Jinsi ya kufungua blog
mtokambali.com
Tangazo

Nafahamu watu wengi hususani vijana wanatamani kumiliki blog lakini hawafamu jinsi ya kufungua blog kabisa. Ziko sababu nyingi za wewe kumiliki blog yako leo hii.

Je unataka kufahamu jinsi ya Kufungua Blog yako leo?

BLUEHOST ndipo mahala pekee nilipoanzishia Blog yangu hii na leo nitakuonyesha jinsi ya kufungua blog yako hatua kwa hatua bila msaada wowote.

Kabla hatujaanza hatua moja baada ya nyingine,

Kuna mambo kadhaa ya kufahamu kabla ya kufungua blog yako na mambo hayo ni DHUMUNI LA KUFUNGUA BLOG YAKO HIYO, UCHAGUZI SAHIHI WA JINA LA BLOG YAKO, NI WAPI UTAPATA SITE NZURI KWA AJILI YA HOSTING, JE UNAJIWEZA KIKAMILIFU KATIKA KILE UNACHOTAKA KUKIANZISHA?

Kwa kuweza kuanisha mambo hayo, basi kazi hii itakua rahisi mno kuliko maana mahitaji muhimu teyari utakua nayo na kilichobakia ni kufanya vitu vitokee.

MUHIMU: Katika chapisho hili sintozungumzia kufungua Blog katika zile FREE SITES kama Blogspots, Tumblur n.k. Hapa nazungumzia zile SELF HOSTED SITES tuu(Yaani zile Blog ambazo mtu anakua anamiliki kwa asilimia 100, ana Domain name na kafanya Hosting mwenyewe). Hivyo ni lazima utambue kwamba Utahitaji kutumia Fedha.

Uko teyari? haya twende..

Mahitaji Ni kama yafuatavyo:-

Ni vyema ukayaandika mahitaji haya kwenye karatasi pembeni kama Checklist yako ili kuepusha kusahau baadhi ya mambo.

1.Domain Name.

Domain name ni Anwani ya blog yako mfano www.jinalablogyako.com au www.jinalablogyako.co n.k

2.Hosting

Host ni mahali ambapo Blog yako itatakiwa kuwepo ama kwa lugha nyingine ni kama sehemu ambapo Blog yako itahidhiwa na Kukulia. Huduma hii ya Hosting inatolewa na makampuni mengi ulimwenguni hivyo utakua na Uwanja mpana sana wa kuchagua. Mimi nakushauri BLUEHOST nitakueleza ni kwa nini BLUEHOST mbeleni

3.Theme

Theme ni muonekano wa blog yako,

Mpaka hapo tupo pamoja si ndio? haya tuanze kufungua blog yetu hatua kwa hatua bila msaada wowote.

1> Nunua Domain na Hosting.

Kama nilivyokuanishia mambo haya hapo juu, basi hatua ya kwanza ni kufanya manunuzi ya mahitaji yetu. Unaweza kununua Domain yako kutoka katika Site tofauti na Hosting site ama ukanunua Domain yako kutoka katika Hosting site uliyoichagua.

Hapa utaweza kuchanganyikiwa kidogo lakini usihofu maana BLUEHOST wanafanya mambo kwenda kirahisi zaidi kwa kua Mambo haya yote yanawekwa katika kifurushi kimoja, na habari njema ni kwamba utakapoamua Kuhost blog yako na BLUEHOST basi hukuna haja ya kununua Domain kwakua DOMAIN ni Bure kabisa.

Bofya >> Bluehost kuanza hatua hii. Au Bonyeza kitufe cha Kijani Get Started Now kama kinavyo onekana hapo chini.blog hosting setup one

Baada ya Kuingia Bluehost na kubofya Kitufe get Stated now utaingia moja kwa moja katika ukurasa wa kuandikisha Domain yako ambayo utapenda Kuitumia mfano www.blogyako.comblog hosting setup twoBaada ya kuchagua Domain yako, basi utaingia hatua yakujaza Details zako kwa ajili ya Malipo ya kifurushi chako hicho na kumbuka kwamba malipo haya utalipia kwa mwaka mmoja ama miaka miwilii ama mitatu utachagua mwenyewe. Hakikisha Details zako ni sahihi kabisa.

Kama unavyoona katika picha hapo chini, ni kwamba katika Kifurushi hicho kuna mambo mengi ya ziada ambayo hayana umuhimu hivyo utalazimika kuyaondoa na Kubaki na DOMAIN PRIVACY PROTECTION kwa ajili ya usalama na Ulinzi wa Domain yako. Ondoa alama za Vyema katika vipengele vyote ila tuu acha kipengele cha DOMAIN PRIVACY PROTECTION. Na kumbuka kwamba Utachagua Ulipie kifurushi hicho kwa Miezi 36, au Miezi 24 ama mwaka mmoja(Itategemea na mfuko wako)

blog hosting wordpress setup

Baada ya Kulipia kila kitu na kufanikiwa, basi tuendelee na Hatua ya Pili.

2>Kuweka(Install) wordpress kwenye Control panel(cPanel) yako.

Baada ya kufanikiwa kulipia kifurushi chetu, basi hatua inayofuata ni kuweka WORDPRESS kwenye kifurushi chetu. WordPress ni nini? WordPress ni Mfumo utumikao katika uandishi wa Post(Machapisho). Hivyo hutoweza Kuchapisha Post zako kama hautokua na mfumo huu. Sasa tuendelee…

Mwanzoni mwa hatua hii utadhani kwamba utashindwa na kuchanganya mambo lakini usiogope maana unaweza kuachana na kila kitu hapa kwa asilimia 95 kwakuwa hayatuhusu.

MUHIMU:Unaweza kuwa-ambia blueHost wakusaidie hatua hii. Kuna ujumbe utajitokeza wakati umeingia hatua hii ya pili kama unavyo onekana hapo chini ila Achana nao maana kazi hii tunaifanya sisi peke yetu maana tunaweza si ndio?

do it for me

Shuka mpaka utakapoona kitufe kilichoandikwa Install WordPress. Mfumo wa BLUEHOST ni mfumo wenye Teknolojia ya hali ya Juu maana kazi hii utaifanya kwa dakika chache mno bila kuwa na msaada.Install WordPress

Sasa baada ya WordPress Kuwekwa(Instilled) kwenye kifurushi chako, hatua inayofuata ni Kuweka JINA LA BLOG YAKO na mambo mengine kama picha hiyo hapo chini inavyoeleza.install wordpress on host

Baada ya kuweka WordPress, Utaona ujumbe umejitokeza Kwenye screen yako na ujumbe huu utakonyesha namna gani utaweza Kuingia katika blog yako hiyo na watakupa Link ya kuingia ambapo link hiyo itakua kama hii kwa mfano http://jinalablogyako.com/wp-admin.

Mpaka hapo utakua umemaliza Kazi, na teyari una blog yako teyari. Twende hatua ya Tatu.

3>Badilisha theme(mwonekano) kisha anza kuchapisha post zako.

Kumbuka kwamba ndani ya WordPress kuna Thems za Bure kabisa ambazo utaweza kuzitumia kwa kadiri uwezavyo ila Kumbuka kwa BURE siku zote sio Nzuri.

Najua uataanza kuniuliza ni wapi nitaweza kupata theme nzuri? Basi jibu la swali lako THEMEFOREST wanalo(Bofya Hapa kuingia Themeforest). Utachagua theme nzuri unayoipenda kisha utailipia na Kuipakua(Download).

Baada ya hapo kitendo cha kununua theme yako, basi hatua inayofuata ni kuiweka(install) theme yako kwenye blog yako.

Ingia kwenye blog yako kwakutumia ile link uliyopatiwa wakati ulipomaliza kuinstall worpress yaani mfano www.jinalablogyako.com/wp-admin. Ukishaingia moja kwa moja nenda kwenye kipengele kilichandikwa APPEARANCE > THEMES > ADD NEW baada ya hapo utaona kipengele kilichoandikwa UPLOAD THEME basi hapo uta-Upload theme yako kisha utabofya kipengele cha ACTIVATE THEME NOW na mpaka hapo kilichobakia ni kuipendezesha Blog yako tuu.

Au

Kama hautoweza kuiupload hiyo theme yako basi unaweza kutumia nji ya APPEARANCE > THEMES > ADD NEW kisha utabofya Sehemu ya kutafuta theme unayoipenda kisha ukiipata utaibofya hiyo theme na Kuiactivate. Angalia picha hii hapo chini.

install theme

Hongera kwa kufanikisha kufungua Blog yako, Sasa anza kuandika. Kumbuka kuwashirikisha wengine Jinsi ya kufungua blog yako kwa hatua chache tuu bila hata msaada.

Je una swali lolote la kuniuliza kuhusiana na Mada hii?? Tafadhali niulize katika coment Box hapo chini nitakujibu kwa kadiri niwezavyo.

AdvertisementMtokambali 728x90

10 COMMENTS

  • Hi Simon!
   1.Kuhusiana na Gharama inategemea na Hosting company(Kampuni ambayo Blog yako itakua kwa Muda wote) mfano mimi nimeongela Bluehost ambapo utapaswa Kutembelea Huduma zao ziko wazi kabisa

   2.Faida utakazopata kupitia Blog yako hiyo ni nyingi mno ikiwa tuu utajizatiti kikamilifu. Ziko njia njingi za kutengeneza Kipato kupitia Blog yako kama Vile Matangazo(Adsence, na yale matangazo ya Kawaida kutoka kwa wadau watakaopenda kutangaza biasha zao katika Blog yako), Unaweza kuwa wakala wa makampuni Fulani Mfano Amazon Ambapo watakupatia matangazo ya Bidhaa zinazoendana na Blog yako kisha kama kuna msomaji wa blog yako hiyo akaliona tangazo hilo na kununua bidhaa hiyo kupitia tangazo hilo basi wewe utapata asilimia kadhaa katika mauzo ya bidhaa hiyo.

   Yapo mengi zaidi ya kufanya ila cha msingi umetengeneza Blog yako hiyo na kuikuza kisha ndipo uanze kufikiria kipato kutoka katika blog yako hiyo.

 1. chapisho zuri ila huna haja ya kutumia pesa yako.domain name huweza kupatikana BURE!! PIA huduma za hosting huweza kupatikana bure!!! kabisa

Comments are closed.