Lipstick on collar
Tangazo

Tabia ya kutoka nje ya ndoa sio nzuri kama ambavyo mtu kuingilia ndoa ya mwenzie sio vizuri. Siku zote anaetoka nje ya ndoa yake ndio anaestahili lawama zaidi kwasababu ndio aliyetoa ahadi ya kuwa muaminifu ila pia hata wanaotoka nao japo sio wote kwasababu wengine huwa hawafahamu kwamba wanaotoka nao ni waume ama wake za watu.

Wapo watu ambao hawako interested na wala hawapendi kabisa kutembea na wake ama waume za watu ila wanadondoka kwenye mitego ya “niko single, mume/mke wangu amefariki, nimekupenda nataka tuoane” n.k bila kujua mwenzie alishaji-commit kwa mtu mwingine kitambo.

Hivyo nimeona tushee vitu ambavyo mtu anaweza kutumia kugundua kama Mr/Miss Perfect wake mpya ni Mr/Mrs Cheater. Japo sio guarantee ya moja kwa moja, inaweza ikasaidia kwa kiasi chake.

 1. Hapokei simu usiku, hajibu msg au anazima kabisa huku akiwa na visingizio lukuki kwanini anafanya hivyo – huu ni muda ambao anakuwa na familia yake.
 2. Mipango yenu sio ya muda mrefu -kwasababu lazima kila mnachopanga kiendane na ratiba ya nyumbani kwake hivyo anakuwa muangalifu kutogonganisha ahadi zenu na mipango ya nyumbani.
 3. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe. Na ikitokea akijitahidi kulala siku moja au mbili basi ujue kaiba siku mbili tatu kwa mke/mume wake kwa kudanganyia safari za kikazi, ila haiwezi tokea kila mara.
 4. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe baada ya kumshtukiza kwamba unataka ‘’a-spend the night’’ . Lazima apange mwenyewe mapema ili awe ameshaandaa mazingira kwa mke/mume wake.
 5. Mara nyingi akikupigia simu anakuwa yuko sehemu ambazo ni public(ofisini, barabarani, sokoni,dukani.nk) – huko ndiko anapopata uhuru wa kuongea na wewe kwa uwazi.
 6. Hakukaribishi kwake, anaweza akakwambia anaishi na mtu. . rafiki/ndugu anaemuheshimu sana hivyo hawezi kukukaribisha anapoishi.
 7. Anaweza akakutambulisha kwa marafiki zake (wanaomfichia siri) ila sio ndugu zake, especially wale watu wazima.
 8. Yeye ndie anaepanga/suggest wapi mkutane ili kuepuka kukutana na watu asiotaka wawaone pamoja.
 9. Ukitaka akusindikize sehemu/kwenye function anatafuta visingizio hata kama alishakwambia siku hiyo atakuwepo kwaajili yako na angependa mkutane kama kawaida.
 10. Siku za sikukuu anakua ‘unavailable’ kwako.
 11. Wakati mwingine simu yake ikiita anai-ignore, akipokea anaomba utulie au anasogea pambeni ndio aweze kuzungumza na aliyempigia.
 12. Marufuku kufika ofisini kwake sababu inawezekana ofisi ikawa inamtambua mke/mumewe.
 13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charge.
 14. Wanachagua sana sehemu za kula,kufanya mazungumzo na kupumzika. Mara nyingi huenda sehemu zenye watu wachache,nje ya mji au hupenda muonane sehemu zilizo na giza na watu wengi waasipopita au nyumbani kwako ,na husisitiza au hata kukung’ang’aniza upange/uishi mitaa fulani fulani.
 15. Wengine hupenda mkikutana in public places basi awe na rafiki yake muwe watatu au zaidi,ili hata kama kuna wa kumuwekea doubts apate wakati mgumu kujua uko na nani kati yake na rafiki yake .Halafu kuna wale wanaopenda sehemu zinazojaa sana kama club ili iwe ngumu kuwa noticed….
 16. Kwenye simu yake kaku-save kama ‘fundi fulani ‘ , initials zako (herufi za mwanzo za majina yako au jina lako halisi na sio honey, mpenzi wala darling.

Unapokuwa na wasiwasi kuhusu mtu ulieanza nae mahusiano kwamba pengine wewe ni kipoozeo tu, jaribu kumchunguza ili kupata ukweli na kujiridhisha iwapo  ni wako ama ni wa mtu mwingine

AdvertisementMtokambali 728x90