Ondoa Mambo haya 8 ili kufanikiwa katika Maisha.

Tangazo

Watu wengi hufikiri kwamba njia nzuri ya kufanikiwa ni kufanya na kufahamu mengi zaidi katika maisha ya kila siku.Wakati mambo haya yanaweza kukusaidia, njia nzuri ni kuyaacha na kuyatupilia mbali mambo yote ambayo hukurudisha nyuma kimaendeleo Kila kukicha.

Badala ya kuongeza mambo mengi katika maisha yako, jaribu kuyaondoa yale yote ambayo yanakuharibia njia yako ya mafanikio katika maisha. Baadhi ni rahisi mno kuyasahau, na mengine yanahitaji muda kidogo kuyasahau.

Haya ni mambo nane(8) ambayo unapaswa kuyaondoa katika maisha yako ili kufanikiwa.

1.Ondoa kusamehe kila mara na kila jambo.

Watu wote waliofanikiwa huwa hawa-walalamikii familia zao ama rafiki zao ama Mabosi zao katika maisha yao. Na badala yake, huelewa kwamba wao ndio wahusika katika hali zote za maisha zinazo wakabili. Wakati mwingine kusamehe kunaweza kukurudisha nyuma mno na wakati huo unakua unajidanganya mwenyewe na hili litakurudisha nyuma katika maisha.

2.Ondoa kufanya mambo katika ukamilifu(Perfectionism).

Ukamilifu ni jambo ambalo haliwezekani kamwe. Kujaribu kufikia Ukamilifu ni kupoteza muda wako mwingi. Badala ya kuyaogopa mapungufu na makosa unayofanya, jaribu kujikita katika yale mambo madogo yanayoweza kukuimaisha kidogo kidogo. Hakuna aliyeumbwa mkamilifu ila mtu yeyote anaweza kufanya maamuzi yakuwa mtu mzuri.

3.Punguza Hofu.

Watu wengi hujishusha na kuwa wadogo pasipo wao wenyewe kujijua. Hunyamaza pale wanapokua katika majadiliano wakati wanapaswa kuongea yale wanayokuwa wakinua kabla ya majadiliano, wanaogopa kufanya makosa na kujiingiza katika hatari. Hali hii itakufanya kupoteza mhimili wa mafinikio yako. Ongea, kimbizana na ndoto zako.

4. Punguza kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.

Huwezi kufanya kila kwa wakati mmoja, kujaribu kufanya kila kitu kwa wakati mmoja ni mzigo mkubwa mno. Utajikuta katika msongo wa mawazo na kupoteza thamani ya vile unavyo fanya. Badala ya kuyafanya hayo, jaribu kujikita katika jambo moja tuu lile ambalo unaliamini na ni moja kati ya malengo yako.

5.Ondoa kuwa na mawazo yasiyo badilika(A Fixed Mindset).

Watu wengi wana mawazo mgando na hawataki kuweka bidiii katika kujifunza mambo na kubadili fikra na mawazo yao. Hawapendi mabadiliko kamwe, wanaamini katika mawazo yao tuu. Mwisho wa kukomalia mawazo yako siku zote ni Kuangukia pua. Jaribu kujifuinza mambo mbali mbali ili kuondokana na mawazo yako hayo ambayo hukufanya kuangukia pua kila kukicha.

6.Ondoa mawazo yakutaka kufanikiwa kwa usiku mmoja(Kufanikiwa kwa haraka).

Kuna baadhi ya watu huamini kwamba mafanikio huja kwa usiku mmoja tuu au huamini kwamba mafanikio huja kwa Zali. Kamwe huwezi kufanikiwa kwa kungojea bahati ingawa mambo ya bahati(ngekewa, zali) nayo ni sehemu ya maisha. Ukweli ni kwamba, mafanikio ya mtu huchukua muda mrefu kumfikia. Panga mipango mathubuti juu ya maisha yako na fanyia kazi ndoto zako utatoka tuu.

7.Achana na watu ambao ni sumu maishani mwako.

Katika maisha ya mwanadamu rafiki ni mtu wa muhimu mno lakini kuna baadhi ya marafiki ni sumu kali mno(Ni wabaya). Hakuna haja ya kuwa na watu wa aina hii kamwe maishani mwako maana wao kazi yao kubwa ni kubomoa tuu na sio kujenga. Jitahidi kukaa na watu wenye Malengo na maono katika kazi zao utafanikiwa.

8.Kuwa muwazi usijivunge.

Unajua kuna yule mtu ambye hufanya jambo mahali ili tuu kuwaridhisha watu wale lakini ukweli ulioko mioyoni mwa mtu huyo ni  Hapendi kufanya jambo lile. Halii hii inatoa picha gani mbeleni…, ukweli ni kwamba kujivunga wakati moyoni hutaki ni kujidanga na jambo hili litakupotezea muda wako mwingi jambo ambali litakurudisha nyuma siku zote.

AdvertisementMtokambali 728x90