Mother breastfeeding baby in living room
Tangazo

Nimeona niandike hii makala baada ya kushuhudia watoto kadha wa kadha wakidhoofika kwa kulazimishwa kula vitu ambavyo umri wao hauruhusu. Wako ambao miili yao inakuwa sawasawa au hata zaidi (overweight) ila bado hawaendelei vizuri kwenye mambo mengine mf. Kuwa wazito kutembea, kuongea, kufikiri n.k.

Kabla ya kwenda mbali, tukumbushane kwamba faida za kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita bila kumpa chochote na kuendelea kumyonyesha kidogo kidogo hata baada ya hapo ni nyingi na ni muhimu sana kwa afya ya mtoto.

Baadhi ni….

  1. Kumsaidia mtoto kuepuka magonjwa, kwasababu maziwa ya mama yatamsaidia kuimarisha immune system yake hivyo anakuwa haugui hovyo.
  2. Inampa mtoto nafasi kubwa kuepuka kuwa na mizio (allergies) kuliko anaepewa maziwa ya formula.
  3. Maziwa ya mama yanaongeza ufahamu wa mtoto maana yana kazi kubwa katika kuimarisha ubongo.
  4. Ukaribu kati ya mama na mtoto unaongezeka na hiyo ‘bond’ inamsaidia mtoto kukua vizuri kwa furaha.
  5. Speed ya ukuaji wa mtoto kiakili, kimwili, kisaikolojia na kihisia inakuwa juu. N.kPS.

KWA WAMAMA, KUNYONYESHA EXCLUSIVELY KWA MIEZI 6 NI NJIA NZURI SANA YA UZAZI WA MPANGO. Wengine hata period wanasahau kwa zaidi ya mwaka mmoja .

Tukirudi kwenye mada, wadada na wamama wengine huwa wanawalazimisha watoto kunywa uji,mtori,mziwa ya ng’ombe kwa kutopenda kunyonyesha,wakidai kwamba hawana maziwa ya kutosha na kuwa busy sana na kazi kwa wale walioajiriwa ama kujiajiri.

1.Wasiopenda kunyonyesha.Huo ni ubinafsi uliotukuka. Ikiwa hauko tayari kumtimizia mtoto mahitaji yake ya msingi kwanini ubebe mimba?! Kula ujana ukimaliza ndio uzae. Kwanza unataka manyonyo yakae juu juu maisha yako yote yamekuwa mawingu?!-;)

2.Wanaoamini hawana maziwa ya kutosha/mepesi kwasababu mtoto ananyonya non-stop bila kuonyesha dalili ya kushiba Nakushauri KULA VIZURI.

Nna rafiki yangu ana mtoto wa miezi minne tu na ana kilo 5,kadogoooo lakini anakunywa uji na maziwa huku maziwa ya mama yakiwa kama nyongeza tu kwa kisingizio cha akinyonya tu “hashibi”. Ila kwa kushinda na rafiki yangu niligundua tatizo lake, anaweza kunywa chai asubuhi na asile tena mpaka saa tisa mchana. Kwa maana hiyo mtoto ananyonya breakfast (Kipande cha mkate labda na mayai mawili) kwa masaa zaidi ya sita. Baada ya hapo anaweza akakaa tena mpaka saa mbili/tatu ndo ale tena. Hapo kitatoka kitu cha maana kweli?! Obviously not. Na sio yeye tu, kuna binti jirani yetu mtoto wangu na wake walipishana wiki tu kuzaliwa lakini kwenye ukuaji wamepishana kama vile wamezidiana mwaka mzima.

Binafsi siamini kwenye kula sana na kula vyakula vyenye mafuta mengi wakati wa uzazi. Na ile imani ya kwamba ugali,wali,maharage,cabbage,dagaa na vyakula vingine kama hivyo sio chakula cha mzazi sio kweli. Kila kitu kinalika na kila kimoja kina faida yake.

Ujanja ni kula portion ndogo ndogo kila baada ya masaa machache. Mf. Saa 1 CHAI na mayai mawili au na vipande viwili vya mkate, saa 3-4 kabakuli kadogo ka uji, saa 6 supu kidogo, saa 8 lunch (wali, ugali,ndizi,viazi, spaghetti, chapati za maji n.k), saa 11 matunda yoyote yale yanayopatikana kwa kipindi hicho au salad, saa 2 chakula cha usiku alafu basi. Katikati ya usiku ukisikia njaa kunywa chai/kikombe cha maziwa au juice labda na kipande cha mkate. Hapo hata ukimaliza uzazi hutoki umenenepa kama tembo na mtoto atakuwa mwenye afya tele.

..Waajiriwa/waliojiajiri. Mkamulie mtoto maziwa yahifadhiwe ili apewe kwa muda ule ambao haupo. Maziwa ya mama yanaweza kuhifadhiwa kwenye friji na mtoto akapashiwa kidogo muda wake wa kula ukifika. Pia, panga ratiba zako vizuri, kama uwezekano wa kurudi nyumbani mchana upo basi rudi unyonyeshe pia kuhakikisha mtoto wako yuko salama.

Kwa kuongezea tu, Maziwa ya ng’ombe ni mazuri kwa afya lakini sio kwa mtoto chini ya mwaka mmoja. Na sababu ni kwamba yana protein na madini zaidi ya ambavyo mwili wa mtoto mchanga unavyoweza kusaga. Pia minerals na vitamin zilizopo kwenye maziwa ya ng’ombe sio kiasi kile ambacho mtoto anahitaji. Ndo unakuta mtoto anakuwa na upungufu wa madini ya chuma ambayo inaweza kupelekea mtoto kupata anemia which is serious.

Kuweni wamama wazuri, kuleni vizuri (vyakula, matunda na mboga za kila aina) mnyonyeshe. Wababa wasaidieni wake,wazazi wenzeni kutimiza wajibu huu kwa kuwajali ili kuwanufaisha watoto wenu

AdvertisementMtokambali 728x90