Jinsi ya kurudisha maisha yako baada ya KUACHANA!!

Tangazo

“The sooner you get out of a bad investiment the better.”

Mahusiano ni kama ‘shared business investiment’ kati ya watu wawili. Hiyo inafanya iwezekane kwamba wote wakachangia sawa kwa sawa katika kufanikisha mahusiano hayo na pia kugawana ‘faida’ sawa sawa (50/50) vile vile au mmoja akachangia zaidi ya mwenzake na bado yeye ndio akapata faida kidogo au hata mwingine akawa hachangii kabisa katika kufanikisha na  kuendeleza mahusiano hayo ila akategemea/akataka mahusiano yao yaendelee kufanikiwa huku akitegemea faida yake kama kawaida.

Kwa bahati mbaya namba ya wanaojikuta kwenye mkataba wa ‘Kazi YAKO,faida YETU/YANGU’ ni kubwa kuliko ambavyo wengi wetu tungependa iwe. Mtu anajikuta anatoa muda mwingi, pesa na hisia au hata kupoteza mahusiano yake mengine (ndugu na marafiki) ili kujenga mahusiano ambayo hayana faida kwake na wala hayana matumaini ya kwenda popote kwa kutokujua kwamba kwa mwenzie ile ni sehemu ya kujipumzisha tu na sio makazi ya kudumu hivyo haoni sababu ya kuchangia na kulinda mchango wake. Wengine hufikia hata kuuza/toa shea kwa siri (mpango wa nje a.k.a mchepuko) kinyume na makubaliano.

Kuna wakati utafika mtu mwenye akili zake timamu atashtuka na kugundua kwamba alipowekeza hapafai  “he/she made a bad investiment”  na matokeo yake ni hasara tupu hivyo muda wa kujitoa na kuangalia mambo mengine umefika. Sasa hapo ndipo kazi inapoanza. . . baada ya kujitoa kihisia, kimwili na kiakili, kupoteza muda na hata hela, kupotea marafiki au hata ndugu kwa kuwa kwenye mahusiano ambayo pengine hawakuyapenda tangu mwanzo na kubadili mipango binafsi, kuanza upya sio rahisi hata kidogo.

So, ufanye nini kukabiliana na maumivu uliyopata . . . . . ?

KUBALI MATOKEO (Accept the fact that it’s over.)Usipoweza KUKUBALI kwamba mahusiano yenu yamefeli hutoweza kupata amani na kuweza kuona mwanga mbeleni.

USING’ANG’ANE NA YALIYOPITA (Do NOT dwell on the past.) NDIO, ulijitoa sana na kwa mengi ila kukaa ukiyafikiria na kuyahesabu kila saa hayatokusaidia kuendelea mbele. . . yatakufanya utakwama (stuck) katikati ya YALIYOKUWA na YAWEZAYO KUWA.

Jiweke mbali na wakati uliopita (Distance yourself from the past.) Yeahh we are supposed to LEARN from the past but NOT live IN or WITH it.  Hivyo ni wazo zuri kujiweka mbali kidogo na huyo uliyekua nae kabla ili asiwe wingu/pazia/kikwazo cha kukuzuia kuona mbele.

JITAFUTE UPYA (Rediscover yourself.) Baada ya kutumia muda mwingi kuwa MKE/MUME/MPENZI WA FULANI fanya jitihada za kurudi kuwa FULANI tu. Kwa maana ya kwamba kabla hujawa mke/mume/mpenzi wa fulani ulikua wewe. . kama una bahati basi ulikua mtu ULIYEJITOSHELEZA, yani furaha yako ilitoka kwako na sio kwa fulani. Sasa rudi huko ili uweze kujitosheleza tena ili upate amani na furaha isiyotegemea watu/mtu mwingine.

JIPE MAPUMZIKO (Take a break.) Give yourself a break. Mapumziko kwenye swala zima la mahusiano ni muhimu sana,jipe muda wa kutosha kuwa mwenyewe badala ya kukimbilia mahusiano mengine papo kwa hapo (right away).                         Hata kikazi kama unaweza kuchukua likizo kidogo chukua ili usije ukaharibu utendaji wako wa kazi  au angalau ‘go way for the weekend’.  Hii itakupa muda wa kuweza kujitambua tena, kujua unachokitaka/hitaji katika maisha yako katika mahusiano ili baadae usije ukaishia kubeba mzigo mwingine ambao hauna faida kwako.

RUHUSU WANAOKUPENDA KUWA KARIBU NA WEWE (Allow those who loves you to be there for you.) Sio lazima uongelee mambo usiyotaka/jisikia kuongelea kwa wakati huo. . .just let them hold your hand, give you hugs, be there if that’s what you need.

USIJILAUMU (Do not blame yourself.) “Ningejua ninge.  .  . hivi au vile” will only hold you back. Maisha ni darasa hivyo jifunze kutokana na yale uliyofanya, ambayo hukufanya, uliyofanyiwa, ambayo hukufanyiwa kisha usonge mbele (move on).

And last but not least BE HAPPY!!!!Na kama ambavyo mimi hupenda kusema 


By Malkia Sun
Insta:malkiasun
 

Tafadhali tupe maoni yako kuhusiana na mada hii katika sehemu ya comment…


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


 

AdvertisementMtokambali 728x90