Tangazo

BAKING SODA (Magadi Soda) ni zaidi ya kiungo cha kukandia maandazi, mikate na keki. Inaweza kutumika kusafisha, kung’arisha vitu, kuondoa harufu mbaya, kuondoa madoa n ahata kutibu.

 • KUSAFISHA JIKO/OVEN & ENEO LINALOZUNGUKA JIKO. Mara nyingi majiko huwa yanagandia uchafu kutokana na mafuta na huwa sio rahisi kuondoa uchafu huo mpaka usugue sana. Ila nyia rahisi na isiyohitaji nguvu ni kuchanganya baking powder nusu kikombe na maji nusu kikombe kisha nyunyuzia kwenye jiko lako na sehemu ya jikoni ilitogandia uchafu na uache usiku kucha. Asubuhi uchafu wote utakuwa umekwishalainika. Chukua kitambaa ama sponge kufuta uchafu.
 • KUONDOA HARUFU MBAYA KWENYE FRIJI. Wakati mwingine huwa zinakuwa  na harufu ambazo sio nzuri sana. Ili kuifanya friji yako iwe na fresh smell muda wote chukua bakuli ama kikombe uweke baking powder vijiko vitatu vya chakula kisha uweke ndani ya friji yako. Baking powder itanyonya harufu mbaya na kuacha friji yako ikiwa fresh.
 • KULAINISHA MIGUU. Changanya baking powder robo kikombe, vinegar kikombe kimoja na maji ya uvugu vugu vikombe vitano kisha uloweke miguu yako kwa dakika 15-25 kabla ya kusugua taratitu.
 •  KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI. Changanya kijiko kimoja cha chai na maji nusu glass kisha usukutulie na kutema.
 • VIPELE BAADA YA KU-SHAVE. Kama una kawaida ya kupata vipele baada ya kushave tumia baking powder kama after shave ili kuepuka tatizo hilo.

 • KUTUNZA SINK LA JIKONI. Ili kufanya sink lako lisiwe na harufu mbaya pia kusaidia lisizibe kirahisi mwaga nusu kikombe cha baking powder kwenye sink kisha ufungulie/umwage maji ya moto kwenye sink.
 • KUONDOA HARUFU MBAYA KWENYE VIATU. Nyunyuzia baking powder ndani ya viatu vinavyotoa harufu mbaya pale unapokuwa huvivai na uvikung’ute kuitoa pale unapotaka kuvivaa.
 • MIGUU INAYOTOA HARUFU. Kama miguu yako inatoa harufu, kweka nusu kikombe kwenye maji kiasi na uloweke miguu yako kisha uisuuze na kuikausha vizuri mara mbili kwa wiki.
 • KUNG’ARISHA MENO. Tengeneza paste upake kwenye meno kisha uache kwa dakika mbili kabla kuswaki.
 • KUONDOA UCHAFU KWENYE MATUNDA NA MBOGA MBOGA. Nyunyuzia baking powder kidogo pale unapoosha matunda na mboga mboga kuhakikisha ni safi na salama kwa kula.
 • KUSAFISHIA CUTTING BOARD (KIBAO CHA JIKONI). Vibao vya jikoni huwa vinabaki na uchafu wa nyama na huwa na rangi inayotokana na vile tunavyokuwa tumekatia (matunda na mboga mboga) hata baada ya kuviosha. Ili kuondoa tatizo hili nyunyuzia baking powder na maji kidogo kisha uache kwa dakika 15-20 kabla ya kukisugua kwa sponge.

 • KUONDOA KIUNGULIA (HEARTBURN) NA TATIZO LA TUMBO KUJAA GAS. Chukua nusu kijiko cha chai baking powder uchanganye na nusu kikombe cha maji kisha unywe.
 • MADOA KWENYE NGUO. Kuondoa madoa weka nusu kikombe cha baking powder, sabuni ya kufulia na maji kisha uloweke nguo zako kwa muda kabla ya kuzifua.
 • SINK LA BAFUNI, BATHTUBS NA TILES. Ili kufanya bafu lako liwe safi(sparkly clean) na libaki na harufu nzuri nyunyuzia baking powder na uache kwa muda kabla ya kusafisha.

 

 

AdvertisementMtokambali 728x90