Tangazo

1994 Nonda Shaaban Papii alikuwa ni mmoja wa Vijana Yosso wa Yanga,…na kabla ya kuja Bongo alikuwa akiichezea Atletico ya Burundi ambayo nayo ilimpiga Benchi kiasi cha kugeuka DJ wa Redio mjini Bujumbura.

Hata hapo Yanga bado hakuaminiwa , ikabidi aanzie Yanga B akiwa na watu kama Anuar Awadhi na Maalim Saleh ‘Romario’ …hivi angewezaje kupata Namba Yanga ya wakubwa mbele ya Mohammed Hussein Mmachinga na Edibily Jonas Lunyamila?

Baadae Nonda na wenzake walifanikiwa kupandishwa Timu ya Wakubwa,…Hatimaye Mwaka 1995 ndiyo alijiunga na Vaal Professional ya Afrika ya Kusini baada ya kumuona akiichezea Yanga katika Michuano ya Afrika, …tena aliingia sub kwa kuwa namba yake alikuwepo Mohammed Hussein Mmachinga a.k.a Chinga One……na ndipo Vaal Proffesional ilipomuona katika Jicho ambalo Viongozi wa Yanga walikuwa Vipofu kabisa!,

Nasema hivyo kwa sababu kama Viongozi wa Yanga chini ya George Mpondela”Castro” wangekuwa wanaona sawa sawa basi Yanga ingejiingizia Mamilioni ya Fedha katika Safari yote ya soka ya Nonda hapa Duniani hasa alipokuwa anauzwa kutoka klabu moja kwenda nyingine kama Sheria za(Fifa) zinavyotaka kwamba mchezaji anapouzwa, basi lazima kuwe na faida kwa klabu inayomuuza katika misingi ya asilimia.

Lakini inasemekana Nonda aliuzwa kwa dola 10,000 tu na viongozi wakachanganyikiwa…yaani hawakutazama Vipengele vya Kimataifa vinasemaje juu ya Mikataba,..laiti kama Nonda angeuzwa kwenda Club nyingine!….hivyo wakazubaa bila kuingia mkataba wa uhakika ambao ungeisaidia Yanga kuendelea kuingiza fedha kwa miaka mingine mingine mingi baadae.

Matokeo yake NONDA akaenda South Afrika, Vaal Proffessional wakawa wajanja wakaandika kwenye wasifu wa Nonda kwamba walimunua kutoka YANGA Academy, yaani (Youth Career) halafu Senior team ameanzia hapo Vaal South Afrika….Jamani tujiulize hivi YANGA ina Academy?…..Wasouth wakatupiga bao.

Vaal Proffesional ambayo ilimpata Nonda kwa dola 10,000 tu, yenyewe ikamuuza kwa dola 150,000 kwa klabu ya FC Zürich ya Switzerland, hiyo ilikuwa ni mwaka 1996, hapa Yanga ingepata dola 15,000, lakini ikaambulia patupu.

Nonda akawa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Switzerland, na mwaka 1998 akauzwa Stade de Rennes ufaransa kwa dola milioni 9, Hapa Yanga ilipishana na 10 percent yaaani dola 900,000, ikaambulia Patupu,….na miaka miwili baadaye Nonda akajiunga na AS Monaco kwa uhamisho uliovunja rekodi kwa dola milioni 25, hapa Yanga ilitakiwa kupata dola 250,000….ikaambulia patupu.

Bado Nonda akaenda AS Roma, Blackburn Rovers na mwisho Galatasaray ya Uturuki,…Safari yote hiyo ya Fedha Yanga ilitoka bila kupata 10 percent huku Viongozi Masamjo wakibaki na Kumbukumbu ya “Nonda alipita hapa”….wakati Fedha inaingia South Afrika

Case closed, going to swim.
0719 122 155@Pio Pius

AdvertisementMtokambali 728x90