Connect with us

Kwanza nipende kukusalimu ewe mtanzania mwenzangu kwa kwakusema uu hali gani? Ni matumaini yangu yakwamba uu mzuima na buheri wa afya ingawaje sii asilimia mia moja ni jambo lakumshukuru MUNGU kwani hapa tulipo sii kwa akili zetu wala kwa ujanja wetu bali ni kwa neema tuu.
Basi kwa kuyasema hayo ambayo ni salamu zangu kwako wewe mtoka mbali , twende moja kwa moja kwenye mada yetu ambayo teyari nimeiwasilisha kupitia kichwa cha habari hapo juu yakwamba KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA.
Ni wazi kwamba neno MAISHA sii neno geni masikioni mwetu yakwamba kila mmoja wetu amekua akihangaika hapa na pale, usiku na mchana hii yote ni sababu ya maisha. Nuliwahi kumsikia mzazi mmoja akimweleza mwanae yakwamba ” Mwanangu kuwa uyaone” name nikajiuliza, Je akue ayaone nini? Magari au majumba? Kumbe alikua akimaanisha MAISHA.
Maisha ya kijana Mtanzania wa leo yamekua kama kitendawili ambacho kimekosa mtu wakukitegua. Je tumpe nani mji ili aweze Kukitegua? Yapo mamba mengi yanayo sababisha maisha kuwa magumu au yasiyo na mwelekeo kwa vijana walio wengi na mambo hayo yanatokana na vijana wenyewe na mifumo mibovu ya elimu wapewazo nijana hawa huko mashuleni hasa hasa katika shule za msingi na zile za sekondari.
Kijana mwenyewe anawezaje kuyaharibu maisha yake?
Yapo mambo mengi mno ambayo kijana akishindwa kuyazingatia wakati wa makuzi yake yanampelekea kija moja kwa moja kupoteza mwelekeo wake katika masha. Mambo hayo ni kama vile : kuto kuweka malengo sahihi katika maisha, Kufuata mkumbo, tamaa mbaya, na mtazamo hasi tuliyo nayo vichwani mwetu. Hayo ni mambo baadhi ambayo kijana mwenyewe anaweza kujisabishia maisha yake kuharibika.
Kutokuwa na malengo. Kati ya makosa makuu ambayo vijana wengi wanafanya ni kutokuwa na malengo katika maisha yao, na ni wazi yakwamba vijana wengi tumejikuta hatuna malengo sahihi katika maisha yetu ya kila siku, unakutana kijana mtaani amekaa magengeni kwanzia mwanzo wa siku hadi mwisho wa siku hana lolote. Kuwa na malengo ni jambo muhimu mno katiaka maisha ya kila mwanadamu na tambua yakwamba kila aliefanikiwa katika maisha alijiwekea malengo thabiti na akayafuatilia vilivyo kuhakikisha yanatimia. Kumbuka yakua malengo yanendana na ndoto ulizo nazo wewe kama kijana. Ili ndoto yako itimia ni lazima uwe na malengo. Sasa pale kijana anaposhindwa kuwa na malengo ya kweli ndipo anapojikuta akihangaika huku na kule bila mafanikio yeyote. Ikumbukwe kuwa maisha ni vile unavyoishi na wewe mwenyewe ndiye utakae hamua yakua maisha yako yawe mazuri au mabala “hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako kijana”.
Labda ni kwa nini kijana anashindwa kuwa na malengo hai katika maisha?
Mara nyingi kijana anakua na tamaa na vishawishi visivyokua na maana. Kama nlivyosema malengo yanawekwa kutokana na ndoto alizo nazo kijana sasa kama huna ndoto na msimamo yakwamba usimamie nini hasa katika maisha ili aweze kujikwamua katika hali ngumu yaki maisha. Tama za hapa na pale na kufuata mkumbo ni vitu ambavyo hupoteza ndoto za vijana wengi, inafika pahala kijana anakuwa anatamaini vitu vingine ambavyo vipo njee ya uwezo wake na kumpelekea kuachana na ndoto zake za mwanzoni na kujiingiza katika vitendo viovu ili kuvipata vitu hivyo.
Kutokuweza kufahamu thamani ya muda; Nipende kuchukua nukuu ya mtu mmoja aliye kuwa maarufu duniani kwa kupitia filamu na huyu sii mwingine ni BRUCE-LEE ambae aliwahi kusema “if you truly love life never play with time coz there is your life originate” vijana wengi tumekuwa tukijikuta tukipoteza muda katika mambo yasiyokuwa na tija katika maisha yetu. Jiulize huko kwenye mitandao yakijamii unapokuwa muda wote huo unafaidika vipi? Ndio yawezekana kuna kitu unafaidika nacho lakini kiuhalisia jambo hilo halikusaidii kukukwamua huko ulipo kama unvyotarajia. Kati ya mali tulizo nazo hapa duniani moja wapo ni Muda. Muda ukiutumia vizuri hakika utafanikisha malengo kwa wakati unao taka wewe lakini pindi ukiutumia vibaya hakika utajuta kwan muda ukisha kwenda haurudi nyuma kamwe. Sasa nacho taka kusema hapa ni kwamba muda sio rafiki ndugu yangu.
Kutokujiami kama tunaweza peke yetu: katika swala lakujiamini, nimekua nikiliona katika vijana tulio wengi yakua tunakua tukishindwa kujiamini kama peke yetu hatuwezi kabisa. Nipende kuwaambia vijana wenzangu kua tukiishi katika misingi yakutokujiamini tutakua tumeshindwa nakuanguka kimaisha. Unakuta mtu ana fursa katika jamii lakini kijana huyo anaogopa kuichukua fursa ile nauifanyia kazi ili iweze kumwokoa hapo alipo. Watu maarufu duniani waliziona fursa kati yao na wakajaribu na hatimae wakafikia kilele cha mafanikio. Ondoa dhana ya uoga na thubutu kufanya na nakuhakikishia utafikia lengo lango. Acha kujiona huna nguvu wala akili na ukifanya watu watakuonaje. We unadhani Mwalimu JK Nyerere angekua na uoga mbele ya wakoloni leo hii tungekua wapi? Ni mfano tuu ambao tunautoa kutoka kwa baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere kwani aliionoa fursa yakudai uhuru wa Tanganyika ndipo akajaribu bila uoga na mwisho wa siku leo hii Tanzania tunatembea vifua mbele.
Kukataa shule; Niliwahi kuulizwa swali na Mtu mmoja swali ambalo liliniumiza kichwa wakati nlipokua natafuta jibu lake na swali hilo ni “do you think education is certificate in your life?” nikuachie nami hili swali ujibu mwenyewe lakini sintokupatia jibu nlililomjibu mtu Yule. Nipende kuambia kijana mwenzangu ambaye una kataa shule katika dunia ya leo tuna kufananisha na kipofu. Leo hii nani atakuajiri kama hauna elimu? Ndio unaweza kwa namna moja ama nyingine ukajiajiri lakini ukweli ni kwamba hata kujiari kunahitaji elimu. Ubongo wa mwanadamu una ujazo wa lita moja na nusu lakini kalamu na karatasi vina weza kuujaza ubongo huo kwa muda mchache mmno. Nakushangaa sana kwani hata maandiko ya MUNGU yametuambia “mshike sana elimu usimwache aende zake maana yeye ndiye mkombozi wa maisha yako” ni maandiko yakutoka katika vitabu takatifu na sio maneno yangu mimi Mtokambali. Nipende kukuambia kijana mwenzangu Elimu iwe msingi wa maendeleo yako wewe kijana.
Hayo niliyo yasema hapo juu ni baadhi tuu ya mambo ambayo yanaweza kukufanya wewe kijan kuharibu maisha yako kwa ujumla. Nakuahidi katika mwendelezo wa makala hii katika mfululizo wa makala zetu hapa MTOKA MBALI nitakuelezea mambo zaidi yatakayoweza kukuangusha wewe kijana katika maisha yako na jinsi gani utaweza kujikwamua kaitika hayo mambo na kutoka katika UTUMWA wa fikra.
Nipende kukushukuru wewe ulie chukua muda wako ulio wa thamani na kusoma makala hii. Nina amini umepata kitu hapo. Nikusihi kaa hapa hapa kwa vitu moto moto.

But I must explain to you how all this mistaken idea of denouncing pleasure and praising pain was born and I will give you a complete account of the system, and expound the explorer of the truth, the master-builder of human happiness. No one rejects, dislikes, or avoids pleasure itself, because it is pleasure, but because those who do not know how to pursue pleasure rationally encounter consequences that are extremely painful.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LifeStyle

Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.

Published

on

Well well well! Karibu tena MTOKAMBALI, imekua kitambo sasa tangu nmeondoka hapa Mtokambali na leo nmerudi tena na nmekuja kukupatia kile ulichokikosa kutoka kwangu. Kwanza nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye hai kwa kunifanya kuiona tena siku hii nikiwa na Afya na Amani Moyoni mwangu, sii kwa akili zangu ama kwa ujanja wangu kufikia hapa nilipo ila ni kwa NEEMA tuu. Nikushukuru ewe mpenzi msomaji wa blog hii kwa kuzidi kutupatia ushirikiano wako.

Leo nmekuja na somo hili linalohusu FURAHA! hivyo nikukaribishe mpenzi msomaji kuwa nami katika somo hili na kabla ya yote nikupatie mwongozo mzima wa somo hili:
Baada ya somo hili utajifunza vitu vifuatavyo:-
1. Maana kamili ya Furaha
2.Mambo yanayokuzuia kutopata Furaha maishani mwako
3.Nini kifanyike ili kurejesha Furaha iliyo potea.

Maana kamili ya Furaha
Furaha kamili ni amani ya Moyo wako. Unajua wanadamu wengi tunashindwa kuelewa maana kamili ya neno Furaha, na matokeo yake tunaposhindwa kuipata Furaha hiyo tunaishia kutafuta furaha hiyo pasipo kuipata popote kumbe dawa ya tatito hiyo tunayo Mioyoni mwetu.

Kuna tofauti kubwa kati ya RAHA na FURAHA, raha ni Tukizo la mwili kutoka kwenye taabu na ifahamike kua raha hudumu kwa muda mchache angali Furaha hudumu Daima. Raha hutokana na Furaha.

Wacha nikupatie story kidogo juu ya Maisha yangu ya hapo awali. Kipindi nikiwa natoka utotoni na kuelekea huku ujanani nilipata tabu mno kuelewa ni FURAHA ya maisha yangu na kiukweli ilinichukua muda mwingi kupata jibu kamili juu ya swala hilo. Niliamini yakua nikiwa napenda raha za ulimwengu huu basi hapo nitakua nmemaliza kila kitu. Kwa kweli mwisho wa siku nilijipata katika hali mbaya sana nafsini mwangu hali ambayo nilikua napata msongo mkubwa wa mawazo, sikua na amani kwa kweli maana vile vyote nilivyo tamani kufanya ili kupata Furaha ya kweli nilikua nikivikosa kutokana na hali ya Umasikini niliokuwa nao. Niliumia na Ujana vilivyo na mwishowe nilivyo tafuta amani ya moyo wangu ndipo maisha yangu yakawa na FURAHA mpaka leo licha ya matatizo niliyo nayo bado nina Furaha moyoni mwangu.

Kwa maana hiyo basi tuanalie mambo ambayo yana kuzuia kupata Furaha maishani mwako
Yapo mambo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakuzuia kupata Furaha ya kweli maishani mwako na mbo hayo yanaweza kuwa yanasababishwa na WEWE mwenyewe ama MAZINGIRA yanayo kuzunguka na mabo hayo ni kama yafuatayo.

1.Kukosa amani moyoni mwako.
Jambo hili limekua likitesa wanadamu tulio wengi hasa vijana, na hii inatokana na mambo mengi mfano Umasikini/ufukara, mapenzi, unyonyaji na hata rushwa na kutokumjua MUNGU. Unapokua na amani kwenye moyo wako, ni wazi kwamba hata akili hufunguka nakufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi na hivyo maisha kuwa Murua kabisa na unapokosa amani hiyo ni wazi kua akili huvurugika nakuishia pabaya katika maendeleo yako kiuchumi na kiimani. Na mwishoni unakosa Furaha ya kweli maisha yako.

2.Kutokumjua Mungu.
Rafiki yangu kama mpaka leo Huamini kuwa Mungu yupo na kuamini kuwa yeye ndiye kila kitu katika kazi za mikono yako na maisha yako kwa ujumla basi umekwisha potea mazima. Unajua hakuna jambo zuri kama kumjua Mungu hapa duniani, Unaweza kuwa na Mali nyingi mno hapa dunia lakini bila Kumjua Mungu ni bure kabisa, utakosa mambo mengi ya muhimu mno kuliko mali ulizo nazo na Furaha ya kweli utaisikia kwa wegine huko barabarani.

3.Imani za kishirikina.
Asikufiche mtu hapa duniani hakuna watu wanaoteseka kama washirikina. Wamekua wakitabasamu katika nyuso zao wakati wakiwa kwenye makutano ya watu wengi lakini mioyoni mwao hawana amani kabisa. We mwenyewe unajiuliza iko wapi Furaha? Hivyo basi, unapokua unaamini katika mambo hayo hakika utakua umeipoteza FURAHA YA KWELI maishani mwako.

4.Wivu na husda usio na Tija.
Kuna watu huwa hawapendagi kuona mtu amepata kitu jamani katika ulimwengu huuu wa Mnyezi Mungu, wamekua wakiteseka mioyoni mwao kila kukicha kwamba “kwa nini Fulani kapata hichi?”. We jiulize mtu kama huyo atakua na Furaha kweli?

5.Dhiki na changamoto za masha.
Dhiki imekua miongoni mwa changamoto za kimaisha na wengi inawapata taabu kweli kweli hapa duniani. Maandiko ya Mnyezi Mungu yanasema “Ulimwengu mna dhiki lakini jipeni Moyo”. Hakuna haja yakufikiri kila siku juu ya taabu na mateso tuliyo nayo.

Hayo ni baadhi ya Mambo ambayo hutufanya wanadamu kuikosa furaha ya kweli na sasa tupate kutizama nini kifanyike ili kuirejesha Furaha iliyopotea;-

Ukiweza kutambua sababu kuu ni kwa nini unakosa furaha ya kweli basi itakua ni rahisi kutatua tatizo lako mazima. Mpende Mungu, Jiamini, Tafuta kuwa na amani ya kweli moyoni mwako, acha mambo yakishirikina, punguza wivu na Husda, Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe, Jifunze kusamehe, shukuru kwa kila jambo.
Kwa kufanya mambo hayo yote basi utakua umejitengenezea FURAHA YA KWELI maishani mwako.

Basi ndugu zanu nimefikia mwisho wa somo langu, na nikushukuru wewe ulipendezwa na somo hili na kuamua kulipitia mwambo mwisho “Ubarikiwe Tena na Tena” nikuache na neno la Mungu kutoka katiaka kitabu kile cha Wafilipi sura ya 4 mstari wa 4 hadi ule wa 5 ambao unasema “Furahini katika Bwana tena nasema Furahini, Upole wenu na ujulikane na watu wote, Bwana yu karibu”
Aksanteni na tukutane tena katika somo jingine hapa hapaMTOKAMBALI.

Continue Reading

LifeStyle

Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

Published

on

Je huu ndio Muda uliopanga kubadili Maisha yako leo? Yawezekana ni “Ndio” . Maisha ni mafupi mno hivyo yakupasa kufanya kile ulicho-dhamiria kufanya katika maisha yako. Hamna haja ya kuishi katika maisha ya taabu kila siku “wewe siyo mpumbavu”.

Vifuatavyo ni Viashiria sita ni kwa nini unapaswa kubadili Maisha yako Leo!
1.Acha Kuingoja Ijumaa.

Ijumaa huwaa ni nzuri kwa kweli maana wafanya kazi weengi walio ajiriwa hua wanapata ahueni na hata kupumua, Nimekua nikiliona hili katika maisha yangu ya kila siku na nimekua nikitafuta kazi ambayo itakua ikinipa Furaha ya kweli kila siku pasipo kuingojea Ijumaa. Kama umekua ukiishi katika maisha ya kuingojea Furaha ya ijumaa, kwa kweli yakubidi ubadili Life-style yako. Usininukuu vibaya katika hili maana nina sababu ni kwa nini nimesema hivyo..Je kama uliingojea ijumaa kupata furaha yako na ikawa ni kinyume na matarajio yako? We pata tuu picha…
Ni vigumu kuishi katika maisha ya Furaha kama ulivyo tarajia lakini inawezekana kuishi maisha ya furaha hata JUMATATU pasipo hata kuingojea ijumaaa. Ukiona hivyo badili maisha yako.

2.You live for your vacations.

Utaweza kujiuliza ni kwa nini nimesema “You Live for your Vacations” ni kwa sababu maisha ulio nayo kwa sasa ni ya Muda tuu na huto-yaishi milele. Kipindi cha mabadiliko ni Kizuri pia lakini ni kwa nini usitengeneze Maisha yajayo leo? mtu mmoja Maarufu huko ughaibuni alisema “Instead of wondering when your next vacation is, maybe you should set up a life you don’t need to escape from.” Kipindi cha mpito huaga muda mwingine kinaleta vichekesho na kuvutia but even better is building a life where you have the potential to do what lights you up many weeks of the year, not just your two allotted vacation weeks.

3.Pale unapo-koma na kufikiri, Unakua una shindwa kutazama maisha yako katika vipao mbele vyako.

Andika chini vitu vitatu unavyo-penda. Kisha andika vitu vitatu unavyo tizamia katika maisha yako, Je unaishi maisha yako katika Vipaombele hivyo ulivyo andika?
Consistently spending time doing what matters most to you is one of the keys to feeling fulfilled in your life. If you’re not focusing your life on what’s important to you, it’s time to make some changes.

4.Huna Idea yeyote inayo kuongoza, na wala huna nafasi katika maisha yako kuupata mwanga huo.

Kama ulishindwa kufahamu what is your passion katika maisha yako ya awali basi hutoweza kuifahamu katika maisha yako yajayo kama utaendelea na mtazamo na msimamo wa maisha yako ya sasa. Ili uweze kupata mwanga katika maisha yako, yakubidi uanze kutafuta nafasi kwa kuitafuta. Jipatie muda wa kujitafakari kua wewe ni nani, unakwenda wapi na nini kinacho kuvutia kufanya maishani mwako. Experiment with learning new things, spending time with inspiring people, and doing more of what excites you and less of the things that suck your energy.

5.Kila mara una kua na wivu.

Kama una muonea fulani wivu, kuna mambo matatu yakufanya kabla hujabadilika!

>Make a point to focus on your path instead of his or her journey. Sometimes this involves taking a break from social media.( na ndivyo ilivyo kwa tulio wengi)
>Jaribu kuwa inspired yule mtu unae-mwonea wivu na fanya vile vitu ambavyo ana fanya yeye na kufanikiwa.
>Decide what the other person has is not something you are willing to put in the effort to achieve, so you’ll cheer him or her on but choose to not be jealous.

6. You can’t remember the last time you stepped out of your comfort zone.

According to Neale Donald Walsch, “Life begins at the end of your comfort zone.” Your life can become even more amazing if you stretch beyond your comfort zone. If you’re not sure where to start, try the tips in this article about small ways to step out of your comfort zone.
Life is too short to spend your years not living to your full potential. If you decide you’re ready to change your life, I encourage you to start taking small action steps toward the life you want to live. Keep moving forward.

Continue Reading

LifeStyle

Tuzungumze yanayo tusibu na Kupata suluhisho.

Published

on

Mtu mmoja alipata kusema “Hasara roho, pesa makaratasi” na mimi nasema ni kweli kabisa.
Je una Amani ya moyo mwako? Je uhuru ulio nao unautumiaje? Je ukitazama ndani ya Fikra zako unaona Mafanikio yeyote? Je una imani juu ya ndoto zako? Je una mpango wowote juu ya Kuthubutu kuishi ndani ya Ndoto zako?…..

Leo nimepanda hapa MTOKAMBALI nikiuliza maswali hayo nikiwa na maana ya kwamba maswali hayo Yamekuwa chachu ya Mafanikio ya mtu yeyote hapa Ulimwenguni,,, Huwezi niambia ya kwamba utaweza kufanikiwa katika mambo yako angali Huna Amani Moyoni mwako wala kufanikiwa wakati umeshindwa kuutumia vyema Uhuru ulio nao ama Kufanikiwa angali hujawahi kuthubutu kufanya chochote juu ya ndoto zako…

Licha ya kuishi katika nchi yenye Uhuru lakini bado kuna vijana wenzangu hawana UHURU katika maisha yao. Wamekuwa wakiishi kama watumwa, wamekuwa wakipoteza hata matumaini yakuishi.. Hii yote inasababishwa na KIFUNGO CHA FIKRA.

Acha nikuambie rafiki yangu,

Hakuna jambo la muhimu na lenye nguvu katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote hapa ulimwenguni litakalo weza kuishinda nguvu ya Fikra.(Weka kumbu-kumbu juu ya mstari huu tafadhali).

Kile ambacho unafikiri kwa Muda mrefu ndicho kitakachotokea katika maisha yako. Fikra zako zina nguvu ya uumbaji.. na zaidi ya yote fikra zako ndizo zitakazo kupatia Uhuru wa kweli katika maisha yako na mafanikio tele utayaona. Ila pale unapokuwa mtumwa wa fikra zako, hakika utatamani kuiona Ardhi inapasuka kisha Uingie ndani yake na kupotea katika ulimwengu huuu wenye dhiki tele.

Leo nitakupatia njia ambazo zitakufanya uondokane na Utumwa wa fikra zako na kisha kupata uhuru wa Fikra zako na kufanikiwa kuishi katika baadhi ya ndoto zako. Tambua yakwamba njia hizi nitakazo kupatia, ni njia ambazo nilizitumia mimi kipindi nikiwa Utumwani na hadi Leo nathubutu kusema “NIKO HURU”.

Je uko teyari? lets move-on…

1. Jiamini unaweza
Katika maisha ya mwanadamu ni lazima kila mmoja ajiamini kwamba anaweza. Mwana harakati mmoja aliwahi kusema “Uoga wako ndio umasikini wako”. Njia ya kwanza ya kutoka katika kifungo cha fikra zako ni kuamini kwamba unaweza kuleta mabadiliko yeyote katika maisha yako licha ya hali uliyo nayo. Amini kwamba utaweza kuboresha maisha yako yakawa bora zaidi kama tuu utaongeza bidii katika hilo.

2.Ondoa Mawazo hasi katika maisha yako.
Moja ya maadui wakubwa wa Uhuru wa fikra za mwanadamu na Maisha kwa ujumla ni Fikra hasi(potofu). Fikra hasi huwa na hulka ya kukua kidogo kidogo katika maisha ya mwanadamu awaye yote yule na mwishoni huleta maafa makubwa mno na majuto yale ya mjukuu. Ili kuepuka hali hii unapaswa kuchukulia mambo kwa upande wa chanya zaidi kuliko upande wa hasi… hii itakusaidia sana katika kufikiri kwenda mbele ya mafanikio yako. Fikra hasi hupoteza matumaini siku zote hivyo yakubidi kuziepuka.

3.Epuka kuchukulia mambo kwa ujumla
Kuna vijana wengi huchukulia mambo kirahisi kama yalivyo na mwisho wa siku wanajikuta katika hali ngumu mno katika maisha yao. Embu jaribu kuchambua jambo moja moja kwa kina kisha ainisha ni lipi jema na ni lipi baya katika huo ujumla ulio nayo. Kumbuka unapokuwa ukichukulia mambo kwa ujumla, hutopata changamoto yeyote ile ambayo itakufanya Kufikiri kwa kina.

4.Thubutu kufanya.
Njia nyingine ya kutoka katika utumwa na kuupata uhuru wako ni kuthubutu kufanya kile ulicho nacho katika fikra zako juu ya maendeleo yako. Natambua kila mmoja wetu hapa ana ndoto fulani kubwa katika maisha yake na kama( huna ndoto yeyote katika maisha yako jua una hali mbaya kupindukia..). Je uliwahi kujaribu kuifika hata nusu ya ndoto zako? kama jibu ni ndio basi endelea na safari maana bado kidogo utafika mpendwa na kama bado hujathubutu basi kwa nzia sasa thubutu.

5.Acha kufanya mambo mengi kwa mawazo yako.
Mwanadamu hajakamilika siku zote na kila mwanadamu ana mapungufu yake , hivyo mapungufu yako wenda ikawa mwenzako anaweza kuyatua na wewe pia unaweza kuyatatua, hivyo utaona ni kwa namna gani utakapo kuwa ukishirikiana na wenzako katika kutimiza mambo yako utafanikiwa zaidi kuliko kufanya peke yako..
6.Jali muda wako.
Nafahamu kwamba kwa asilimia kubwa mno vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda wao katika mambo yasiyo na msingi na mwisho wa siku wanajikuta hawajafanya mambo yaliyo wapasa kufanya kwa wakati ule na kuanza kujuta ni kwa nini….. Embu kabla ya kupata majuto, jaribu kufanya mambo katika muda husika bila hata kupoteza sekunde moja katika Muda wako. “Majuto ni mjukuu”

Kwa kusema hayo, nammba nikwamie hapo na ni matumaini yangu kwamba nimekupatia kile unachokihitaji. Nimejfunza mengi mno katika maisha haya licha ya Umri wangu mdogo nilio nao. Likini kwa kuwa naamini katika ndoto zangu, sioni kama naumia bali nayaona maisha yangu katika Ulimwengu wa mafanikio.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 mtokambali.com