Tangazo

Baadhi ya watu husumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia yaliyosababishwa na malezi hasi.

Katika hali ya kawaida watoto hujifunza kutokana na matendo ila hujengwa kiakili na kihisia kutokana na maneno . Katika maisha ya mtoto mzazi ndio mwenyewe nafasi kubwa ya kuweza kumfanya mtoto wake awe mtoto mzuri, mwenye kujiamini, mkorofi, dhaifu na baadae kuwa mtu mzima wa aina hiyo hiyo. Hii yote ni kutokana na kwamba watoto huwaamini wazazi/walezi wao kabla ya mtu mwingine yeyote yule. Hivyo mzazi akiitumia nafasi yake vibaya atamuathiri mtoto wake kwa namna ambayo ni hasi.

Hizi ni baadhi ya matatizo ya ukubwani yanayosababishwa na malezi…

Kuwa na hofu iliyokithiri katika maisha(Anxiety), msongo wa mawazo (Depression) , kukosa uwezo wa kujitegemea (Lack of independence). Hii hutokana na mzazi kuangalia na kuchunguza kila kitu mtoto anachokifanya ili kuwa incontrol (HELICOPTER PARENTS) na kumkosesha mtoto nafasi ya kufanya maamuzi yake mwenyewe. Kijana ambae hawezi kufanya maamuzi muhimu na binafsi  hata pale yanapohusu mahusiano yake na mpenzi wake bila kushirikisha (kuomba ruhusa ya) wazazi wake alilelewa katika malezi ya aina hii.

Addiction na michezo hatarishi, msongo wa mawazo (Depression) na kujiona mwenye hatia kila wakati. Mzazi anapomuambia /sema mbele ya mtoto mara kwa mara ni kiasi gani cha matatizo uwepo wa mtoto huyo umemsababishia maishani mwake, ‘‘Tumejinyima sana kwaajili yako’’ kutamfanya mtoto atakuwa akitafuta namna za kujidhuru bila yeye kujua, kujiona hastahili huduma ambazo ni jukumu la mzazi wake kumpatia n.k. Mf. Pombe, madawa ya kulevya, michezo inayoweza kuhatarisha maisha yake n.k

Kushindwa kupumzika vizuri (Inability to rest & relax compeletly)Maneno kama ‘‘Kuwa serious!’’ ‘‘Acha utoto/kujidai mtoto’’ ‘‘Acha kukaa kaa tu’’ wakati wote itamfanya mtoto atakapokuwa kijana awe mtu asiyeweza kurelax, asiweza kuelewa watoto na anaechukia watu ambao anaona bado hawajakomaa kwakuwa hawako serious katika kila jambo.

Kutokujiamini (Low self-esteem) na tamaa ya kuwa kama mtu mwingine. Wazazi ambao huwalinganisha watoto wao na watoto ambao wamemzidi Zaidi kiuwezo hufanya watoto wo wakiwa na inferiority complex. Watafanya jitihada za kuwa bora huku wakijichukia kwa kutokuwa na uwezo mkubwa/mzuri kama wanaolinganishwa nao.

Hofu ya kuamini watu wengine. Maelezo ya ‘‘Usimuamini mtu yeyote’’ ‘‘Hamna mtu anaeaminika dunia hii’’ humfanya mtoto akuwe akiwa na hofu ya kumuamini yeyote yule. Iwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, kirafiki, kifamilia na hata kikazi.

Kutafuta mwenza ambae ni kama mzazi. ‘‘Wewe ni mdogo sana hiki au kile’’ mara kwa mara kutamfanya mtoto awe mtu mzima huku akibaki kuwa mdogo (young) siku zote huku akiwa tegemezi na kuhitaji mwenza ambae ata-act kama vile mzazi wake.

Kukandamiza vipaji binafsi, kukosa initiative, kujifurahisha kwa vitu hatarishi.                     

Kama mzazi atatumia kauli kama ‘ ‘Usijidai ama usijione unajua sana’’ ‘ ‘Hizo ni ndoto tu’’ ‘ ‘Unachofanya hakitokufikisha popote’’ n.k mara kwa mara mtoto atakuwa mtu asiyekuwa na maoni, ari ya kuanzisha kitu (initiative) wala sifa za uongozi (leadership qualities).Matokeo yake atajikuta akijaribu kujisahaulisha tamaa yake ya kufanya mambo (ambition) kwenye ulevi na hata madawa ya kulevya.

Kukosa ukaribu (Closeness) na kukandamiza hisia binafsi(Suppression of emotions). Kuwa mzito kuonyesha hisia (lack of emtions) na kujali kwa mzazi humuathiri sana mtoto bila ya yeye kutambua. Mtoto anapoambiwa aache kulia ama kulalamika mara kwa mara hata pale anapokuwa na haki ya kulia ama kulalamika kunamfamnya akandamizie hisia zake ndani kwa ndani ambapo huweza kumsababishia Psychosomatic Disorder.

Utegemezi uliokithiri (Lack of Independence), Kutokuwajibika (Irreponsbility na kukosa ukomavu (Immaturity).

 Kuna wazazi ambao huwa wanawalinda watoto wao kupita kiwango (Overprotective) na kuwazuia kufanya chochote kwa hofu ya kuwa mtoto ataumia ama atadhurika kwa namna moja ama nyingine. Kauli kama ‘‘Usimguse paka atakuparua’’ ‘‘Usikimbie utaanguka’’ ‘’Usicheze nje’’ n.k zitamfanya mtoto akuwe huku akiogopa kufanya chochote kile na kuwa PASSIVE (mtu anaekubali kirahisi chochote anachoambiwa na watu wengine pia maamuzi anayofanyiwa na watu wengine).

 

AdvertisementMtokambali 728x90