Tangazo

“Hakuna mahali pengine kama nyumbani “- Francis Mawere

Hapo awali kulikuwako na Misemo kadhaa juu ya Nyumbani, maneno hayo ni kama “Nyumban ni Nyumbani hata kama ni Kichakani” na misemo hii ilitumika vilivyo kuhamasisha watu kupenda nyumbani kwao.

Hivi karibuni kumeibuka tabia ya watu kukimbia na Kukana kabisa nyumban kwao walikotoka. Siwezi nikafahamu kiundani ni kwa nini hasa watu hawa hufanya hivi, Pengine hali za maisha na Umasikini ulio kithiri huwafanya watu kukimbia na Kukana kabisa nyumbani kwao.

Yawezekana huu ukawa ni ulimbukeni kwani Maisha ni popote na kama umeshindwa kuleta maendeleo na kuondoa haliu ilokufanya ukimbie hapo nyumbani kwenu tuu utaweza sehemu nyingine?

Labda wengi wanaofanya hivyo hawafahamu kufanya hivyo ni sawa na Kumkufuru Mwenyezi Mungu alowaumba na kuwaweka katika nyuma ile. Nafahamu wengi wanaokimbia majumbani kwao ni sababu tuu ya hali duni ama Machungu waliyowahi kuyapata huko nyumbani kwao kiasi kwamba wanaapa kutokukanyaga nyumbani kwao Daima, ila watu hao wanapaswa kutambua chimbuko lao ni lipi na Linapatika wapi.

Ziko sababu nyingi za mno za Kudai kwamba nyumban ni Nyumbani na hakuna pahala Pengine kama nyumbani.

#1: Uhuru na Mamlaka kamili.

Kuna mambo mengine hata kama wewe ni mzoefu wa eneo hilo ulilopo(Ugenini) Huwezi kamwe kufanya ila ukiwa nyumbani unaweza kufanya tena bila hata hofu yeyote. Mfano mzuri tuu ni pale unapokua Ugenini na kutaka kubadili Desturi za eneo lile kwa kua tuu hazipendezi hasilani, jambo lile litakupa wakati mgumu na mwisho wa siku utajikuta ukiangukia pua sababu tuu haukua na Uhuru na Mamlaka katika eneo lile kwa sababu wewe ni Mgeni katika eneo lile. Jambo hili litakuumiza akili na nafsi yako kwa Ujumla na kujikuta ukipoteza amani ya moyo wako Muda wote.

#2.Ulinzi na Usalama wakutosha.

Wakati mwingine tukubali tuu ugenini hakuna amani zaidi ya nyumbani, usininukuu vibaya maana najua utaniuliza je Kama kwenu kuna Vita amani utaipata wapi? ila Usalama ninouzungumzia hapa ni Ule unapatikana kutokana na uwepo wa Wazazi wako ama Ndugu zako na Familia yako.

#3.Msaada wakati wowote ule.

Nyumbani kwenu wanaweza wasikupatie msaada ambao wewe utatakua unahitaji kwa asilimia mia Mfano pale unapokua una changamoto za Kifedha, Ila wakakupa hata Mawazo na mawazo yale yakakufanya ukafanikiwa angalao Kwa kiasi Fulani. Lakini Jambo hili linakua ni aghalabu huko Ugenini kwani utakua huna Uhuru wa kujieleza vilivyo.

Ni hayo Tuu kwa leo nafahamu ua mengi zaidi ya haya, Hivyo nieleze mengine hapo chini kwenye Comment Box.

AdvertisementMtokambali 728x90