Tangazo

Steve Jobs ni moja kati ya watu walio wahi kuwa Maarufu katika ulimwengu wa teknologia na Amekuwa mfano wa kuigwa na kazi zake zimekuwa changamoto katika ulimwengu wa Sayansi. Watu wengi wamekuwa wakihamasika kupitia speech zake alizokuwa akitoa katika mikutano mbali mbali ya kibiashara na hata katika teknologia Alifariki mnamo mwaka 2011 akiwa na umri wa mika 56.

Mimi nimekuwa mmoja kati ya watu ambao wamekuwa wakihamasika kutokana na speech za Job na ndio maana mpaka leo nzaidi kumfuatilia maana nafahamu sinto weza kukosa kitu kutoka kwake, namaanisha “ukitaka kunukia basi kaa karibu na Waridi”

Basi leo acha nikupe mambo tisa ya kujifunza kutoka kwa Steve Jobs

1.Futa nafsi yako(Follow your heart).

Embu kuwa na maono juu ya kile unacho kiamini kwamba unakiweza, weka malengo yako ambayo yatakufikisha kule uliko tamani kufika siku zote za maisha yako, fanya mwenyewe ili kuyaona machungu ya kazi yako pasipo kuingiliwa na mtu yeyote. Amini kama unaweza. Kumbuka mafanikio hayaji kwa kukata tamaa bali huja kwa kuongeza nia na ghadhabu katika kazi zako.

Karibu kila kitu, kila mataraijio yako, Furaha ya umoja, Hofu yeyote yakuharibiwa ama Kufeli- Hivi ni vitu ambavyo huangukia mbali mbele ya uso wa kifo, Acha kile tuu kilicho na umuhimu, Kumbuka unakwenda kufa katika njia ambayo unafikiria kwamba utapoteza kitu ulicho nacho. Teyari umekwisha achwa Mtupu(Uchi). Hakuna sababu ya wewe kutoacha kuusikiliza Moyo wako ama nafsi yakoSteve Jobs

 

2.Jiamini peke yako(Trust yourself).

Tunapo kuja katika kipengele hichi ni lazima mtu ajikubali kwanza kwamba anaweza kusimama yeye kama yeye katika Vission(maono yake) na zaidi ya yote aweze kusimama katika kutimiza ndito zake kwa vitendo, hivyo swala la kujiamini la muhimu sana. Umeamua kufanya biashara na kuacha kazi ofisini usiogope we fanya biashara maana kile ulicho kitaka katika maisha yako yote kitakuwa katika hiyo biashara endapo tuu utaamua kufanya hivyo. Njia nzuri ya mtu kujifunza ni kufanya makosa na kisha kujifunza kutokana na makosa.

Huwezi kuunganisha nukta(.) ukiwa unangalia mbele, utaweza tuu kuziunganisha ukiwa unaangalia nyuma. Hivyo unapaswa kuziamini nukta hizo maana zitakuunganisha baadae katika maisha.Unapaswa kuamini katika kitu iwe ni Kipaji/kipawa, Maisha, ama chochote kile. Hali hii haijawahi kuniangusha, ni ndiyo iliyofanya mimi kua hapa leo-Steve Jobs

 

3.Penda kile unacho kifanya (Love what you Do).

Mafanikio siku zote huja kwa kupenda kile unacho kifanya, naamini kabisa endapo utapenda kile unacho kifanya kwa moyo wako na akili zako basi chance ya wewe kufanikiwa ni kubwa kuliko yule ambae anafanya kitu ambacho moyo wake hauridhiki. Ngoja nikupe mfano hai( Mimi nilipo hitimu chuo cha mafunzo ya Utabibu, niliamua kusitisha kujihusisha na mambo ya hosipitalini pamoja na Madawa na badala yake niliamua kuwa Blogger…. mmh maajabu eeh!) hii yote ilisababishwa na mimi kuamini kwamba mafanikio yangu yatakuja katika kile nachopenda kukifanya(Blogging).

Kazi yako inakwenda kujaza sehemu kubwa ya maisha yako, na njia pekee ya wewe kurizika moja kwa moja ni kufanya ile kazi unayo amini ni kazi kwako. Na jia pekee kufanya kazi hiyo ni Kuipenda kazi hiyo. -Steve Jobs

 

4.Usidharau Ubora wa kazi yako.

Kitika maisha yako yote kamwe usizarau ubora. Ubora ni zaidi kuliko kiasi. Fanya kazi zako kwa bidii na hakikisha unazalisha mazao yenye Ubora na siyo tuu bora mazao. Umeamua kufanya kitu basi hakikisha umekitendea haki. Jambo hili litakuletea mafanikio makubwa katika maisha yako.

5.Fanya uchaguzi kwa makini(Pick carefully)

Kuwa bize, fanya mambo yako, futa yale mambo ambayo ni ya msingi tuu achana na hayo mengine, muda wako mwingi uwe ni wakujifunza mambo ya maendeleo tuu, epuka vitu vinavyo kusabisha kupoteza muda mfano kuangalia Tv kwa muda mrefu, Kufuatilia habari za udaku, kupoteza muda mwingi kwenye social medias ukitafuta new updates n.k.

People think focus means saying yes to the thing you’ve got to focus on.It means saying no to the hundred other good ideas that there are. Youhave to pick carefully. -Steve Jobs

 

6.Fanya kazi kwa bidii kurahisisha mambo

Kuna nguvu yakutengeneza kile unacho kiamini kwamba ndicho utakacho kifaya katika maisha yako. Fanya kazi kwa bidii na mwisho wa siku utasimama mbele ya umati wa watu na kuzungumza kitu chenye sura na mtazamo chanya wa kazi yako. Pangilia magumu yako yote katika kazi zako na kisha yatendee kazi na kuyatatua na mwisho wa siku kila kitu kitakaa katika mstari wake kama inayo takiwa kuwa.

7.Iba/iga/chukua idea kubwa( Steal great ideas).

Unajua wakati mwingine kama kitu kimekupendeza na kinaendana na wewe, siyo mbaya ukakichukua na kukifanyia kazi kikamilifu. Jifunze Mengi kutika kwa watu wenye fikra kubwa , fanya mengi ya kuiga kutoka kwao na mwishoni na wewe utaweza kubadilisha idea zile zikawa mafanikio yako na ikawa ni rahisi kwako wewe kuwa pahala ulipotamani kuwa katika maisha yako yote.

Siku zote Tumekua waoga na wenye aibu kuiba idea kubwa -Steve Jobs

 

8.Lengo lako lisiwe ni Kutengeneza hela kwanza (Your goal isn’t to make money).

Usiweke pesa mbele bali tumia muda wako kutengeneza na kukuza jina pamoja na kazi zako. Watu watakuja kuiga ujuzi na kukuukiza maswali na kujifunza kutoka kwako na mwisho wa siku pesa zitakuaja tuu(Kizuri cha jiuza na kibaya chajitembeza, na pesa huja baada ya mafanikio).

Apple’s goal isn’t to make money. Our goal is to design and develop and bring to market good products. We trust as a consequence of that, people will like them, and as another consequence, we’ll make some money.

 

9.Usipoteze Tumaini/imani(Don’t lose faith)

Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, bayana yasiyo onekana. Unapokua ukifanya kazi zako, kuna muda uanatamani kukata tamaa na kupoteza tumaini.. lakini hupaswi kuiruhusu hali hivyo iwepo katiaka kazi zako. Kumbuka pale unapokuwa ukikata tamaa, ndipo mafanikio yako huwepo ama huwa karibu. Jiulize na kujitazama ulikotoka na hapo ulipo.

Wakati mwingine Maisha yanaweza kukugonga kwa tofali kichwani mwako.Usipoteze tumaini. -Steve Jobs

 

Kwa leo nimetia nanga na meli iko bandarini, ni matumaini yangu umejifunza kitu katika post hii,ningeomba unachie maoni ama ushauri hapo chini kama utakuwa nayo, basi tukutane tena panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Ni mimi Swahiba wako Francis Mawere

 

AdvertisementMtokambali 728x90