Maisha ni mazuri na matamu kweli kweli LAKINI kamwe maisha Sii rahisi kama Unavyodhani.
Tangazo

Maisha ni kila kitu.Maisha ni kila kitu. Maisha ni mazuri na matamu kweli kweli LAKINI kamwe maisha Sii rahisi kama Unavyodhani. Kuna wengine maishai. Kuna wengine maisha kwao ni rahisi na mepesi kweli kweli ila nyuma ya pazia ni kwamba nguvu ya ziada ilitumika mpaka maisha yakawa rahisi kwao.

Wakati mwingine tunatembea katika maisha haya huku tukiepuka mambo madogo madogo ambayo sisi tunayaona ni Mabaya kwetu na wakati wote tumekua tukiyakimbia na kuyakwepa kabila Lakini ukweli ni Kwamba Lazima tuyakubali mambo haya na kuyachukulia kama sehemu ya maisha yetu kwa kua tuu hii ndio njia pekee ya Kufanikiwa katika maisha na Kuondokana na Vifungo vya Maisha(Mateso, Kuvunjika mioyo na Kukata tamaa).

Yapo mambo mengi mno yanayozungumzia Ukweli juu ya maisha ila kwa haya machache niliyo kuandalia leo, utapata picha halisi juu ya maisha na utakua Huru daima.

1.Kifo ni kwa kila mtu unayempenda na Kifo hakiepukiki.

Wakati mwingine tunajisahau na kuwachukulia wale wote tunao-wapenda kama zawadi ya pekee ambayo mtu yeyote ama kitu chochote kitakachoweza kuichukua zawadi hiyo kutoka katika mikono yetu. Ila ukweli ni kwamba Kifo Juu yetu na hawa watu ambo ni Zawadi kwetu ni Lazima na kamwe hatutoweza Kulikwepa jambo hili maana kila Chenye mwanzo kina mwisho wake.

Iko siku tutashindwa Kuwaita wazazi ama rafiki zetu kwa majina yao bila kusikia chochote kutoka kwao maana Pumzi yenye uhai itakua teyari haipo ndani ya Miili yao na zaidi ya yote hata fursa ya kuona miili yao haitakuwepo na Hapo tutaishia kuangua Vilio na Majonzi tele. Na huu ndio ukweli wa Maisha haya.

2.Tunayapa Maisha yetu Maana.

Kuna watu kama Buddhists huamini kwamba tunayajenga maisha katika ulimwengu wetu wenyewe kwa kupitia Maono yetu na Vitendo vyetu. Hatuna haja ya Kutoka na kwenda kuungana na wale wanaitafuta amani ama wale wanaopambana na Baa la Njaa ama Kutoka kutafuta Chakula cha Kifahari katika mahoteli ya Kifahari ama Kutafuta Ukuu katika kampuni Kubwa ulimwenguni.

Mara nyingi hua tunatamani na Kufikiri juu ya yale mambo ambayo hatuna Uwezo wa Kuwa nayo na Hali hii hutufanya Kuyaona Maisha kwamba sii chochote na kuyasahau yale yote tuliyoyajenga kwa Nguvu zetu hapo awali na mwisho wa siku tunakata tamaa ya maisha na Kujitoa Uhai.

3.Mpenzi wa Kweli hapatikani Dunia Hii.

Wakati mwingine Tunayatamani mapenzi ya dhati kutoka kwa mpenzi mwenye mapenzi ya Kweli ila mpaka tunazeeka na miili yetu kuchoka kabisa hatuyaoni mapenzi hayo.

Wengi wetu tunaishi na Ndoto za mchana yakwamba Mpenzi sahihi katika maisha yetu yupo na tunakua tukiyaharibu mahusiano yetu tuliyo nayo kwa sasa kwa sababu tuu mioyo yetu hairidhiki kwa kile tulicho nacho. Na hii inatokana na kule tunapoweka Mioyo yetu na Akili zetu kwa wakati mmoja kukosa yale tuliyo yatarajia. Unaweza Ukamwona mtu ukadhani Huyu ndiye yule tuliyemwota Ndotoni ya kwamba utakua nae daima na Kukupatia lile penzi la Dhati kabisa lakini baada ya Kuzama penzini ukatoka kapa kabisa na Kubaki ukililia mapenzi kili kukicha.

4.Maisha ni Mchezo

Je ni kwanini tutembee juu ya mayai huku tukiwa na Umakini wa hali ya juu tusijeleta balaa? Haya maisha ni ya kwetu na tunapaswa kujifunza na kupata uzoefu. Yatupasa kuyachukulia maisha kama mchezo siku zote huku tukishirikisha kile tunachokitaka maishani na Kujifunza Sheria za Mchezo huu na mwishoni Kupanda katika ngazi ya Juu(Mafanikio).

Hatutoweza Kufanikiwa katika mchezo huu kama hatutajiingiza katika mchezo huu. Uliwahi kusikia mcheza Mpira maarufu ulimwenguni ambaye hakuwahi kuingia uwanjani ila kwa maarufu?

5. Kila kitu kina mwisho.

Kila chenye mwanzo mara zote kinakua na mwisho, hakuna jambo litakalodumu milele. Tunakua katika ujana kwa muda Fulani  na kisha tunaingia Uzeeni. Watu wanazaliwa kisha wanakufa, Tunazama katika mapenzi na Tunatoka pia katika mapenzi. Tunapaswa kutambua kwamba binadamu wote ni sawa ila tuu tunatofautiana katika mafanikio. Hukuna kitakachodumu daima na ndio maana kama mambo yangedumu milele tusingeyapa Mambo hayo Umuhimu kabisa.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


AdvertisementMtokambali 728x90