Tangazo

Kujua jinsi ya kusoma alama za nyakati ni kujua wakati gani ufunge ukurasa mmoja na kufungua mwingine, wakati gani wa kufanya maamuzi magumu na kusema INATOSHA badala ya kuendelea kukubali kuwa MISTREATED .

Kuna wakati unaweza kumkuta mtu yupo kwenye mahusiano yenye kila aina ya karaha na unyanyasaji lakini bado yupo tu na wala hafikirii kuondoka na sio kwasababu hataki bali kwa sababu anakosa ujasiri/msukumo wa kufanya maamuzi na kujitoa kwenye mahusiano hayo. Unakuta mtu anatukanwa… anapigwa… anadharauliwa… anasimangwa… yani kwa ujumla anaonyeshwa kila dalili za kuchokwa ama kutotakwa tena na aliyenae lakini anaendelea kubaki palepale.

Katika hali ya kawaida, uvumilivu ni kitu cha muhimu sana kwenye mahusiano lakini sio hata pale mtu unapofanyiwa vituko vilivyovuka kiwango. Unapaswa  mtu kujifunza  kusoma alama za nyakati bila ya kumtengenezea mwenza wako ‘excuses’ za kwanini anakutreat vibaya kwasababu hakuna anaestahili kufanyiwa vibaya na mpenzi wake. Kuna vitu ambavyo mwenzi wako akianza kuvifanya tena kwa kuvirudia rudia unatakiwa ujue kwamba hapa sitakikani tena na utafute jinsi ya kujitoa, tena haraka. Ndio maana wahenga walisema ”Akufukuzae hakuambii ondoka.” usisubiri kufukuzwa kama mbwa, ni juu yako kuondoka kabla hujafukuzwa. Maana mara nyingi mtu atakufanyia visa akijua kwamba ikiwa utachoka visa vyake utaondoka mwenyewe…ila sasa kuna wale wenzangu na mie wanaoamini na kujipa moyo wa mabadiliko hata pasipo na nia wala matarajio ya mabadiliko. Unavumilia manyanyaso ukijua kesho itakua bora ya jana alafu matokeo yake jana inageuka bora ya leo pale unapovunjwa moyo kabisa n ahata kuaibishwa.

Ni wakati  tujifunze kusema inatosha na tuache kua ving’ang’anizi. Jiamini kwamba ulivyompata huyo ndivyo ambavyo utampata mwingine. Usiishi kwa mateso, wasiwasi na hofu ya kutokupendwa tena kwasababu hujui kuna kizuri gani kinachokusubiria nje ya mahusiano mabaya uliyomo sasa hivi. Na hicho kitu kizuri hakiwezi kujitokeza bila wewe kuweka nafasi hiyo wazi! Hamna mtu anaestahili kulala akilia kila siku au kutokua na furaha kwasababu ya binadamu mwenzake. Ukiona mtu hakufai ama anakutreat kama vile hufai na huna hadhi ya kupendwa na kujaliwa achana nae.

Athari za kuruhusu mtu mwingine akufanyie vile apendavyo bila kujali hisia zako, bila kujali anakuumiza kwa kiasi gani ama anakuchoresha kwa kiasi gani kwa watu wengine ni kwamba itafika mahali wewe mwenyewe utajiona hufai kwa lolote.

Self-esteem na Confidence yako vitakuwa chini. Utajiona kuwa huna hadhi ya kupendwa. Na  hata wewe mwenyewe hutojipenda kwasababu ukijipenda utajijali, na ukijijali hutoruhusu mtu mwingine akuaminishe kwamba huna thamani kama watu wengine.

Mtu anaekupenda kweli atakujali kwa kila namna na kila hali. Atakuinua pale utakapokuwa chini badala ya kukukandamiza Zaidi, atajitahidi kukufurahisha kadiri ya uwezo wake badala ya kukupa huzuni muda wote etc. etc.

Kuwa jasiri, usimpe mtu mwingine nafasi ya kuyaendesha maisha yako atakavyo yeye, hiyo ni kazi yako na yako pekee.

Ukitaka furaha itafute, usikumbatie majonzi moyoni mwako kwa woga wa kutokupendwa. Na Zaidi, usisubiri kuvunjwa moyo wako uishie kuokota vipande viapande….ondoka na moyo wako ukiwa bado mzima ukatafute atakaeupa furaha na amani mbele ya safari!!

AdvertisementMtokambali 728x90