Tangazo

Kwanza kabisa mahusiano mabaya ni yale mahusiano ambayo maumivu na huzuni vinazidi furaha na ile hali ya kuridhika na mwenzi wako. Ndani yake kuna manyanyaso ya kila aina (mental, physical,emotional,financial abuse n.k). Kusema ukweli kuna watu ambao wako kwenye mahusiano mabaya na wanajikuta maisha yao nayo yanazidi kuwa mabaya kwa kushindwa kufanya maamuzi mazuri na kwa wakati sahihi.

Nimejikuta tu nafikiria kwamba kama watu wangekuwa wanajipanga kabla ya kufanya maamuzi linapokuja swala la kuanza ama  kujitoa kwenye ‘’bad relationships’’ wengi wao wangeepuka kukimbia matatizo kisha kukimbilia matatizo mengine makubwa zaidi kutokana na kurudia makosa yale yale.

Kwanza unajuaje uko kwenye mahusiano mabaya??

*Maisha yenu pamoja yanapotawaliwa na maudhi, ugomvi wa mara kwa mara na chuki.

*Unapotamani hata asikuongeleshe kwasababu ukimya wake ni bora kuliko kumsikiliza akiongea chochote kile hata kama sio kitu cha kusababisha ugomvi.

*Kuwa karibu na mwenzio kimwili kunakukosesha raha kama sio kukuchefua.

*Mawasiliano yanapokuwa hasi, yeyote anaweza kwenda popote na akakaa kwa muda wowote bila kujali wala mwenzie kujua alipo ama anachokifanya.

*Unapokosa kujiamini mbele ya mwenzi wako na kujikuta unalazimika kufanya vyovyote vile anavyotaka hata kama hujisikii ama hupendi.

*Unapoona kwamba wewe pekee ndie unaehangaika kutafuta maelewano pale inapotokea matatizo kati yenu.

*Mwenzi wako anapoonyesha waziwazi kwamba hauna umuhimu wowote kwake.

*Pale unapokosa raha unapomuona au hata kumsikia tu mwenzako. Ukiona jina lake pale simu inapoita unajikuta unatamani usipokee, unajilazimisha ili tu ujue anataka nini ila wakati mwingine una-ignore kabisa simu yake.

*Una-prefer na ku-enjoy zaidi kuwepo nyumbani pale anapokuwa hayupo.

*Kama mna mtoto /watoto unaona kama hauwi vizuri nao pale anapokuwepo karibu. Wakati mwingine unahisi kama unajilazimisha kufurahi nao awapo karibu.

*Pale unapomuangalia/mfikiria mwenzako na kujiuliza ‘‘WHAT THE HELL WAS I THINKING BEING WITH HIM/HER?’’ ‘‘ Nilitokana nae wapi huyu??’’ ‘‘Niliona kitu gani kwake?’’

*Unapotumia muda wako mwingi kujutia kuwa na yeye na  kuwaza ni jinsi gani maisha yako yangekuwa na amani ama bora zaidi iwapo usingekuwa na mahusiano nae ama iwapo ungeweza kuachana nae.

*Unapotamani kumuumiza iwe kwa maneno au matendo (mf. Cheating,kumpiga, au kumkomoa kwa namna yoyote ile).

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaashiria kuwa upo kwenye mahusiano mabaya.

 

Now straight to the point, dawa ya mahusiano mabaya ni kujitoa na kujiweka mbali nayo. Kumbuka kwamba mara nyingi kadiri muda unavyoenda ndivyo mambo yanavyozidi kuwa mabaya.

Hapo ni rahisi kumshauri mtu aachane na aliyenaye bila kufikiria kitakachotokea baada ya hapo, na mara nyingi tatizo kubwa huwa ni fedha na namna ya kuishi baada ya hapo. Binafsi simshauri mtu aondoke /aachane na mtu tu bila kuwa amejipanga ataishi vipi baada ya hapo haswa watoto wanapokuwa involved. Sikuzote ni rahisi kwa mtu kuweza kuomba msaada kwa mwingine pale anapokuwa mwenyewe kuliko anapokuwa na mtoto/watoto. Ndio watoto ni baraka, lakini kubeba watoto na kwenda kukaa nao kwa ndugu/rafiki bila kuwa na mipango ni mzigo. Hata wewe mwenyewe hutojisikia vizuri.

Wamama kwa wababa, wadada na wakaka, kama umeshajiandaa kiakili na unajiweza kwamba baada ya kuachana na Yule uliyenae utaweza kujihudumia vyema pamoja na watoto ulio nao, kama una uhakika utaweza kujilinda/kujiweka mbali na mwenzi wako kama ni mkorofi go ahead and walk out. Ila kama unaona kabisa hauko tayari kifedha au kiakili ndugu yangu stay put na ujipange. Mimi nasema ‘‘Making a hasty decision is just as bad as staying in a bad relationship’’. Yani unajikuta unakimbia tatizo moja na kukimbilia jingine. Ni bora ukakawia kuondoka ila ukafika salama sehemu salama, kuliko kuharakisha ukajikuta matatizoni. Haswa kwa wadada ambao ni tegemezi, hamna haja ya kuwatoa watoto au hata wewe mwenyewe sehemu ambayo unaweza kula ukaenda kutangatanga nao bila kujua hatma yenu itakuwaje. Hapa simaanishi kwamba  ukomae tu hivyo hivyo mpaka mwisho, HAPANA. Ficha ficha hata vi-sh 500 mpaka upate mtaji hata wa biashara ndogo, na kodi ya miezi sita, na kama uwezo upo DO BIG ili utakapoondoka usigeuke omba omba hata uliyemuacha akuone kichekesho.

USIKURUPUKE, fanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.

AdvertisementMtokambali 728x90