Ni kwa nini Watu waliofanya Vizuri Darasani hawafanikiwi katika maisha?

Tangazo

Wakati tulipokuwa wadogo, tulifundishwa yakwamba kama tunataka kufanikiwa katika maisha ni lazima tusome kwa bidii na kupata matoke mazuri darasani. Kupata “A” ndio lilipaswa kuwa lengo letu ili tufanikiwe katika maisha. Lakini kiuhalisia ni watu wangapi waliopata A na B+ darasani unao wajua wamefanikiwa kikamilifu katika Maisha baada ya Kuwa wakubwa?

Wale vijana wakike na wakiume waliokuwa na nidhamu darasani na bidii darasani, waliokuwa wakifanya Kazi za darasani kwa muda na kusahihishwa kwa muda kisha kupata Matokeo mazuri huishia kufanya kazi ambazo hawazipendi Licha ya kwamba wanapata kipato na kuendeleza maisha ya kila siku. Je ni kwa nini hivi? Je hatukuambiwa kwamba Tukisoma nakufanya vizuri katika masomo basi tutafanikiwa katika maisha??

Yale mambo muhimu tunayoyahitaji ili kufanya vizuri na kufanikiwa katika maisha hayafundishwi mashuleni!

Siko hapa kukupotosha ama kuupotosha uma ili Uache/waache masomo hapana. Bado shuleni kuna masomo kama LUGHA, HESABU, MUZIKI, STADI KAZI n.k ambayo nayo haya yana Umuhimu katika maisha yetu ya kila siku. Nachojaribu kusema hapa ni kwamba MITAALA yetu mashuleni sio Kamili. Kuna mambo mengi ya Muhimu katika maisha yanakosekana katika Mitaala hiyo. Na kuna mengi Mabaya yaliyoko katika Mitaa hiyo.

WAZO:”Wanataka sisi tunyooshe kidole Juu kisha tusubiri kuchaguliwa kujibu, Wanataka tuwaombe watu wengine ruhusa yakufanya jambo fulani, Wanatufundisha Kusoma Ideas za wengine kuliko kutengeneza za Kwetu,They teach us to trust that they have our largest, best, life-long interests at heart; without letting on that they are merely interested in our achievements.”

Kimsingi, ili ufanikiwe katika masomo darasani basi huna budi kuwa mtiifu, na haijalishi upo vizuri kiakili ama sivyo itategemea matarajio ya Mwalimu wako. Na badala ya Kumsaidia mwanafunzi ni namna gani wanapaswa kufanya jambo Fulani, wao hulazimisha mwanafunzi kufuata sheria na kumuacha katika chumba ambacho mwanafunzi anashindwa Kufikiri kwa kina na Kuwa mbunifu. Lakini kiuhalisia Maisha hayako hivyo watakavyo Walimu huko Mashuleni.

Kufanikiwa katika Maisha, ni lazima ufikiri nje ya Box na sio kufanya yale wanayoyafanya wengine. Na kuna mambo mengine yakufanya nje ya Masomo, mfano Ni nini cha kufanya ili uweze kuwa mtu wa Furaha, Ni kwa namna gani utaweza kuwa na Mahusiano Bora, ama ni kwa namna gani utaweza Kuishi maisha Ya MAANA nk.

Kufanya Vibaya darasani hakukufanyi wewe Kushindwa katika maisha(Takwimbu zinaonyesha).

Ikiwa ukweli ni kwamba kila mwenye angalao Elimu ya chini basi atakua na nafasi yakufanya poa katika maisha sababu tuu ana ujuzi aliopata huko Shuleni/chuoni, Lakini takwimbu zinaonyesha kwamba wale wote waliofanya vibaya darasani nakufeli masomo hawakufeli Maisha. Pengine Utakua umekwisha pata kumsikia Steve Jobs(Mwanzilishi wa Kampuni ya APPLE Soma zaidi kuhusiana na Steve Jobs), Richard Branson, Oprah Winfrey na Jim Carey nk hawa hawakufanya vizuri darasani lakini Katika Maisha Wamekua mfano wakuigwa. Wapo wengi mno ambao hata shule hawakumaliza ila leo hii ndio Matajiri wakubwa Ulimwenguni. Kwa Mujibu wa Current Biography Yearbook (Toleo la 1959-2005 & 2007), Wale wote waliotajwa katika List hiyo, 768 ni wale walioacha shule lakini wamefanikiwa kimaisha katika nyanja mbali mbali.

  • Billionaires: 26
  • Nobel Prize Winners: 10 (6 Literature, 2 Peace, 1 Physics, 1 Chemistry)
  • Oscar Winners: 63
  • Oscar Nominees: 105 (includes above)
  • Best-Selling Authors: 56
  • Presidential Medal of Freedom recipients (U.S.’s highest civilian honor): 25
  • Congressional Gold Medal recipients (U.S.): 12
  • Knighthoods: 28
  • List inaendelea………

Unaweza kuona List ya watu waliofanikiwa kimaisha kwa Kubofya hapa. Na sasa umweza kufahamu tofauti ya Kufanya Vizuri darasani na Kufanya Vizuri katika maisha. Sasa kazi ni kwako kuchagua Ufanye nini …

Maisha ni somo pana sana, hivyo hata hutoweza kuelezea mafanikio ya mtu kwa kusoma Sura Moja tuu ya somo hilo(Maisha).

Kama umekwisha maliza masomo yako, tafadhali endelea kujifunza maana Elimu uliyopata darasani haitotosha kukusaidia wewe kufanikiwa katika maisha. Na kama bado unasoma, iwe unafanya vizuri ama vibaya Darasani usiyachukulie matokeo yako ya darasani serious kiviile. Kamwe usiwe kipofu kwa kuwa umeambiwa kwamba Ili ufanikiwe katika maisha basi lazima ufanye vizuri darasani, au kufuata sheria basi utafanikiwa. Lakini pia usizivunje sheria hizo mpaka pale utakapo fahamu ni Kwa sababu gani ziliwekwa hapo. Kam na wewe ni Mwalimu ama mzazi, usijikazie sana katika Grades anazopata mtoto bali wekeza katika kipaji chake na Mitazamo yake.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


 

AdvertisementMtokambali 728x90