Tangazo

Long Distance Relationship ni mahusiano ya kimapenzi kati ya watu wawili ambao wanaishi mbali mbali. Wasioweza kukutana bila ya mmoja wao kufunga safari. Katika mahusiano haya ni rahisi kuanguka na kupoteza ukaribu kati ya wapendanao ikiwa hawajajipanga kisawasawa kwasababu kila mmoja ana uhuru na muda mwingi anaoweza kufanya ‘mambo yake’ bila mwezie kujua.

Sasa basi..utajuaje kama wewe binafsi unaweza kumaintain LDR au la? Angalia utayari wako kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo….

  1. COMITMENT ISSUES – Kama wewe ni mtu ambae una “commitment issues” this is not for you. Kuweza kuvumilia kutokuwepo kwa mwenzio karibu kunahitaji kujitoa kwa hali ya juu na dhamira iliyonyooka.
  2. LUST(TAMAA) – Kama humpendi mwenzako (unamtamani tu) this is not for you. Ukiwa unatamani kitu ambacho  hukipati kwa wakati ni rahisi sana kukimbilia kile kilichopo karibu yako.
  3. TRUST ISSUES – Kama humwamini mwenzi wako, mwenzi wako hakuamini wewe au wewe mwenyewe hujiamini this is not for you. Bila kuaminiana kwenye mahusiano ya mbali mtajikuta mkiwa na mtafaruku kila siku. Umbali utasababisha maneno kati yenu, kuwekana hatiani na kuhisiana vibaya kuwepo sana. Kitu ambacho kitasababisha ugomvi wa mara kwa mara na kusababisha mrudi nyuma kimahusiano badala ya kusonga mbele.
  4. MALENGO – Kama huna malengo ya mbali na mwenzako this is not for you. Ikiwa huoni ukiwa na huyo mwenzako miaka miwili mitatu mbeleni mwache aende tu. Hamna haja ya kumfunga mwenzako na mahusiano ya mbali wakati hana umuhimu sana kwako.
  5. MANENO – Kama ni mwepesi wa kuchukua maneno ya watu bila kuyafanyia kazi this is not for you.Utaishia kupata presha bure na kugombana na mwenzio kila siku maana wachonganishi hawaishagi.
  6. COMMUNICATION – Kama ni mvivu wa mawasiliano this is not for you. Kitu pekee kinachoweza kukuweka karibu na mwenzako wakati mko mbali mbali ni mawasiliano ya mara kwa mara. E-mail, Simu, Texting, Skype,watssap etc. etc. ndivyo vinavyoweza kupunguza umbali uliopo kati yenu walau kidogo. Hivyo kama wewe mzuri katika swala zima la mawasiliano jua ya kwamba muda utafika wa mahusiano yako kuvunjika kutokana na lack of communication.

Kwa wale ambao wanafikiria kujiingiza kwenye mahusiano ya mbali jua inawezekana ikiwa tu una nia ya kuyawezesha mahusiano yenu. Kama huna nia thabiti bora uende uendako au umuache mwezio aende alafu siku ukirudi/akirudi na kujikuta bado mpo mpo ndio mjaribu kuliko kujiingiza kwenye mahusiano ambayo yataisha vibaya.

Kwa wale ambae ndio wanahangaika nayo sasa hivi muhimu ni uwe mwaminifu,uwe na imani na mwenzako,ujitume kwenye swala zima la mawasiliano na msisahau kuongelea na kukumbushana “them good times”. Hii itasaidia kukumbushana umuhimu wenu kwa kila mmoja na kwamba japo mnakosana kwa muda, mtakapoweza kuwa karibu tena maisha yenu yatapendeza na mtafurahiana. Mjali mwenzako kwa maneno mazuri, epuka kuanzisha maugomvi yasiyo na pembe wala mkia na usimpe sababu ya kufurahia umbali wako hata chembe.

Mwisho. . . kama ni kucheat hata unaelala nae kitanda kimoja kila siku, unaekunywa nae chai kila asubuhi na kupitiana kazini kila jioni anaweza kucheat kwasababu vishawishi viko kila mahali. Hivyo usaliti hauletwi na umbali bali tabia binafsi ya mtu. Hivyo kama wewe ni mvumilivu go ahead and give it a try huku ukiomba na kuamini kwamba mwenzako nae yuko hivyo hivyo pia iwapo hajakupa sababu ya kufikiria vingenevyo.

 

AdvertisementMtokambali 728x90