matarajio-expectations-kwenye-mahusiano
Tangazo

Unrealistic expectations are planned resentments.

Kila mtu anapoingia kwenye mahusiano/ndoa anakua na matarajio yake. “Tutapendana milele!!” !Hawezi kuniumiza.” “Atanitatulia shida zangu zote.’’ ‘’Hatuwezi kugombana!!’’ etc. etc.

Wapo watu ambao wana matarajio ambayo napenda kuyaita “reasonable/realistic”  ambayo ni rahisi kutekelezeka na yenye uhalisia na wengine wana matarajio ambayo ni “unrealistic”. Sadly, mara nyingi baadhi ya hizi ‘unrealistic expectation’ ndo haswaa hufanya baadhi ya mahusiano yashindwe kwenda mbele.

Mf. wa Realistic expectations katika mahusiano:

. . . Nampenda nae ananipenda ila migongano ya hapa na pale haitokosekana – TUTAITATUA PAMOJA.

. . . Ananifurahisha nami namfurahisha ila kuna wakati tutakasirishana – TUTASHIRIKIANA KUITAFUTA HIYO FURAHA TENA.

. . .Napenda/nafurahia uwepo wake nae wangu ila kuna wakati tutachokana – NI JUKUMU LETU KUTAFUTA NAMNA YA KURUDI KWENYE HALI HIYO.

. . .

. . .Tuna afya ila magonjwa/ajali zaweza tokea – TUTASIMAMA PAMOJA.

. . . Tutabadilika kadiri muda unavyoenda (muonekano, fikra, mazoea n.k) – TUTAJITAHIDI TUENDANE NA MABADILIKO YA KILA MMOJA WETU n.k. . . . . .

Mf. wa Unrealistic expectation katika mahusiano:

. . . Ndoa/mahusiano ndio mwisho wa matatizo yangu ya kifedha.

. . . Ana gari, sitokaa nipande daladala tena.

. . . Kila siku tutakua tunacheka na kufurahi tu.

. . . Aliyonivutia nayo yote yataendelea kuwepo sikuzote.

. . . Yeye ndie mtoaji mimi ni mpokeaji tu.

. . .Hatuwezi kuchokana ama kukasirishana.

. . . Hamna chochote kinachoweza kutokea na kubadili kila kitu mf. matatizo ya kifamilia, magonjwa n.k

Matarajio unayokua nayo wakati unaingia kwenye mahusiano yana nafasi kubwa sana katika kustahimilisha mahusiano yako, pia hisia/mapenzi uliyonayo juu ya mwenzi wako.

Unapokua unaelewa kuwa maisha ndani ya mahusiano yako hayatokua mteremko kila siku, ukaelewa kwamba kutakua na milima, mabonde na viunzi basi unakua umejiandaa kifikra namna ya kukabiliana na vikwazo vyovyote vinavyoweza kutokea. Badala ya kulaumu na kulalamika unasaidiana na mwenzi wako kukabiliana na matatizo yenu. Kinyume cha hapo, utajikuta unamchukia mwenzi wako kwa kushindwa kutimiza/fikia matarajio yako ambayo hayakua yamekaa kihalisia toka mwanzo. Hii inatokana na wewe kuishi katika ulimwengu wa kufikirika huku ukijivua uwajibikaji linapokuja swala zima la kufikia matarajio yako na kumvisha mwenzi wako kana kwamba yeye anaweza kucontrol kila kinachotokea. Kwa style hiyo utajikuta unaingia na kutoka katika mahusiano kwa sababu zile zile kila mara.

Kuwa na matarajio yaliyokaa kiuhalisia ili kupunguza disappointments kwenye mahusiano yako.

AdvertisementMtokambali 728x90