Mambo ambayo hutakiwi kufanya pindi ufikapo miaka 24
Tangazo

Hongera nikupongeze kwa kufika miaka 24 bado uungali kijana lakini upo njiani kuelekea uzeeni. Sasa basi ni kwa namna gani utabadili maisha yako na kuwa Vizuri zaidi? Fuatilia kanuni zifuatazo zenye mwongozo wa mambo ambayo hupaswi kufanya tena unapofikia umri wa maika 24.

#1.Punguza au acha kuvaa nguo za Bei rahisi.

Kama mtoto na kijana mdogo basi ni kawaida sana kuvaa nguo za Bei rahisi, ila kwa kuwa umekwisha kuwa mtu mzima na ni wakati umehitimu chuo na unajipanga kufanya kazi ya maana, ni wakati wa wewe kuvaa nguo za hali ya juu na kuchukulia mitoko yako katika viwango vya juu ( it’s time to start taking style more seriously). Nunua nguo chache za hali ya juu kuliko kununua mafurushi ya nguo za mtumba ambayo haifai hata kuvaa na kuingia ofisini.

#2.Acha kutoka kimapenzi na mtu ambaye humpendi kwa dhati.

Nafahamu ni ngumu kumpata mpenzi mwenye mapenzi ya dhati ambaye atakuthamini wewe na mali zako, lakini mpaka umefikia miaka zaidi ya 20 utakua teyari ushapata picha kwamba ni mwanamke ama mwanaume wa aina gani unaye mhitaji katika maisha yako. Achana na mambo ya majaribio kila kukicha, yakwamba unamjaribu huyu na yule. Ni wakati sasa wakufanya mambo katika uhalisia na sio nadharia.

#3.Puuzia yale yote wayasemayo watu juu yako na maisha yako

Ni kawaida ya wanadamu kuhofia maneno ya wanadamu wengine, ila kiuhalisia 

Usiyachukulie maneno ya watu wayasemeyo na kutaka kuishi katika maisha wayatakayo wao. Jiamini peke yako na simamia ndoto yako.

#4.Usiwalaumu wazazi wako.

Tambua yakwamba wazazi wako nao ni wanadamu kama wewe ulivyo na hakuna mwanadamu aliye kamilika. Yawezekana wao wa kawa chanzo cha matatizo uliyo nayo kwa wakati huu lakini hupaswi tena kuwalaumu kwakua tuu jambo limekwisha tokea na hutoweza kuwafanya chachote kile. Unapojaribu kuwalaumu na kujitenga nao ni njia ya wewe kusaka laana na mikosi kutoka kwao. Achana na mambo hayo kisha jenga njia za kutoka katika janga hilo na zaidi ya yote jenga uhusiano mzuri na imara kati yako na wazazi wako. Hii itakusaidia sana maishani mwako.

#5.Acha kushikilia ndoto zako za zamani na matumaini ya zamani.

Yawezekana ukawa bado na matumaini na ndoto zako za awali ambazo hazitimii kila kukicha, na umri nao unasonga kweli kweli ila sii vibaya ukaziacha ndoto hizo na Kukumbatia zile ndoto ambazo ni za sasa maana hata ule uwezo wako wa kudadavua mambo utakua uko juu zaidi ya hapo awali hivyo utasonga mbele na sio tena kukaa na kufikiria ndoto za awali zisizotimia.

#6.Acha kulalamikia ugumu wa Maisha na ukosefu wa pesa.

Tambua ya kwamba maisha ni jinsi unavyoishi siku zote, ugumu wa maisha na ukosefu wa fedha ni wewe pekee utakaye weza kuvitatua. Ni wakati sasa kupanga mambo na kufanya kazi kwa hali na mali kwa vyovyote vile ilimradi viwe ni halali. Shida na Ukosefu wa Fedha vitaisha pale tuu utakapo amua kutoka gizani(Uvivu na Ujinga) na Kuja nuruni(Kufanya kazi). Umri wa miaka 24 ni kiwango cha juu sana katika upambanaji.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika
AdvertisementMtokambali 728x90