Fahari ya Mwanaume!!

Fahari ya mwanaume ni MKE WAKE, FAMILIA YAKE na NYUMBA YAKE.

Kiukweli, hamna kitu kizuri kama mtu kuwa na kitu ambacho kinampa ufahari. Kitu ambacho anajivunia kuwa nacho popote na wakati wowote. Na ukiwa a kitu kinachokufanya ujisikie fahari hakika hutoacha kukishow off.

Sadly, familia nyingi kwenye jamii yetu zina wanaume wasioona fahari kuwa na wake walio nao, wakati mwingine hata watoto kwahiyo kuwashow off’ ni nje kabisa ya matakwa yao.

Juzi kati kuna mkaka alirudi nyumbani kwake usiku akaanza kugombana na mke wake (heeey I couldn’t help it. Huku uswahilini kwetu hatuna ceilingbord wala madirisha, your business is everyones bussines). Anyway, baadae jamaa akawa analalamika kwamba mwanamke wake ana kauli chafu, kila akirudi anapokelewa na makelele, yani hawezi kufika nyumbani akapumzika kwa amani hata siku moja. Which made me think, wanawake (sio wote wala sisemi wengi) huwa wanalalamika waume zao kuchelewa nyumbani, kutopenda kuongozana nao, kutokuwa karibu na watoto na mengineyo bila kujali wala kujiuliza ni kwa kiasi gani wao wenyewe wanachangia hali hiyo.

Katika hali ya kawaida, wanaume huwa wanaona fahari sana (sifa) kuongozana na wenza wao pia  kuwatambulisha wakiwa katika muonekano mzuri. Wanaona sifa kukaribisha wageni/marafiki zao kwenye nyumba iliyopangiliwa vyema, kwa mke asiye na gubu kila wakati, kwa mke anaeweza kukaribisha wageni chakula wakakifurahia badala ya kudanganya wameshiba kumbe wanakwepa msosi (heheheheh), kwa watoto wanaobebeka (sio mtoto ananuka mkojo muda wote na makamasi/udenda unatiririka kama chemchem) n.k

Mwanamke ni msaidizi wa mwanume, hivyo anatakiwa amsaidie mwanaume wake kuona na kupata fahari kwa kuwa na mkewe huyo, familia yake, nyumba yake n.k . Ofcourse, hata mwanaume anatakiwa achangie kwenye haya ila kila kitu kinaanza na sisi wanawake.

HAYA NI BAADHI YA MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA KUMFANYA MUMEO AWE PROUD NA WEWE……

1.Jua kupendeza badala ya kuchekesha. Mfanye mwanaume wako apende na afurahie kuongozana/kuonekana na wewe bila woga wala aibu. Sio mtu tumbo ni kubwa kuliko kiwiliwili cha chini lakini bado unavaa nguo za kubana na kuchora mpaka wanaokuangalia wanakuonea aibu, mumeo ataona nini? Uso umepambwa kama Christmass tree nani aonekane na wewe achekwe?

2.Jitahidi kuwa na kauli nzuri ili ukaribishe watu(including mumeo) badala ya kuwafanya wakukimbie. Mwanamke ukiwa na kauli mbovu na kuropoka hovyo mwanaume hatoona fahari kukaribisha wageni nyumbani kwenu ili wavutiwe mdomo,wanuniwe na kuropokewa mpaka watamani kuondoka wala hatoshawishika kuwahi kurudi nyumbani kamwe, labda kuwe na tatizo. Hata kama hana hela atakuwa radhi kuzagaa zagaa tu mahali ili mradi tu muda uende.

3.Kuwa msafi. Usafi wa nyumba unamvutia mtu kuwa nyumbani, usafi wa mwili unamvutia mtu kuwa karibu na wewe. Ukishidwa kutofautisha nyumbani na kiwanda cha karatasi kwa hewa nzito/dampo kwa mvurugiko hamu ya kuwepo nyumbani inapungua.

4.Angalia Watoto wako vizuri. Kuna watoto bwana hata kama unapenda watoto namna gani huwezi kuwabeba. Utaishia kumuongelesha tu na kumshika mashavu. Usiache mtoto aonekane mchafu mchafu kila wakati.

5.Jitahidi kwenye maswala ya UPISHI. Sio lazima uwe mtaalam sana, jifunze kiasi cha kuwafanya watu wafurahie chakula chako, haswa mumeo. Badala ya mwanaume kurudi na kisingizio cha ameshiba kila mara iwe hata akila nje ya nyumbani bado awe na hamu ya kula/kuonja chakula cha mkewe. Na badala ya kwenda kukutana na marafiki zake kwenye nyama choma/supu za mtaani awakaribishe nyumbani kwa chakula.

Wanawake tuna nguvu kubwa sana katika kujenga nyumba zetu. Hivyo matatizo mengine tunayasababisha wenyewe kwa kusahau nafasi zetu. Jitahidi kuwa mzuri (a good woman) kadiri uwezavyo ili mwenzako nae awe na nafasi ya kuwa mzuri kwako.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


 

AdvertisementMtokambali 728x90