Tangazo

Je una blog/web na unataka kutengeneza kipato katika Blog yako?

Najaribu kuepuka kuandika kuhusu pesa hapa Mtokambali, na badala yake nashauri kujikita zaidi katika njia za kukuza na kuendeleza Blog/web yako. Lakini imenibidi kuandika swala hili maana nimekua nikipokea maombi mengi ni kwa namna gani Blogger ataweza kuingiza kipato kupitia blog/web yake na hata kuweza kuendesha maisha yake ya kila siku.

Katika ulimwengu wa sasa mambo yanazidi kurahisishwa vilivyo kiasi kwamba kila mmoja wetu yupo njiani kuelekea katika digitali, Matumizi ya internet yanazidi kukua kwa kasi ya ajabu, Upatikanaji wa Taarifa nao unazidi kukua kila siku, hivyo basi uwanja wa Uandishi nao umezidi kukua na hata kujeuka Biashara. Leo hii mtu anaweza kukaa katika internet na Kutengeneza kipato sawa na yule mfanyakazi wa serekali(Mara nyingine kumshinda hata mfanyakazi wa serekali).

Story Yangu mtandaoni kwa Ufupi..

Safari yangu ya kutengeneza kipato mtandaoni ilianza kipindi nikiwa Chuoni( Kusema kweli sikuwa napenda Shule) hivyo nilikua natumia muda mwingi katika internet nikijifunza mambo mbali mbali yahusuyo teknolojia na maendeleo ya teknolojia katika nchi za Africa (Licha ya kwamba chuoni nilikua nasoma kozi nyingine, Am a medical Personnel). Nakumbuka mara ya kwanza kusikia kwamba Blog/web inaweza kukuingizia kipato na kuendesha Maisha yako ilikua ni kwenye Blog ijulikanayo kama ProBlogger.com na hapo ndipo safari yangu ya Kuanzisha Blog hii ilipoanzia.

Hakika sintoisahau ile siku yangu ya kwanza Kupokea kiasi cha Dola za kimarekani $130 ambazo zilitokana na Blog hii(Kiasi hichi ni kidogo mno machoni lakini kwakweli kilinifungua macho kwamba naweza tengeneza kipato cha kutosha kupitia Blog hiii). Yale yote niliyoyasoma Kule Problogger nilianza kuona kwamba ni ya Kweli na ndipo nilipoanza Kuyafanyia kazi vilivyo na leo nitakuonyesha mambo hayo ili na wewe uweze kufikia hapa nilipo.https://pbs.twimg.com/media/C8BHHreWkAAU2-x.jpg:large

Nisiongee sana maana mwanadamu kwa kusema tuu, kazi rahisi hiyo anaweza ongea hata mwaka mzima bila kusitisha.

Najua yapo maswali mengi utakayo jiuliza kabla ya kujiingiza katika kazi hii mfano, Ni wakati gani wakuanza kutangaza katika blog yako? Njia zipi nitatumia ili kufanikisha jambo hili? na nitahitaji namba kubwa kiasi gani ya watembeleaji kwa Siku? Yote haya nitayaeleza moja kwa moja hapo chini.

Awali ya yote ili uweze kufanikisha swala hili ni lazima uwe na Blog, tena sio zile blog ambazo ni Free Hosted(Blogger, Tumblur nk) hapa nazungumzia zile self Hosted Blogs/webs. Sisemi kwamba hizi free hosted site kama vile Blogger, Tumblur n.k haziwezi kufanikisha jambo hili Hapana ila ni Vyema ukawa na Blog yako peke yako.(Bofya hapa kuona jinsi utaweza kufanikisha kungua blog yako leo ).

Mambo yakuzingatia…..

Yawezekana ukawa Pengine umewahi sikia kuwa ukimiliki blogu ama tovuti unaweza kutengeneza pesa kirahisi?, ndio yawezekana kutengeneza pesa kirahisi kwa kutumia blogu, ila usiwe na shauku sana maana si rahisi tu.

Napokua naulizwa ni kwa namna gani blog inaweza kutengeneza pesa,

huwa napata picha kwamba, wanahisi blogu ni kama kitu ambacho ukiwa nacho tu chenyewe kinafanya kazi hiyo ya kutengeza faida, na wengine hudhani, pengine walipotoshwa kuwa anaweza anzisha blogu na kuanza kupata pesa bila yeye kama mmiliki wa blogu kuweka juhudi zozote zile!, Hapana, tena ukiwa bloga mpya ndio inakuwa ni ngumu zaidi kupata faida, tazama orodha hii ndogo ya mambo ambayo unapaswa kufanya:

 1. Andaa na anzisha blogu yako
 2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako
 3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako
 4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako
 5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

Unaona mambo yalivyo? Ni kazi ngumu mno, Hivyo swala la pesa huja la mwisho kabisa kama Mafanikio ya kazi ngumu uliyoanzisha.

1. Andaa na anzisha blogu yako

Ndio, ni lazima uwe na blogu, na uwe unaimiliki wewe mwenyewe, inaweza kuwa rahisi kujifunza jinsi ya kuanzisha blogu kwa kusoma bandiko hili. ambalo ndilo limefanya niulizwe mswali mengi sana kuhusu faida.

 2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako

Blogu haina maana yeyote kama haina maudhui, maudhui(Content) ndio kitu pekee kitakacho tofautisha blogu yako na blogu zingine mtandaoni, maudhui ndio yatakayo kupatia wasomaji na wafuatiliaji wakudumu na hata wapya kwenye blogu yako.

Kimsingi hili ndio jambo la muhimu sana kuzingatia, mfano mwandishi wa habari ana nafasi nzuri ya kuwa na mudhui kwa sababu anakua na habari mpya kila mara, namna atakavyoziandaa habari zake na kuzichapisha kwa wakati inampa fursa kutumia blogu kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi na wengi watapenda kuarifiwa punde tu unapochapisha habari mpya.

Chochote unachotaka kukizungumzia kwenye blogu yako chaweza kuwa ni kinalenga jamii fulani, au kundi fulani mfano watoto, vijana, wazee, wakulima, wanafunzi nakadhalika, jitahidi kiwe ni bora na chenye upekee. Maudhui mazuri na yenye muelekeo chanya yatawafanya wasomaji wako wajihisi kukufahamu na kukuamini sana hivyo kukuwekea mazingira bora zaidi ya kupata pesa baadae kupitia blogu yako.

 3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako

Blogu yako  ni mpya, hakuna mtu anaifahamu na unaamini una maudhui mazuri, sasa weka juhudi ya kuwapata wasomaji na wafuatiliaji, unatakiwa kuitangaza blogu yako. Muhimu hapa ni kujua ni watu gani (type of people) unaotaka wawe wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako. Kwa mfano umeandaa blogu ya mapishi!, ukishafahamu wasomaji wako ni watu wanaojihusisha na mambo ya mapishi basi fuatilia aina hii ya watu inaweza patikana wapi mtandaoni. Andaa orodha fupi yenye vitu kama:

 • Je!, wanafuatilia blogu zipi zingine zinazofanana au tofauti na maudhui ya blogu yako?
 • Wanashiriki kwenye majukwa gani mtandaoni? mfano (JamiiForums)
 • Kuna vipindi vya radio ama tv wanaweza kuwa wafuatilia pia?
 • Wanatumia mitandao ipi ya kijamii? orodhesha walau mitatu mikuu
 • Wanafuatlia watu gani kwenye hiyo mitandao ya kijamii?

4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako

Kwa kuzingatia hizo hatua hapo juu, utakuwa na blogu nzuri, yenye maudhui sahihi na bila shaka umeanza kupata  wasomaji, sasa unapaswa kujenga mahusioano ya karibu na wasomaji wako ili waendelee kubaki na pia kukuletea wasomaji wapya.

Jibu maswali yao wanayouliza kuhusu mada husika kwa wingi kadri unavyoweza, pia wasiliana na baadhi yao wanapohitaji mawasiliano nawe kwa njia ya barua pepe nakadhalika.

Kushirikiana na wasomaji ni njia nzuri kukuwezesh akuapata pesa kupitia blogu yako.

 5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

Sasa, umeshafanya yote yamsingi, lakini kupata pesa bado, na unahitaji kujaribu na kujuhudi njia mbalimbali kupata pesa. Bado safari ya kujifunza inaendelea, kuna njia nyingi sana za kupata pesa, ila hapa nitorodhesha chache ambazo mimi binafsi huwa nawashauri watu kuzitumia, tena ni njia ambazo bloga wengi huzitumia kupata pesa. Tuanze kujifunza njia hizi:

Tahadhari! Nijia Hizi nitakazozungumzia sio zile njia ambazo utafanikiwa kwa haraka. Hakuna njia ya mkato. Ni lazima ujitume na kuwekeza muda wako katika hili. Kutengeneza kipato katika blog sio kazi rahisi hata kidogo

Kupata pesa kupitia matangazo ya CPC au CPM

Hii ni njia kuu ambayo hutumiwa sana na wamiliki blogu kupata pesa kwa kuweka matangazo madogo madogo kwenye kurasa za blogu zao, ziko aina mbili;

 • CPC/PPC – Cost per Click (au Pay Per Click), matanagazo ambayo yanakuwepo kwenye kurasa au pembeni mwa kurasa ya blogu yako yatakuingizia pesa kila msomaji atakapo gonga (click) tangazo hilo.
 • CPM – Cost per 1000 Impressions, yani kadiri tangazo litakavyoonekana mara nyingi katika nyakati tofauti tofauti na wasomaji tofauti tofauti utapata pesa kutoka kwa anayetangaza.

Google Adsense ndio mtandao maarufu wa kuchapisha na kupachika matangazo ya namna hii kwa wamiliki wa tovuti na blogu mbali mbali duniani, na inawalipa wamiliki wa blogu hizi vizuri kadiri blogu husika invyofaya vizuri kuzingatia hatua tulizojifunza awali, matangazo yanayopachikwa huteuliwa kielectroniki kuendana na maudhui, pia lugha ya blogu yako.

Uza matangazo binafsi

Ukiwa na watembeali wengi wa blogu yako kwa siku, sio lazima kutumia mitandao ya matangazo kama Google Adsense, Badala yake Makampuni yanaweza kukufuata moja kwa moja kutaka uwatangazie biashara zao. Unaweza pia kuwasiliana na wahusika moja kwa moja, na kwa kuwa hakuna mtu wa kati, hii inakuwezesha kuweka viwango unvyotaka kutoza kwa kila tangazo na ukapata faida kubwa zaidi.

Tangazo linaweza kuwa mfumo wa picha, video, an au hata chapisho zima kuhusu bidhaa fulani, nakadhalika.

Uza bidhaa za kidigitali

Ikiwa hutaki kuhangaika kutangazia watu wengine, unaweza kutumia blogu yako kutangaza na kuuza bidhaa za kidigitali mfano vitabu, picha, muziki, video n.k.

Unachotakwa kuzingatia hapa, bidhaa utakazoziuza ziandane na maudhui ya blogu yako na pia mahitaji ya wasomaji wako, hutakiwi kuacha kuandika mambo muhimu kwenye blogu yako na kufanya biashara tu, kumbuka watu wanafungu ablogu yako kujifunza, hivyo biashara iwe ni jambo la ziada ili wasomaji wako wasichukizwe na waendelee kufurahia blogu yako.

Jiunge na Affiliating programs mbali mbali.

Labda utaniuliza Affiliating Programs ni nin?. Affiliating programs ni program maalumu watumiazo makampuni makubwa makubwa ya Uuzaji wa bidhaa mbali mbali mitandaoni ambapo wewe utatumika kama dalali wa bidhaa zile za makampuni hayo. Mfano wa makampuni hayo ni Amazon, Ebay, Commision Junction, Bluehost nk. Utapewa Link maalumu ambayo utatumia kuunganishia watu wanaopenda kufanya manunuzi katika kampuni hiyo kisha Mauzo yatakayopatikana basi wewe utapewa Asilimia kadhaa kwenye mauzo hayo.

Kwa hiyo basi kama blog yako itakua ni kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya Teknojojia basi utaweza kupata matangazo yanayoendana na Blog yako mfano, Simu, Computer na vyote viendanavyo na maudhui ya blog yako na hivyo watembeleaji wa blog yako wakitumia yale matangazo kuingia Labda Amazon na kununua Bidhaa yeyote mule basi wewe utapata gawio lako.

Andaa unachama wa kulipia kwenye blogu yako

Unaweza kuwa mbunifu zaidi na ukaandaa uanachama wa wasomaji wako ambao watajisajili na kulipia ili kupata huduma na maudhui ya kipekee zaidi, mfano mwandishi wa habari anaweza kuwalipisha wasomaji wake kupata habari mahususi zenye kuchambuliwa kwa kina na hata kushuhusia mahojiano aliyoandaa na baadhi ya watu mashuhuri.

Jenga jina na hadhi ya weledi wako

Blogu inaweza kuwa ni njia ya wewe binafsi kuonyesha uwezo na ufanisi ulionao katika fani mbalimbali na hivyo ukapata mialiko ya kufanya mafundisho, ama kupata kazi za kimikataba ambayo utakubaliana na wateja wako wakulipe.

 

Je una swali juu ya mada hii?

Je ni kuna njia yeyote niliyosahau kuitaja hapo Juu? ama kuna jambo limekutatiza hapo juu? Napenda sana kujua umekwama wapi ili niweze kusaidia, Tafadhali niandikie Maoni yako hapo chini na mimi nitakujibu

 

#Mtokambali, Special thanks to WebNerd Solution, Blog Tyrant, Wpbiginner, na Problogger kwa kunisaidia kufanikisha kuandika article hiii.

AdvertisementMtokambali 728x90

2 COMMENTS

 1. Ahsante sana Mkuu kwa article hii ya kuelimisha hakika kuna kitu ambacho mtu anakipata kutokana na kuisoma hii makala.
  Nadhani ni muda huu sasa kijana yeyote wa Kitanzania ambae anahitaji kuwekeza kwenye Mitandao ya Kijamii.
  Kuna suala lingine la Muhimu ambalo pengine umelisahau .
  “MUDA” Muda ni suala la kuzingatia sana katika uendeshaji wa Tovuti yako kama una nia nayo ya dhati. Kutenga muda wa kutosha na kuandika machapisho yenye kuwavutia watu ni njia nyingine pia ambayo itasaidia kuwa na kitu bora.
  Yangu ni hayo kwa ufupi.

  • Hi Jalilu Zaidi,
   Mkuu nashkuru kwa comment yako, na shukrani tena kwako kwa kunikumbusha “MUDA” hakika Muda ndio kila kitu, pengine hata Point hii ndio ningeanza nayo maana ndio yenye kubeba Post hii, Nitajitahidi mara baada ya Update ya post hii nizungumzie “MUDA”
   Hakika Unastahili kupigiwa makofi kadhaa….

Comments are closed.