Mfahamu Mwanamuziki Adele, historia yake na Muziki kwa ujumla

Tangazo

Karibu na leo nimekuandalia historia ya Msanii Adele.

Adele ni mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo kutokea Uingereza ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na Kipaji na sauti yake yenye mvuto kweli kweli. Alizaliwa nchini Uingereza na kulelewa na mama yake pekee tangu akiwa mdogo.

Alianza Kuupenda na kuusikiliza muziki aina ya Pop ambapo baadae alizidi kuvutiwa na Muziki kutoka kwa wasanii Ella Fitzgerald na Etta James ambao wote hao walikua ni wanamuziki maarufu nchini humo. Alianza kukifikiria kipaji chake tangu akiwa mdogo ambapo wakati huo alikua BRIT School.

Kipaji chake na uwezo wake katika muziki ulianza kuzitoa udenda record labels kubwa nchini Uingereza na mara baada ya kuhitimu masomo yake alipata dili la Kusainishwa na Record Label inayojulikana kama XL Recordings.

Baada ya kuiteka Vilivyo Uingereza kwa live Performance zake, Adele aliachia Album yake ya kwanza Iliyopewa Jina la “19” na hii ilikua ni mnamo mwaka 2008 ambapo album hii ilifanikiwa kufanya poa kaika chati kubwa mbali mbali za muziki nchini Uingereza na album yake hiyo ilifanikiwa kunyakua nambo moja katika British album chart.

Baadae alichia album yake ya pili iliyokwenda kwa jina la “21” ambapo ndani ya album hii kulikua na hit songs kama vile Rolling in the Deep na ile ya Someone Like You. Nyimbo zote hizo mbili zilifanikiwa pia kuzitikisa chart mbali mbali za muziki Nchini Uingereza na Ulimwenguni kwa Ujumla na zaidi ya yote alifanikiwa pia kuvunja rekodi za mauzo katika masoko ya muziki ulimwenguni kote.

Uimbaji wake sauti yake na Perfomance zake vimemfanya Adele kuonekana kwamba ndiye mwanamuziki anaependwa na mwenye mvuto kwa wengi katika kizazi hichi cha leo.

Maisha yake ya Utotoni na Hapo awali.

Majina yake kamili anajulikana kama Adele Laurie Blue Adkins na alizaliwa mnamo May 5, 1988 katika jiji la Tottenham nchini Uingereza. Hakulelewa na wazazi wote wawili na hii ilitokana na baba yake ambaye alikua na asili ya Welsh aliyejulikana kwa jina la Mark Evans kuikimbia familia yake wakati Adele akiwa bado mdogo hivyo alilelewa na Mama pekee.

Adele alianza kuupenda muziki tangu akiwa mdogo na alikua inspired na Spice Girls analikua akifurahia kazi za Lauryn Hill, Destiny’s Child na Mary J. Blige.

Safari yake ya Muziki wake.

Mnamo mwaka 2008 aliachia album yake ya kwanza 19 ambapo aliipatia album hii jina hilo kutokana na Umri aliokua nao wakati akirekodi album hiyo. Ndani ya album hii kulikua na ngoma Hits ambazo zilimtambulisha Vyema Adele katika Muziki, ngoma hizo ni “Hometown Glory” na “Chasing Pavements” na ndani ya mwaka huo huo 2008 mwezi March alipata Deal kutokea Colombia Records na XL record na baadae alinza Tour yake aliyoipatia jina la ‘An Evening with Adele’ ambapo tour hiyo ilimalizika mwezi June mwaka 2009.

Mnamo Mwezi January mwaka 2011 aliachia album yake ya pili 21 ambapo tena aliita album yake hiyo jina la 21 akiwa anamaanisha alikua na Umri wa Miaka 21 wakati akirekodi album hii. Album yake hii ilipata Mwitikio mkubwa sana ulimwenguni kote. Ndani ya Album hii Kulikua na Ngoma KALI mbili ambazo ndizo ziliuza album hii vilivyo katika masoko ya UK na Marekani, nyimbo hizo ni “Rolling in the Deep” na ‘Someone Like You”.

Pia ndani ya Album yake hiyo kulikua na Ngoma ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100.

Mwaka 2012 aliandika wimbo mpya ambao wimbo huo ulitumika kama Sound Track kwenye Movi moja ya James Bond iliyojulikana kwa jina la Skyfall. Adele aliamua pia kutumia Jina la Skyfall kama jina la wimbo wake huo. Wimbo huo pia ulifanikiwa kuingia katika chati za Billboard Hot 100 nakushika nafasi ya 8 na alifanikiwa kuuza zaidi ya copy zaidi ya milioni Moja ndani ya siku tatu za Kwanza nchini Marekani.

Mafanikio aliyoyapata katika Muziki.

–> Album yake 21 iliuzwa zaidi ya 3.4 milioni huko UK na kufanikiwa kuweka Rekodi ya Album iliyopata mauzo mengi katika karne hii ya 21. Pia ilimfanya Adele Kuwa msanii aliyeuza kopi milion Tatu ndani ya Mwaka mmoja Tuu huko UK.

–> Mwaka 2009 alipokea Tuzo za mbili za Grammy kama ‘Best New Artist’ na ‘Best Female Pop Vocal Performance’.

–> Mwaka 2012 alitangazwa na Gazeti moja nchini Marekani “TIME” kama mmoja kati ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.

–> Pia wimbo wake Skyfall ulimpatia Award kutoka Academy Award katika kipengele cha wimbo Bora a mwaka.

Maisha yake Binafsi.

Mwaka 2012 alitangaza kuwa katika mahusino na Mfanya biashara Simon Konecki na baadae ikatangazwa kwamba wapenzi hao wanatarajia kupata mtoto na kweli walipata mtoto wao wa kwanza alopewa jina la Angelo.

Adele anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Kiashi cha dola za kimarekani milion 75. Pia anajihusisha na charities mbali mbali. na Badhi ya charities anazojihusisha nazo ni zile za Muziki zaidi. Na amekua akifanya shows ili kukuza charities hizo.

Kwa sasa Mwanamuzi huyu anatamba na Vibao vyake latest kama vile HELLO, na kile kibao maridhawa cha SEND MY LOVE.

Video hiyo ina miezi Nane tuu katika mtandao wa Youtube na Imefanikiwa kutazamwa mara 338,655,357.

Na Huyo ndiye Adele, Makala hii imeandikwa na kuchapishwa na Francis Mawere mti mkavu usio-chimbwa dawa, nifuate twitter pia kama @Mawere3

AdvertisementMtokambali 728x90