, ume ungali bado umesimama, shikilia kondomu kwa juu ili ibaki kwenye ume wakati ukichomoa ume kutoka ukeni. Baada ya hapo, toa kondomu kwenye ume. (Tupa kondomu kwenye chombo cha taka – usitupe kondomu hovyo ili watu wengine wasiiguse au kuiokota!) Tumia kondomu mpya kila mara unapofanya tendo la ngono.

 

2.Dawa za kuua mbegu za kiume (Spermicide)

Dawa za kuua mbegu za kiume kwenye shahawa zinaweza kuwa katika mfumo wa povu, vidonge, mafuta ya krimu, jeli au vidonge ambavyo huyeyuka kwenye uke na kuua mbegu za kiume ili zisiweze kurutubisha yai. Dawa za kuua mbegu huingizwa ukeni mara kabla ya tendo la ngono. Dawa haifanyi kazi vizuri ikitumika peke yake, lakini hutoa kinga zaidi dhidi ya mimba inapotumika pamoja na kondomu. Dawa za kuua mbegu za kiume hazitoi kinga dhidi ya maambukizi yanayopitia kwenye ngono au VVU.

 

3.Vidonge vya kuzuia mimba (vidonge vya majira).

Vidonge vya kuzuia mimba vina homoni ambazo zinafanana na homoni za asili kwenye mwili wa mwanamke. Huzuia mimba kwa kusimamisha ovari za mwanamke kuachia yai. Kuna aina kuu 2 za vidonge vya majira: vidonge mseto vyenye homoni 2, estrojeni na projestini, na vidonge vidogo ambavyo vina homoni moja tu ya projestini.

   Uzazi wa mpango: Kutumia vidonge vya majira.

Vidonge vya kutumia kwa njia ya mdomo kudhibiti uzazi .

Vidonge vingi vya kudhibiti uzazi hujumuisha homoni 1 au 2 zinazofanana na homoni ambazo hutengenezwa na mwili wa mwanamke. Homoni hizi zinaitwa estrojeni na projestini.Vidonge vya kudhibiti uzazi au vidonge vya majira huja vikiwa na nguvu tofauti za kila homoni na pia huuzwa chini ya majina ya kibiashara tofauti. Aina 3 za kwanza ambazo zimeoneshwa hapa chini zina homoni ya estrojeni na projestini  na aina ya 4 vina homoni moja tu ya projestini (angalia vidonge vidogo).
Aina ya homoni ya estrojeni inayotumika sana huitwa ethinyl estradiol. Dozi ya kawaida ni makrogramu 35. Kiasi cha kawaida cha homoni ya projestini kwenye vidonge mseto ni miligramu 0.1.

Wanawake wanaotumia vidonge vya majira kawaida hupata hedhi ya kila mwezi kidogo kuliko kama wangepata bila kutumia vidonge vya majira. Hili linaweza kuwa jambo zuri, hasa kwa wanawake wenye tatizo la upungufu wa wekundu wa damu (anemia). Lakini kama mwanamke hapati hedhi ya kila mwezi au hupata hedhi nyepesi (kidogo) mno kwa miezi kadhaa na hapendezwi na madhara haya ya pembeni, anaweza kujaribu aina nyingine ya vidonge vya majira vyenye kiasi kikubwa zaidi cha homoni ya estrojeni.

Vidonge vyote vya majira hufanya kazi vizuri zaidi kudhibiti mimba kama vitatumiwa katika muda ule ule kila siku. Utaratibu huo hurahihisha mwanamke kukumbuka kumeza kidonge. Ni muhimu hasa kutumia vidonge vidogo (vyenye homoni moja ya projesti tu ) katika muda ule ule kila siku kwa sababu kwa kidonge hiki, kuna uwezekano mkubwa wa kupata mimba kama mwanamke atasahau kumeza hata kidonge kimoja tu.

Kwa paketi ya vidonge vya siku 28, tumia kidoge 1 kila siku na kuanza paketi nyingine baada ya kumaliza ya kwanza. Paketi ya siku 28 inaweza kuwa na vidonge 21 vyenye homoni na vidonge 7 vilivyobaki vikiwa havina homoni. Vidonge hivi 7 ni kwa ajili ya kukumbusha kumeza kidonge kila siku. Baadhi ya paketi za siku 28, hata hivyo, zina vidonge vyenye homoni tu. Kwa paketi ya vidonge 21, tumia kimoja kila siku na baada ya hapo subiri hadi siku 7 kabla ya kuanza paketi nyingine .

VIDONGE MSETO VYENYE DOZI ZA HOMONI AMBAZO HUBADILIKA BADILIKA

Vidonge hivi hujumuisha mchanganyiko wa homoni za estrojeni na projestini ambazo hubadilika badilika kipindi chote cha mwezi mzima. Kwa vile kiasi cha homoni hubadilika, ni muhimu kutumia vidonge vyote kama ilivyopangwa.

Baadhi ya majina ya kibiashara: Gracial, Logynon, Qlaira, Synphase, Trinordiol, Trinovum, Triquilar, Triphasil

VIDONGE MSETO VYENYE DOZI ZA HOMONI AMBAZO HAZIBADILIKI: HOMONI ZOTE MBILI ZA ESTROJENI NA PROJESTINI

Vidonge mseto hivi hujumuisha estrojeni (kawaida makrogramu 35) na projestini (kawaida miligramu 0.1). Paketi ya siku 28 inakuwa na vidonge 21 vyenye homoni na 7 ambavyo havina chochote ila kwa ajili ya kukumbusha kumeza kidonge kila siku. Paketi ya vidonge 21 inakuwa na vidonge vyote vyenye homoni. Kiasi cha kila homoni ni sawa kwa vidonge vyote 21 kwenye paketi.

Baadhi ya majina ya kibiashara: Alesse, Cilest, Diane, Femoden, Gynera, Harmonet, Norinyl, Ortho-Novum, Ovysmen.

VIDONGE MSETO VYENYE DOZI ZISIZOBADILIKA: PROJESTINI ZAIDI NA ESTROJENI KIDOGO.

Vidonge hivi vina kiasi kikubwa cha projestini (miligramu 0.15 ) na kiasi kidogo cha estrojeni (makrogramu 30 ). Paketi ya siku 28 ina vidonge 21 vyenye homoni na 7 havina chochote ila kwa ajili ya kukumbusha kumeza kidonge kila siku. Paketi ya vidonge 21 ina vidonge vyote vyenye homoni. Kiwango cha homoni ni sawa katika vidonge vyote 21 katika aina zote 2 za paketi. Vidonge hivi vinaweza kufanya kazi vizuri zaidi kwa mwanamke ambaye hupata hedhi nzito kila mwezi au wanaopata maumivu kwenye maziwa kabla ya hedhi kuanza.

Baadhi ya majina ya kibiashara: Lo-Femenal, Lo/Ovral, Microgynon, Microvlar, Nordett.

VIDONGE VYENYE HOMONI YA PROJESTINI TU (VIDONGE VIDOGO)
Vidonge hivi vina homoni moja tu ya projestini na huwa katika paketi ya vidonge 28. Vidonge vyote kwenye paketi vina kiwango cha homoni ya projestini sawa.
Baadhi ya majina ya kibiashara: Femulen, Microlut, Micronor, Micronovum, Neogest, Microval, Ovrette, Exluton.

Uzazi wa mpango wa dharura (vidonge vya dharura vya kuzuia mimba)

Unaweza kutumia vidonge vya dharura vya kuzuia mimba au baadhi ya vidonge vya kawaida vya majira kuzuia mimba ndani ya siku 5 baada ya kufanya ngono bila kutumia kinga. Idadi ya vidonge ambayo unahitaji hutegemea aina ya homoni na kiwango cha homoni katika kila kidonge. Chati hii imeorodhesha aina chache tu za vidonge hivi. Hakikisha unajua aina na kiwango cha homoni katika vidonge kabla hujavitumia. Chati inaonesha jumla dozi kamili ya homoni ambazo zinahitajika na vidonge vingapi unahitaji kutimiza dozi hiyo.

Madhara ya pembeni ya kawaida ya vidonge vya dharura vya kuzuia mimba ni maumivu ya kichwa, kichefuchefu au maumivu tumboni, lakini yote haya hutoweka ndani ya siku moja au mbili. Ni kawaida kutokwa na damu kidogo au kutokea mabadiliko katika siku zako za hedhi mwezi unaofuata. Unapotumia vidonge vya dharura vya kuzuia mimba, vidonge ambavyo ni maalum kwa dharura au dozi sahihi ya vidonge vya projestini tu husababisha madhara ya pembeni kidogo kuliko kutumia vidonge mseto vya majira. Kama utatapika ndani ya saa moja ya kutumia dozi hii, hii inamaanisha kwamba unapaswa kurudia dozi ile uliotumia. Kamwe usichanganye aina tofauti za vidonge vya dharura vya kuzuia mimba au vidonge vingine vya majira kwa sababu vinaweza kushindwa kabisa kufanya kazi.

Jinsi ya kutumia vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango

JINSI YA KUTUMIA VIDONGE MAALUM KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Vidonge vya dharura vyenye miligramu 1.5 (makrogramu 1500 za levonorgestrel (NorLevo 1.5, Plan B One-Step, Postinor-1)
Dozi kamili ya kidonge 1 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia kidonge 1, mara moja tu.

Vidonge vya dharura vyenye miligramu 30 za ulipristal acetate (ella, ellaOne)
Dozi kamili ya kidonge 1 =miligramu 30 za ulipristal acetate
Tumia kidonge 1 , mara moja tu.

Vidonge vya dharura vyenye miligramu 0.75 (makrogramu 750) za levonorgestrel (NorLevo 0.75, Optinor, Postinor, Postinor-2, Plan B)
Dozi kamili ya vidonge 2 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia vidonge 2 , mara moja tu.

Vidonge vya dharura vyenye miligramu 0.05 (makrogramu 50) za ethinyl estradiol na miligramu 0.25 (makrogramu 250 ) levonorgestrel (Tetragynon, Neogynon, Nordiol)
Dozi kamili ya vidonge 4 =miligramu 0.2 (makrogramu 200 za ethinyl estradiol na miligramu 1.0 (makrogramu 1000) za levonorgestrel
Anza kwa kutumia vidonge  2 Halafu tumia vidonge 2 zaidi baada ya saa 12.

 

JINSI YA KUTUMIA VIDONGE VYA MAJIRA MSETO KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Kwa paketi ya siku 28 yenye vidonge mseto 28, tumia kidonge kutoka vidonge vya kwanza 21 ili kupata dozi iliyooneshwa hapo chini lakini usitumie vidonge vya mwisho 7 kwa sababu huenda vikawa havina homoni – ni kwa ajili ya kukumbusha kumeza kidonge kila siku.
Vidonge vya majira mseto vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za ethinyl estradiol na miligramu 0.15 (makrogramu 150) za levonorgestrel (Anna, Combination 3, Gestrelan, Microgynon, Microgynon-30, Nordette, Roselle)
Dozi kamili ni vidonge 8 =miligramu 0.24 (makrogramu 240) za ethinyl estradiol na miligramu 1.2 (makrogramu 1200) za levonorgestrel
Anza na vidonge4 Halafu tumia vidonge 4 zaidi baada ya saa 12
Vidonge mseto vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za ethinyl estradiol na miligramu 0.3 (makrogramu 300) za norgestrel (Lo-Femenal, 5Lo/Ovral)

Dozi kamili ya vidonge 8 = miligramu 0.24 (makrogramu 240) za ethinyl estradiol na miligramu 2.4 (makrogramu 2400) za norgestre

Anza na vidonge 4 Halafu tumia vidonge 4 zaidi baada ya saa 12
Vidonge vya majira mseto vyenye miligramu 0.02 (makrogramu 20) za ethinyl estradiol na miligramu 0.1 (makrogramu 100) za levonorgestrel (Alesse, Loette, Lutera, Miranova)

Dozi kamili ni vidonge 10 = miligramu 0.2 (makrogramu 200 ) za ethinyl estradiol na miligramu 1 (makrogramu 1000) za levonorgestrel
Anza na vidonge 5 Halafu tumia vidonge 5 zaidi baada ya saa 12.

JINSI YA KUTUMIA VIDONGE VYENYE PROJESTINI TU (VIDONGE VIDOGO) KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Katika paketi ya vidonge vyenye projestini tu, kila kidonge kina kiwango sawa cha dozi ya homoni.
Vidonge vya projestini tu (vidonge vidogo) vyenye miligramu 0.075 (makrogramu 75) za norgestrel (Ovrette, Minicon)
Dozi kamili vidonge 40 = miligramu 3 (makrogramu 3000 za norgestrel)
Tumia vidonge 40 mara moja tu (ni vidonge vingi lakini salama)
Vidonge vyenye projestini tu (vidonge vidogo) vikiwa na miligramu 0.0375 (makrogramu 37.5) za levonorgestrel (Neogest, Norgeal)
Dozi kamili ni vidonge 40 =miligramu 1.5 (makrogramu 1500 za levonorgestrel
Tumia vidonge 40 mara moja tu (vidonge vingi lakini salama)
Vidonge vyenye projestini tu (vidonge vidogo) vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za levonorgestrel (Microlut, Microval, Nortrel)
Dozi kamili ya vidonge 50 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia vidonge 50 mara moja tu (vidonge vingi lakini salama)

Ifahamike kwamba:Vidonge vya majira havitoi kinga dhidi ya VVU au maambukizi mengine kupitia ngono. Ili uweze kujilinda dhidi ya magonjwa hayo, unapaswa kutumia pamoja na kondomu.
Baadhi ya wanawake huamua kutumia vidonge vya majira kwa sababu vidonge hivyo husaidia kuweka vizuri mpangilio wa hedhi, ili waweze kujua lini siku zao za hedhi zitaanza. Vidonge vya majira pia hupunguza wingi wa damu ya hedhi, na mabonge ya damu na maumivu wakati wa hedhi. Vidonge vya majira havisabishi saratani.

Vidonge vya majira mseto (vyenye homoni za estrojeni na projestini).

Aina tofauti za vidonge mseto vya majira vina dozi tofauti za homoni hizi mbili. Kuna mseto wenye dozi za kawaida kama vile miligramu 1 au chini yake ya projestini na maikrogramu 30 au 35 za estrojeni (ethinyl estradiol), au maikrogramu 50 ya estrojeni nyingine iitwayo mestranol.
Baadhi ya vidonge vya majira vina homoni ya projestini tu.
Vidonge vya majira hufanya kazi vizuri kuzuia mimba vinapotumika kila siku na muda ule ule. Ni salama kwa wanawake walio wengi.

Jinsi ya kutumia vidonge mseto vya majira

Kama una uhakika kuwa huna ujauzito, unaweza kuanza kutumia vidonge vya majira wakati wote. Vidonge vya majira havitazuia mimba hadi uwe umekua ukivitumia angalau kwa wiki. Hivyo katika siku 7 za mwanzo baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira, tumia kondomu au epuka ngono.
Unatakiwa kutumia kidonge 1 cha majira kila siku kuzuia mimba, hata kama hutafanya tendo la ngono siku hiyo. Jitahidi kutumia kidonge muda ule ule kila siku. Kuweka vidonge mahali unapolala, kunaweza kukusaidia kukumbuka kumeza kidonge kila siku kabla hujalala. Aina nyingi za vidonge vya majira mseto huwa katika paketi ya vidonge 28 au 21.

 

Madhara ya pembeni ambayo yanaweza kuhusiana na vidonge mseto vya majira
Madhara ya pembeni siyo hatari sana lakini mengine yanaweza kukera. Kawaida hupungua au kutoweka baada ya miezi 3. Wakati mwingine unaweza kujaribu aina nyingine ya vidonge vya majira.

 • Mabadiliko katika hisia kama vile kuhisi huzuni au kuudhika kwa urahisi
 • Matiti kuvimba na kuuma
 • Maumivu ya kichwa
 • Kichefuchefu
 • Kutokwa na damu kidogo katikati ya vipindi vya kawaida vya hedhi.

Vidongo mseto vya majira vinaweza kutumika kupitia njia 3
Kutumia siku 28: Tumia vidonge vyenye homoni kwa siku 21 na baada ya hapo, kwa siku 7, tumia vidonge vilivyobaki. (Vidonge vya ziada kwenye paketi havina homoni), au usitumie tena vidonge. Utakuwa unapata hedhi kila mwezi wakati wa siku hizo 7 kama hedhi nyingine ya kawaida.

Matumizi ya muda mrefu: Tumia vidonge vyenye homoni kwa siku 84 vinavyofuatana na baada ya hapo pumzika kwa siku 7. Wakati mwingine vidonge huwa kwenye paketi zenye vidonge 91 (84 vyenye homoni na 7 kwa ajili ya kukumbusha tu ambavyo havina homoni). Wakati wa siku hizo 7, utakuwa unapata hedhi kama inavyokuwa katika hedhi ya kawaida lakini mara moja tu katika kipindi cha miezi 3. Matone ya damu (hedhi nyepesi sana) yanaweza kutokea lakini hutoweka baada ya miezi michache.

Matumizi endelevu: Tumia vidonge vyenye homoni kila siku bila kuacha. Kama utaona usumbufu na hedhi isiyotabirika, acha kutumia vidonge kwa siku 3 au 4 ili kupata siku chache za hedhi ya kawaida, halafu endelea kutumia kidonge tena kila siku.
Utaratibu wote huu wa kutumia vidonge mseto ni salama. Mtu yeyote ambaye anatumia vidonge mseto vya majira anatakiwa kujua afanye nini kama ataruka kemeza kidonge kimoja au viwili:

Kama utasahau kumeza kidonge 1 au 2, tumia kidonge 1 haraka mara utakapokumbuka. Baada ya hapo tumia kidonge kinachofuata katika muda wa kawaida. Hii inaweza kumaanisha kwamba utatumia vidonge 2 katika siku moja.

Kama utasahau kutumia vidonge 3, siku 3 zinazofuatana, tumia kidonge 1 mara moja. Baada ya hapo, tumia kidonge 1 kila siku katika muda ule ule. Tumia kondomu hadi utakapoanza hedhi yako, au usifanye ngono hadi utakapokuwa umetumia kidonge kila siku kwa siku 7 mfululizo.
Kama hedhi yako haitakuja muda wake wa kawaida na umesahau kumeza baadhi ya vidonge, endelea kutumia vidonge vyako, lakini pata kipimo cha mimba. Kama utakuta una mimba, simamisha kutumia vidonge.

Kusitisha matumizi ya vidonge mseto vya majira
Unaweza kusimamisha matumizi ya vidonge wakati wote. Unaweza kupata mimba mara moja, hivyo iwapo unataka kuepuka kupata mimba, tumia kondomu au njia nyingine.

Nani hapaswi kutumia vidonge mseto vya majira
Baadhi ya wanawake wana matatizo ya kiafya na matumizi ya vidonge mseto vya majira vinaweza kuhatarisha maisha yao. Usitumie vidonge mseto vya majira iwapo:

 • Una tatizo la presha kubwa ya juu (160/110 au juu zaidi).
 • Ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 20.
 • Kama una zaidi ya miaka 35 na ni mvutaji wa sigara.
 • Tatizo la maumivu makali ya kichwa (maumivu ya kichwa makali yakiambatana na kichefuchefu) kama yakiambatana na kufa ganzi au na matatizo makubwa katika kuona.
 • Saratani ya matiti, saratani ya ini, au saratani ya kibofu cha mkojo.
 • Uliwahi kupatwa na kiharusi
 • Damu kuganda kwenye mshipa (hali hii kawaida husababisha joto na maumivu kwenye mguu mmoja).

Wanawake wengi wenye tatizo moja la kiafya wanaweza kutumia kwa usalama vidonge vya majira vyenye projestini tu au njia ya vijiti au sindano za projestini tu. Wanawake wenye ugonjwa wa saratani ya matiti au saratani ya tumboni hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango zenye homoni, na badala yake watumie njia nyingine.

Dawa ambazo zinaingiliana na vidonge mseto vya majira
Rifampicin (dawa ya kifua kikuu), ritonavir (dawa ya VVU) na baadhi ya dawa za kifafa huathiri utendaji wa vidonge vya majira. Kama utatumia dawa hizi, chagua njia tofauti ya uzazi wa mpango. Wanawake wanaotumia insulini kwa ajili ya kisukari wanaweza kuhitaji kurekebisha kiasi cha insulini baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira.

Nani wanapaswa kufikiria njia zingine kama zipo
Kuna matatizo machache ya kiafya ambayo hufanya njia ya vidonge vya mseto vya majira kutofaa baadhi ya watu. Ni bora zaidi kwa wanawake wenye matatizo haya kutumia njia nyingine ya kupanga uzazi:

 • Tatizo la shinikizo la juu la damu-presha ya juu (zaidi ya 140/90).
 • Kama una zaidi ya miaka 35 na una matatizo ya kuumwa kichwa (maumivu ya kichwa yanayoambatana na kichefuchefu).

Kama mwanamke mwenye matatizo atatumia vidonge mseto vya majira, angaliwe kwa karibu kuhakikisha matatizo hayo ya kiafya yasizidi. Kama hakuna mabadiliko, basi ni bora kuendelea kutumia vidonge mseto vya majira. Kama matatizo yataongezeka, asimamishe mara moja kutumia vidonge hivyo haraka.

Madhara ya pembeni ya vidonge vidogo vya majira
Madhara ya kawaida kwa vidonge vyenye homoni moja ya projestini (vidonge vidogo) ni mabadiliko katika mpangilio wa hedhi ya kila mwezi. Unaweza kupata damu wakati hutarajii. Hedhi inaweza kutopatikana kabisa. Hii siyo hatari. Madhara mengine yanaweza kujumuisha kuongezeka uzito, kuumwa kichwa, na vipele vidogo mwilini.

Dawa zinazoingiliana na kidonge kidogo cha majira
Rifampicin (dawa ya kifua kikuu), ritonavir (dawa ya VVU) na baadhi ya dawa za kifafa huathiri utendaji wa vidonge vya majira. Kama utatumia dawa hizi, chagua njia tofauti ya uzazi wa mpango. Wanawake wanaotumia insulini kwa ajili ya kisukari wanaweza kuhitaji kurekebisha kiasi cha insulini baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira.

Kusitisha matumizi ya vidonge vidogo vya majira
Kama unataka kupata mimba au kubadilisha njia ya kuzuia mimba, unaweza kuacha kutumia vidonge vidogo vya majira wakati wote. Unaweza kupata mimba mara baada kusimamisha vidonge hivyo. Kama unataka kuepuka mimba, anza njia nyingine mara moja.

 

>>>>>>>>>>> Updated<<<<<<<<<<<

 

4.Njia ya vijiti na sindano za kuzuia mimba.

Kama kilivyo kidonge kidogo cha majira, njia ya vijiti na sindano za kuzuia mimba vina homoni ya projestini tu, lakini mwanamke hatakiwi kukumbuka kutumia kidonge kila siku. Njia ya vijiti na sindano za majira ni rahisi kutumiwa kwa siri. Hata hivyo, siyo njia ya vijiti wala sindano za majira ambayo inatoa kinga dhidi ya maambukizi yanayopitia ngono vikiwemo VVU.

Jinsi ya kutumia njia ya vijiti au sindano za majira

Vijiti vya majira ni virija vidogo vya plastiki ambavyo mfanyakazi wa afya huingiza chini ngozi ya upande wa ndani wa mkono wa mwanamke. Huzuia mimba kwa miaka 3 hadi 5, kutegemea na aina ya vijiti. Sindano za majira hutolewa na mtaalam wa afya, mara moja kila mwezi 1, 2, au 3, kutegemea na aina ya sindano. Vijiti na sindano za majira ni njia rahisi kutumika kwa siri, na mwanamke hatakiwi kukumbuka kutumia kidonge kila siku. Vijiti vyote vya majira na baadhi ya sindano zina projestini tu.

 

Aina moja ya sindano (sindano ya kila mwezi) ina homoni zote mbili –estrojeni na projestini. Hivyo sindano hii haifai kwa wanawake ambao hawawezi kutumia vidonge mseto vya majira. Mwanamke anaweza kuamua kusimamisha sindano za majira au kuondoa vijiti vya majira kama atataka kupata mimba. Njia ya vijiti au sindano haiwezi kutoa kinga yoyote dhidi ya maambukizi yanayopitia ngono vikiwemo VVU.

Madhara ya pembeni

Sindano za majira za kila mwezi zinaweza kuwa na madhara ya pembeni yanayofanana na vidonge mseto vya majira. Njia ya vijiti na sindano za projestini tu zina madhara ya pembeni yanayofanana na vidonge vidogo vyenye projestini tu.

Dawa ambazo huingiliana na njia ya vijiti na sindano za majira

Rifampicin (dawa ya kifua kikuu) na baadhi ya dawa za kifafa hupunguza ufanisi wa njia ya vijiti na sindano za majira. Kama unatumia dawa hizi, tumia njia tofauti ya uzazi wa mpango. Wanawake ambao wanatumia insulini kwa ajili ya tatizo la kisukari wanaweza kuhitaji kurekebisha kiasi cha insulini wanachotumia baada ya kuanza njia ya vijiti au sindano za majira.

Kusitisha matumizi ya vijiti au sindano za majira

Ili kusitisha matumizi ya vijiti, unapaswa kupata mtaalam wa afya ambaye ataviondoa. Mwanamke anaweza kupata mimba mara moja baada ya kuondoa vijiti hivyo vya majira. Kusimamisha sindano za majira ni rahisi. Ni suala la kuacha kuchoma sindano hizo. Inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kwa mwanamke kupata mimba baada ya kusimamisha matumizi ya sindano za kuzuia uzazi. Hata hivyo wanawake wengi wanaweza kupata ujauzito ndani ya mwaka 1.

5.Njia ya kitanzi.

Kitanzi cha kuzuia uzazi ni kidude kidogo cha plastiki, au plastiki na shaba, ambacho huwekwa kwenye kizazi cha mwanamke na mtaalam wa afya. Kitanzi huzuia mbegu za kiume kurutubisha yai la uzazi, na pia huzuia yai kutojibanza kwenye ukuta wa tumbo la uzazi.

Njia ya kitanzi ina kiwango kikubwa cha ufanisi, na kitanzi kinaweza kukaa ndani ya kizazicha mwanamke kwa muda kuanzia miaka 5 hadi 12, kutegemea na aina ya kitanzi. Kitanzi hakitoi kinga dhidi ya maambukizi yanayopitia ngono vikiwemo VVU.

Kitanzi ni njia salama kwa wanawake ambao wamewahi kupata ujauzito na wale ambao hawajawahi kupata mimba. Kitanzi kinaweza kuingizwa kwenye kizazi cha mwanamke wakati wote ule anapokuwa hana ujauzito, na akiwa hana maambukizi ukeni au maambukizi yanayopitia ngono. Kitanzi kinaweza pia kuondolewa na mtalaam wa afya wakati wowote ule. Baada ya kuondolewa, mwanamke anaweza kupata mimba bila kuchelewa.

Mara baada ya kuingizwa kwenye kizazi, siyo rahisi kitanzi kutoka lakini inawezekana. Mara moja kwa mwezi, unaweza kukagua kama kamba za kitanzi ambazo huninginia kutoka kwenye mlango wa kizazi bado zipo kwa kuingiza kidole ndani ya uke wako na kuzigusa (lakini siyo kuzivuta). Kama huwezi kuzigusa au kama unafikiri kitanzi kimetoka, tumia kondomu au epuka kufanya ngono hadi utakapopata uchunguzi wa mtaalam wa afya.

Madhara ya pembeni ambayo yanaweza kutokea kutokana na matumizi ya njia ya kitanzi

Madhara ya pembeni ya kawaida ni hedhi kuwa nzito zaidi, ikiambatana na maumivu zaidi kuliko kawaida. Hali hii inaweza kuumiza lakini siyo hatari na taratibu hupungua baada ya miezi michache. Baadhi ya aina za vitanzi vina homoni ya projestini, ambayo husaidia kupunguza kero na damu ya hedhi. Kitanzi chenye projestini kinaweza kusababisha madhara ya pembeni yanayofanana na ya vidonge vidogo vya majira.

Nani hapaswi kutumia kitanzi

 • Wanawake wenye saratani ya mlango wa kizazi au tumbo la uzazi. Wanawake wenye saratani ya matiti hawapaswi kutumia kitanzi chenye projestini, lakini wanaweza kutumia kwa usalama kitanzi chenye shaba.
 • Wanawake wanougua kisonono, klamidia, au maambukizi sehemu ya nyonga (kwenye kinena). Kwa taarifa zaidi juu ya ugonjwa wa kisonono na klamidia,
Continue Reading

Health

Health tips: What To Eat During Pregnancy?

Published

on

Are you wondering how to keep you and baby healthy in these nine months? Here are the few tips on what to eat during your pregnancy and what to limit and avoid for the next 40 weeks(Infographics),

 

precision-nutrition-pregnancy-nutrition-2

 

Continue Reading

Health

Wewe ni mtumiaji wa vilevi? mambo ya muhimu unayopaswa kufahamu kuhusiana na Vilevi

Published

on

“Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18, kunywa kistaarabu” ujumbe huu unapatikana katika matangazo yote ya vilevi, na nadhani hilo linatambulika kwamba pombe si ya vijana chini ya miaka 18. Unywaji wa pombe ni kawaida kwa watu wengi lakini unakunywa kistaarabu? Sina mpango wa kukufundisha kunywa pombe wala kukushawishi uanze kunywa Pombe wote tunajua madhara yanayoletwa kwa unywaji wa pombe wa kupindukia. Leo tuongelee upande wa pili wa shilingi, faida za unywaji wa pombe kwa wastani. Narudi unywaji wa pombe kwa wastani.

Magonjwa ya Moyo.
Utafiti kutoka Harvard University Marekani, umegundua unywaji wa pombe kwa kiasi cha wastani kinasaidia mzunguko mzuri wa damu,hii inasaidia kuzia matatizo ya moyo na magonjwa ya kiharusi na kupooza (stroke)

Urefusha Maisha

Utafiti uliofanywa na Catholic University huko Campobasso, waligundua kuwa kunywa chupa chini ya 4 au 2 kwa siku kwa mwanamme au mwanamke, kwa asilimia 18 inaongeza muda wa kuishi kama ililipotiwa na Reuters. Dr. Giovanni de Gaetano wa Catholic University pia alisema sio mbaya kama unaweza kunywa pombe kidogo wakati wa kula. Makala nyingine iliyoandikwa na Mediterranean diet, kuwa mvinyo (wine) ni kinywaji safii wakati wa chakula cha mchana na cha jioni. Lakini usinywe tu pombe wakati wote.

Inasaidia kuamsha Hisia za Mapenzi.
Kama ilivyo Red Wine inasaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya moyo, Mwaka 2009 jarida lililotambulika kama Sexual Medicine, liliandika kwa utafiti waliofanya asilimia 25 – 30 wanywaji wa pombe hawapati matatizo ya kushindwa kushiriki tendo. Mkuu wa utafiti , Kew-Kim Chew Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka University of West Australia alifanya utafiti kwa wanaume 1,770 wa Australia, Chew aliwashauri pia wanaume hao wasitumie pombe kupitiliza sababu bado wanafanya utafiti juu ya swala hilo kwa kina zaidi.

Pombe huamsha Akili.
Utafiti uliohusisha watu zaidi ya 365,000 toka mwaka 1997 iliripotiwa na jarida la Neuropsychiatric Disease and Treatment watu wanaokunywa kwa wastani wanauwezo wa kuzuia ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya akili. Kiwango kidogo cha pombe kinafanya seli za ubongo ziwe hai (fit/active) alisema Edward J. Neafsey, Ph.D mwandishi wa Science Daily. alisema pia hawashauri watu wasiokunywa pombe waanza kunywa pombe. Na akasema kama wale wanaokunywa wanakunywa kwa wastani basi itawasaidia.

Husaidia Tatizo La Mawe kwenye Kibofu.
Kwa wanywaji wa wastani kuna uwezekano wa kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la mawe kwenye kibofu huo ni utafiti uliofanywa na University of East Anglia, watafiti walisema faida zinaonekana kwa wale wanywaji wa kawaida na sio waywaji wa pombe kupinduki sababu unywaji wa pombe kupitiliza huleta matatizo ya kiafya

Ugonjwa wa Sukari.
Tafiti zilizofanywa uholanzi, watu wenye afya wanao kunywa glass moja au mbili kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata aina ya pili ya kisukari ukiachilia mbali wale wasiokunywa hata kidogo, wale wanaokunywa kidogo wana afya zaidi, walisema watafiti hao kupitia Reuters.

Angalizo

kujua faida hizi za pombe haina maana kama hujaanza kunywa pombe uanze sasa na kama wewe unatumia kilevi basi kunywa kwa kiwango kidogo sababu ni faida kwa afya yako kuliko unywaji wa kupindukia. Kunywa kistaarabu.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 mtokambali.com