Tangazo
 Njegere ni moja wao ya vyakula vya kawaida sana kwenye jamii yetu. Baadhi yetu hula kwa mazoea tu bila kujua faida zake mwilini na wengine huchagua kutokula bila sababu ya msingi bila kujua faida ambazo wanakosa.
Image result for njegere
Faida za njegere :
1. Zinapunguza cholesterol kwenye damu.
2. Zinaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani (cancer) za aina
zote kutokana na kua na kiasi kikubwa cha Vitamin A na C.
3. Zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke.
4. Zinasaidia kupunguza hatari ya kuzorota kwa seli kunakoweza kuhusiana na umri.
5. Zina madini ambayo ni muhimu kuimarisha afya ya mifupa.
6. Zina madini ya chuma ambayo yanaweza kusaidia kuepuka upungufu wa damu
mwilini (Anemia)

Kama inavyoonekana hapo juu faida ni nyingi..ila sasa wangapi kati yetu hua tunazila? Nna uhakika sio wengi ukilinganisha na wasiokula kwakua nimeona kutoka kwa watu wanaonizunguka. Na ukweli ni kwamba hata mimi nilikua sili (kwakua nilidhani sizipendi) miakaya nyuma. Ila ukweli ni kwamba uandaaji wake ndio ambao haukunivutia.

Namna mbali mbali za kuandaa njegere…..

Changanya kwenye mboga e.g kuku au nyama, ndizi (machalari) au viazi mbatata.

Kuchemsha : Waweza zichemsha tu na chumvi (au kama zimegandishwa unapasha) kisha ukatengeneza salad na kuzila pembeni ya chakula chochote upendacho mf.wali, ugali, viazi, maccaroni, chapati za maji etc.

 Unaweza ukatengeneza supu.Baada ya kuzichemsha unaziponda ponda kisha unaweka maji/maziwa na viuongo vingine upendavyo (vitunguu swaumu, black pepper, curry, binzari n.k) kuongeza ladha.
Lastly my favorite…… zilizochanganywa na wali pia kwenye filling ya sambusa za mboga mboga au hata za nyama.
 
Hizi napenda sana kwakua zinakua na ladha zaidi.Kwa kawaida hua baada ya kuzichemsha pamoja na carrot nazikaanga na vitunguu swaumu, binzari, pepper na curry kidogo kabla ya kuzichanganya na wali.
 
 
Natumaini kuwa wale ambao mlikuwa hamli njegere kwa kutopenda ama kutojua umuhimu wake mtaanza sasa.
 


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


AdvertisementMtokambali 728x90