Tangazo

Mumewe alipack vitu vyake kimya kimya na kufungua mlango kisha akaondoka na hakurudi tena. Angel alianguka magotini na kulia kwa uchungu huku akitetemeka. Alikua na aliachiwa watoto wawili Mkubwa wa miaka mmitano na mdogo wa miaka mitatu.

Atafanya nini, hana Kazi, hana ujuzi wowote ule wala hafahamu biashara yeyote ile ya kufanya. Ni miezi sita tangu mumewe amkimbie na hajapokea simu wala ujumbe wowote kutoka kwa mumewe, nyumba waliokuwa wakiishi walifukuzwa kwa kukosa kodi, na fedha alizokua nazo kiasi cha dollar 100 zilikaribia kuisha.

Alitamani kujiua lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa alijua teyari ana watoto wawili ambao wangeteseka zaidi kama angejiua.

Lakini siku moja machozi yalikauka, maumivu yalijeuka ghadhabu na njaa ya kutaka kufanikiwa katika maisha ili kuiokoa familia yake. Ndio alijitambua, akasimama kama mama na kupambana.

Aliishi kwa rafiki zake kwa miaka saba(7) huku akitumia muda wake wote akifanya kazi za ndani kwa watu na huku akichukua masomo yake ya Shada kwa kupitia mtandao. Aliteseka na kurudia kulia kila siku lakini hakukata tamaa na kuzidi kulelea watoto wake.

Alifanikiwa kumaliza chuo na kuhitimu shahada yake, aliamua kufungua kampuni yake ya usafirishaji wa bidhaa kwa pesa kidogo alichokihifadhi kutokana na kazi za usafi alizokua akifanya kwa watu. Na sasa kampuni yake imekua kubwa sana na inafanya vizuri. Alinunua Nyumba na Gari mpya, na sasa wanawe wote wako college na anaweza kuwalipia ada na mahitaji mengine. Vilio na machungu vyote vimetoweka, na furaha Imemrudia tena.

“Kila mmoja wetu anataka kujenga juu ya Mlima, lakini Furaha na makuzi hutokea katikati mwa safari ya kupanda mlima huo” -Andy Rooney

Wengi wetu wanaamini kimakosa kwamba Furaha ni kukusekana kwa kuvunjika mipyo na mateso ya ulimwengu huu. Tunatamani maisha mazuri na mepesi pasipo kutambua ya kwamba changamoto hazikwepeki hata kidogo.

Kwa sisi kufanikiwa kuyashinda matatizo hayo ni lazima kukubali mambo haya yafuatayo kuchukua nafasi katika maisha yetu ya kila siku. Ni mabadiliko makubwa mno:-

#1.Mabadiliko ni sehemu ya Makuzi(Kukua).

Angel aliamua kufanya mabadiliko(Ingawa mabadiliko yalimlazimisha) ili kufanikisha kile alichokidhamiria katika maisha yake. Machungu aliyoyapata mara baada ya kuondokewa na mumewe kulibadilisha mfumo wake wa maisha kwa ujumla, ilimlazimu kukubaliana na matatizo yale na kuyachukulia kama sehemu ya maisha yake. Usiogope kubadilika na kamwe usiyakimbie majaribu yako maana majaribu ni mwanya wa kukua kwako.

#2.Msukumo na mahangaiko yako ni sehemu ya Maendeleo na kukua kwako.

Tuchukulie mfano mdogo tuu wa kuujenga mwili, njia kuu itumikayo kuujenga mwili ni kuinua Vyuma vizito. Ule uzito unaobeba hupelekea misuli yako kuongezeka na kuwa na nguvu zaidi. Kinyume chake ni kweli. Kukwepa mahangaiko ya maisha kutekupelekea wewe Kudumaa kimaendeleo maana utakua unakosa mengi katika maisha.

#3.Unajifunza mengi katika kushindwa kuliko katika kufanikiwa.

Kushindwa ni njia nzuri sana ya kujifunza na kuku katika maisha yetu ya kila siku. Unapokua unashindwa, unatafuta njia na kufamu ni kwa nini ulishindwa. Kushindwa kunatufanya tufikiri kwa kina zaidi.

Maisha siku zote yanaendana na changamoto. Maumivu hutufanya kubadilika. Mizigo ya mateso tuliyonayo hutuongezea kufikiri ni kwa namna gani tutaweza kuipunguza na hata kuitua moja kwa moja.

AdvertisementMtokambali 728x90