Tangazo

”Nitamuacha kwaajili yako” hutokea kwasababu kuna wakati  huwa inatokea watu wawili wakakutana mmoja au wote wawili wakiwa kwenye mahusiano na watu wengine.  Na wakati huo huo  kila mmoja wao akaishia kuvutiwa na mwenzie hata kufikia hatua ya “KUTAKA” kuwa pamoja.

Wanapofikia hatua hiyo yule mwenye mahusiano anaweza akatoa offer ya kuvunja mahusiano aliyokuwa nayo,  “Nitamuacha niliye nae/nataka nimuache niliye nae ili mimi na wewe tuwe katika mahusiano”. Kwa namna moja huu naweza kuuita ustaarabu kwasababu mhusika atakua mkweli kwa yule mwenzi wake kuwa mahusiano yao yamefikia tamati na ni muda kila mmoja akasonga mbele kivyake, which means hamna anaecheat.

Ila sasa. . . .Wewe binafsi unaonaje swala la mtu kumuacha mtu wake aliyekuwa nae “KWAAJILI YAKO”?!Sio kwakuwa hampendi tena, sio kwakuwa hamtaki tena ila kwa kiasi kikubwa ni kwasababu wewe umejitokeza.

Binafsi hiyo “KWAAJILI YAKO” hua inanipa ukakasi. Naona kama ni namna ya kuanzisha mahusiano ambayo ni very complicated tangu mwanzo, maana hata siku akikuchoka anaweza asichelewe kukutupia dongo la ” we ndo ulinisababisha nikamuacha mpenzi wangu. . .and for what? Huna maana!” . Hapo mmeshachokana, mihemko imeshapungua, penzi lenu limeshachuja au complication zimeshakuwa nyingi.

Nadhani njia ambayo ni sahihi na bora kudeal na mtu ambae yupo kwenye mahusiano anayodai hayataki tena bali anataka kuwa na wewe , huku nawe ukipenda kuwa nae ni kumtaka ajitoe kwenye situation aliyomo  kwanza (current relationship) bila ya kukuhusisha wewe kabisa. Kwamba avunje mahusiano yake ya awali bila ya kujua kama utampokea au la (bila yaw ewe kumuahidi chochote), avunje hayo mahusiano anayodai hayataki tena alafu ndio arudi kutaka kujua kama unamtaka na kama uko tayari kumpokea au la.

That way atakua ameonyesha kwamba kweli yale mahusiano aliyokuwamo kabla ya kukutana na wewe hakuwa anayataka wala kufurahia bali alikuwa anaendelea nayo tu labda kwa kukosa ujasiri ama msukumo wa kuyasitisha. Pia utakwepa lawama ya kuwa ‘ulihusika’ kuvunja mahusiano ya mwenzio kwa namna yoyote ile maana kumkubalia mtu amuache mpenzi wake aliyekuwa nae siku zote kwaajili yakow ewe ni kujibebesha lawama zisizo na maana na pia kujiingiza kwenye mahusiano bila kujua iwapo huyo mtu anakutumia kama kama kisingizio cha kukimbia matatizo yake au vipi.

AdvertisementMtokambali 728x90