Tangazo

Sio siri hali ya uchumi sasa hivi kwa Watanzania wengi sio nzuri sana. Karibu kila unaekutana nae analia shida, wafanya biashara wanalalamika biashara haziendi vizuri kama zamani, shule zinalalamika wazazi hawalipi ada kwa wakati, wafanya kazi nao hawana uhakika wa kulipwa mwisho wa mwezi hawana. Yani ni shughuli!!

Hivyo basi, inabidi tupeane mbinu za kuweza kubana matumizi na kupambana na hali ya maisha.

Tunawezaje kubana matumizi kwenye matumizi ya kila siku na kwenye vitu ambavyo ni vya msingi na lazima??

 • Mahitaji ya nyumbani. Chakula, mboga, nyanya, vutunguu, carrot, mafuta, sabuni n.k ni vitu ambavyo hatuwezi kukwepa kununua kwa namna yoyote ile. Ila sasa badala ya kununua kidogo kidogo kila siku jitahidi uwe unanunua vitu kwa mkupuo. Yani badala ya kwenda dukani kila siku kununua majani ya chai, mchele, mafuta, sukari n.k…nunua kiasi cha kukuweka hata wiki mbili. Vitu kama sabuni za kuogea/ya unga ukinunua nyingi kwa wakati mmoja gharama inapungua kidogo.
 • Manunuzi ya vitu vya nyumbani(blender, jiko, vyombo nk), simu, nguo, viatu etc. etc. Kabla ya kununua jaribu kufanya utafiti kuhusiana na bei. Ila kuwa mwangalifu usije ukasahau kuzingatia ubora wa kile unachonunua ili usije ukaishia kupata hasara.
 • Hela za chenjichenji (sarafu). Kuna watu huwa hawatilii maanani sh. 100, 200 au hata 500 za sarafu.Tunza hela ndogo ndogo za sarafu vizuri badala ya kuzidharau na kuziweka hovyo. Tafuta chiombo maalum (kikombe/bakuli) ambayo utakuwa unazitupia humo na baada ya muda (wiki au hata mwezi) angalia na utashangazwa kiasi utakachokikuta humo.
 • Pika kiasi cha chakula ambacho una uhakika kitaisha iwapo hauna uwezo wa kukitunza kwenye friji ili kuepuka kutupa chakula mara kwa mara.
 • Kabla ya kupika chakua kipya angalia viporo ulivyonavyo kwenye friji. Usifuje chakula.
 • Kama sio lazima kula barabarani (hotelini/mgahawani/kwa mama ntilie n.k) nunua vitu na uandae chakula chako nyumbani. Hapa sio tu utasave hela, bali pia utakula chakula ambacho una uhakika umeandaa katika mazingira masafi.
 • Kama una friji inayofanya kazi vizuri epuka kuchemsha vitu vinavyotumia muda mrefu kuchemsha mara kwa mara mf. Maharage, nyama, makande, maji ya kunywa etc .etc. Badala yake chemsha kiasi kikubwa kwa wakati mmoja ili kuepuka kutumia sana mkaa, gesi ama umeme.
 • Usitoboe mfuko wako kumfurahisha sana mtu mwingine. Zamani Wahenga walisema ‘‘Karibu mgeni mwenyeji apone.’’ kwa hali ya sasa it’s more like ‘‘Karibu mgeni mwenyeji akome.’’. Usijitoe ufahamu ukamridhisha mgeni na mapochopocho mengi ya gharama wakati huna uhakika kesho utakula nini na familia yako. Andaa kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wako bila ya kujiumiza. Wageni wenyewe siku hizi wanajua soda ni anasa. Wali maharage , kipande cha chungwa akishushia na maji inatosha kabisa.
 • Badala ya kununua vitafunwa kila siku andaa mwenyewe nyumbani.
 • Zima vifaa vya umeme ambavyo hutumii kwa wakati huo. Ila hapa naomba niwajulishe kwamba KUZIMA NA KUWASHA FRIJI KUNAKULA UMEME ZAIDI BADALA YA KUSAVE. Hii ni kwasababu unapowasha friji inatumia umeme mwingi mpaka itakapopoa, ila baada ya kupoa inakuwa inaji-regulate yenyewe na kutumia umeme kidogo tu kumaintain ubaridi uliopo tayari.
 • Usiache taa zikiwaka ikiwa hazihitajiki na hakikisha ta azote zinazimwa alfajiri kabla hamjaenda kwenye mizunguko.
 • Jitahidi kununua vitu ambavyo ni original na kama ni electronics epuka vitu vya mtumba kwasababu vinatumia umeme mwingi kuliko vile ambavyo ni vipya .
 • Kama una eneo kubwa jaribu kulima mboga mboga kwaajili ya matumizi binafsi.
 • MWISHO kabisa, usiwe na matumizi yanayozidi kiasi cha hela uliyonayo. Jitahidi kuishi kwa budget na kusave hela kidogo kila mwezi.
AdvertisementMtokambali 728x90