Health eating – faida za CABBAGE

Tangazo

Kuna aina 2 za cabbage: Kuna ile ya kijani na ile ya rangi nyekundu/purple.

Faida zake:
1.Kabichi mbichi inasaidia kutoa uchafu tumboni na kusafisha utumbo wa juu kitu ambacho kinasaidia mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri pia kupunguza kuvimbiwa.
2.Inasaidia kuzuia saratani (cancer) hasa saratani ya tumbo.
3.Inachochea mfumo wa kinga kwa kuua bakteria hatari pia inasaidia kupunguza makali ya vidonda vya tumbo.
4.Majani ya nje ni chanzo kizuri cha vitamin E hivyo husaidia kupendezesha ngozi.
5.Ni chanzo kizuri cha ‘antioxidants’ hivyo kusaidia sana kuondoa sumu mwilini.
6.Kutokana na kuwa na kiasi kidogo sana cha kalori (calories) cabage husaidia pale mtu anapokuwa amekusudia kupunguza uzito.
7.Inafanya ngozi iwe na afya na kuilinda isiharibiwe na jua.
8.Vitamin A inayopatikana kwa wingi kwenye cabbage nyekundu inafanya macho yawe katika afya nzuri.
9.Pia cabbage nyekundu ina kiasi kikubwa cha madini ya  calcium, magnesium, manganese. Madini hayo ni mazuri katika kuimarisha mifupa.
TAHADHARI
  • Haishauriwi kwa mama mjamzito kula cabbage nyekundu kwasababu inaweza kusababisha mtoto atakaezaliwa awe anajaa gesi tumboni (colic) na kupata maumivu makali.
  • Kwa wale ambao hua wanasumbuliwa na tatizo la gas baada ya kula cabbage unaweza ukazisteam/weka kwenye maji ya moto kwa dakika kama tano hivi kabla ya kuzipika.
  • Kama una matatizo ya goita inabidi ushauriane na daktari kabla ya kula cabbage kwasababu kwa kula cabbage unaweza ukavuruga matumizi ya madini ya chumvi mwilini.
Namna tofauti tofauti ya kuandaa CABBAGE…..
  • Kupika mboga ..hii nadhani wengi wetu tumezoea na tunaijua.
  • Pizza salad…hii ni moja ya uandaaji nnaopenda sana mimi na unaweza kula na chochote kile upendacho au hata yenyewe tu.

Mahitaji ni cabbage yenyewe, pilipili hoho nyekundu, carrot (hii nimeongeza mwenyewe), kijiko kimoja cha sukari, kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia (ya alizeti/zeituni kama unayo),siki (vinegar)  kiasi upendacho na pilipili manga (black pepper…samahani kama nimekosea kwa kiswahili) iliyosagwa kidogo.

Ukishakatakata kila kitu  una-steam cabbage kwa dakika zisizozidi 5 maana hazitakiwi kuiva .Baada ya hapo unaziweka kwenye chombo ambacho utapenda kuchanganyia…kisha weka viungo vyote pamoja (vinegar unaweza kuweka kidogo kwanza na kuongeza baada ya kuonja na kuona kwamba unahitaji kufanya hivyo) alafu unavichanganya. Ukisharidhika funika vizuri alafu weka kwenye jokofu na itakua tayari kuanzia masaa manne baadae na kuendelea.
  • Aina nyingine ya salad ni hii (sina jina) unachanganya cabbage zilizokwisha katwakatwa pamoja na carrot zilizokwanguliwa.Unanyunyuzia chumvi alafu unaweka kikaangio chako jikoni….weka mafuta kidogo sana na uache kikaangio kipate moto kabla ya kuweka cabbage yako. Ukiweka cabage hutakiwi kuifunika wala kuiacha jikoni muda mrefu…geuza geuza kwa dakika chache zikianza kulainika tu unatoa jikoni (hazitakiwi kuiva) kisha ziache zipoe kidogo. Zikishapoa nyunyuzia limao kidogo tayari kwa kula.
  • Raw red/purpe cabbage salad. Mchanganyiko wa cabbage (red/purple),slices za nyanya, vitunguu, pilipili hoho kidogo, chumvi na limao.
  • COLESLAW –  Changanya mayonnaise, vitunguu, masturd kidogo, sukari kidogo, vinegar, chumvi, black/white pepper,mahindi ya kuchemshwa na cabbage yenyewe.
  • Cabbage soup…..Unakata cabage vipande vipande, unachanganya na viungo vingine upendavyo (hoho, pilipili, vitunguu, viazi, vitunguu swaumu, nyanya n.k) alafu unavichemsha pamoja (nzuri sana kama uko kwenye DIET).
Kama ulikua hupendi cabbage jaribu kuitengeneza kwa namna tofauti na ile uliyozoea kuona  kama hupendi cabbage ama hupendi namna ambayo umezoe kuandaa/kuandaliwa cabage.

Tafadhali tupe maoni yako kuhusiana na mada hii katika sehemu ya comment…


By Malkia Sun
Insta:malkiasun

 

AdvertisementMtokambali 728x90