Tangazo

Mamlaka nchini Somalia imevifunga
vituo viwili vya redio nchini humo baada ya kutangaza habari za
wapiganaji wa Al-shabaab kuhusu shambulio la chuo kikuu nchini Kenya.

Kituo cha redio cha Sky FM na kile cha Shebelle vilifungwa huku mtangazaji na mkurugenzi wakikamatwa.
Vikosi
vya usalama nchini Somali vimekuwa vikiwakamata wanahabari ambao
hufanya mahojiano na wapiganaji wa Al-shabaab ama kutangaza habari zao.

AdvertisementMtokambali 728x90