Tangazo

Paranoia ni kitendo cha mtu kuwa na tabia ya kuwa na wasiwasi,hofu, mashaka, na kutoamini mtu mwingine bila ya kuwa amepewa sababu ya kufanya hivyo. Na mara nyingi hii huwa inasukumwa na wivu uliopitiliza kiasi , muhusika kutokujiamini(low self-esteem), imani ya kwamba hakuna mtu ambae ni muaminifu n.k

Paranoia ni zaidi ya sumu kwenye mahusiano. Inapotokea mmoja ya watu wawili ndani ya mahusiano anakuwa ama ana-act paranoid inapunguza amani ndani ya mahusiano, kunakuwa na tuhuma nyingi kumuelekea mtu ambae anaweza akawa hana hata mpango wa kufanya yale anayoshutumiwa amefanya ama anafanya. Hali hiyo huweza kupelekea mahusiano yakavunjika hata kama mapenzi bado yapo kwasababu ‘’mtuhumiwa’’ anachoka shutuma za kila siku na anashindwa kujitetea muda wote  na kwa kila jambo huku mwenzake akiwa hayuko tayari  kuelewa chochote zaidi ya kile anachodhani yeye.

Ndio pale unapokuta mtu ana-question na kutilia wasiwasi kila text message inayoingia kwenye simu ya mwenzi wake hata inayotoka kwa ndugu zake, mitoko na mizunguko hata ile inayohusiana na kazi tu n.k. Anaona kila aina ya kutendwa kwenye kila kitu mwenzake anachofanya. Mwenzake akila chakula kidogo, ametoka kula kwa hawara, mke akianza kupendeza/kujijali basi kuna mwanaume mwingine zaidi yake, jirani akiulizia “mama nanii hajambo” basi lazima kuna kitu kinaendelea baina yao. Alimradi kila kitu kimeficha jambo nyuma yake na hata akieleweshwa hataki kuelewa.

Ukibahatika kupata  mtu ambae anaridhisha moyo na nafsi yako muheshimu kwa kumuamini mpaka pale atakapokupa sababu ya kuamini vinginevyo. Jitahidi kuwa muelewa pale unapoeleweshwa kitu ili kulinda mahusiano yenu. Usione vitu ambavyo havipo, usilazimishe matatizo wala usitafsiri vitu tofauti wala usivipe vitu maana zaidi ya ile iliyo halisi. Mahusiano na ndoa vinatakiwa kuwapa watu furaha na sio kuwaondolea furaha, kuwapa mawazo lukuki na kugeuka karaha. Usiwe mmoja wa watu wanaowafanya wenzi wao watamani asubuhi isifike haraka kila mtu anaende kwenye mizunguko yake wala muda wa kurudi nyumbani usifike haraka kwasababu anajua maswali na tuhuma atakazokutana nazo bora hata kuwa interrogated na polisi. Itafika mahali mwenza wako atachoka kujitetea na kujieleza kwako over and over again na atajikuta akikosa hamu ya kuwa karibu na wewe kwasababu anajua lazima amani itatoweka kati yenu.

Kuna movie moja ya zamani inaitwa WIFE vs SECRETARY inayohusiana moja kwa moja na hii mada. ‘‘Mwanaume ni boss mkubwa kwenye publishing house. Katika harakati za kutaka kununua akajikuta anatumia muda mwingi sana kufanya kazi (mpaka usiku )akiwa na secretary wake. Mkewe kuona vile akaanza kumu-accuse mume wake anatembea na secretary wake, ku-doubt anachoambiwa na mume wake na kung’ang’ania kile alichodhani kuwa kweli. Hiyo hali ikatengeneza distance kati yao kiasi kwamba kama mume wake asingekuwa strong angeangukia kwa secretary kweli kweli.’’

Hii quote ni kutoka kwenye hiyo movie…“all the fighting and worrying people do, it always seems to be about one thing. They don’t seem to trust each other. Well, I’ve found this out. DON’T LOOK FOR TROUBLE WHERE THERE ISN’T ANY, BECAUSE IF YOU DON’T FIND IT, YOU’LL MAKE IT.”

Usitengeneze matatizo pale pasipo na matatizo.

AdvertisementMtokambali 728x90