Tangazo

Najua Mapenzi siku hizi ni Pesa ..sura zinakwenda Red Carpet,….lakini Leo turudi kwenye Ukweli kidogo,….Hivi Ushawahi kuwa na Best Friend wa Jinsia Tofauti na wewe halafu wote mna hisia za Mapenzi baina yenu? ..Sharing Same feelings of Love towards each other….halafu mnaogopana?

Yap, kwa Mazingira ya Afrika Mwanamke aliyependa kweli huogopa kusema kwa sababu anahisi thamani yake itashuka, atahisiwa tofauti n.k..na atatumia zaidi matendo kuelezea hisia zake…na kama kunakuwa hakuna postive response basi ataendelea kuumia kimya kimya.

Mwanaume yeye kuna mawili anaweza asiwe domo zege au akawa Domo zege, na mara nyingi Wanaume ambao ni Much confident hapa Confidence hiyo mara nyingi hupeperuka..anaweza kuwa alishatongoza wanawake 3,210 lakini hapa akangiwa na hofu na woga, na hii ni kwa sababu kutongoza mtu unayemtamani ni rahisi kwa sababu anakuwa tayari kupokea majibu yoyote iwe YES au NO na hana cha kupoteza, si katamani?….lakini kutongoza ampendaye anakuwa hana utayari wa kupokea majibu mabaya.. Negative Rosponse (kukataliwa) na ampendaye (hii inauma)..so atavuta vuta muda na timing.

Unajua nini kinakwenda kutokea?.👇

Mwanamke huyu atakaa na hisia hizo kwa muda huku akionyesha tu vitendo kwa bwana huyu, lakini akiona kimya basi hukata tamaa kabisa na anakuwa mentally frustuated,..sasa ktk wakati huu wa kuchanganyikiwa ndio mwanamke anapoweza kudondokea hata mikononi mwa zombi….yaani ndipo anapotokea Jamaa mwingine kutoka huko atokako, tena amemtamani tu na hana cha kupoteza…huyu bwana anajiropokea maneno yake marefu kuliko zaburi ya 118 ..anakubaliwa kwa hasira tu….mwanamke huyooo anatokomea zake

Jamaa sasa ndio anaanza kuona ile Friendship inakufa taatiibu, mrembo amekuwa adimu,..jamaa anajiona Looser na anataka sasa aropoke kuhusu Feelings zake, na ndipo anapokuta anachukiwa na mwanamke huyo kwa kiwango cha Lami…yaani ile Chuki ya mafuta ya taa kwa inzi.(there is a thin wall between Love and hate)

Mwisho wa siku hawa wote wawili ni Loosers…Mwanamke amekwenda pasipo malengo na huyu jamaa nae atatafuta kichaka ajipoze, ..huko waliko wawili hawa ni Mashaka na Majaliwa….END.

Pio Pius..0719 122 155.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


 

AdvertisementMtokambali 728x90