Sababu 5 ni kwa nini watu wano-lia sana wanakua vizuri kiakili.

Tangazo

Karibu mtokambali na leo nitakupatia Sababu 5 ni kwa nini watu wano-lia sana wanakua vizuri kiakili.

Kwa bahati mbaya hisia zote hazikuumbwa sawa. Hisia ambazo zinakubaliwa na wengi zaidi ni Furaha, Ulinzi na mafanikio ya kitu fulani. Tumekua tukiambiwa kwamba Furaha hutuleta karibu na mafanikio na zaidi kutuleta karibu na watu.

Hofu nayo hutumika kwa sana maana kila mmoja wetu kaipitia na atazidi kuipitia kivyake vyake. Tumekua tukihofia mambo mengi kama vile:- Kuacha kazi, mapenzi, kugombana na marafiki tuwapendao katika jambo fulani nk.

Hasira ni hisia za aina yake pia, tumekua tukizipitia hizi hisia kila kukicha, unaweza patwa na hasira kiasi ambacho unatamani hata kumtoa/kuutoa mtu uhai wake ila baada ya muda hasira hukata na kurudia katika hali ya kawaida.

Mjimuisho wa hisia zote hizo husababisha wengi kujikuta katika hali yakububujikwa na machozi. Mtu yeyote anayeweza kustahimili hisia hizi muda wowote basi anakua na uwezo mkubwa kiakili kwa sababu zifuatazo:-

1.Huwa hawaogopi hisia zao.

Hivi kweli ukiwa umezidiwa na furaha utaweza kuficha tabasamu lako? kwa mfano umekua kazini na ukawa umechoka nakurudi nyumbani na kukuta rafiki yako ambaye hana kazi kanywa kinywaji chako ambacho ulikia unakiwazia tangu ukiwa kazini hutokasirika? Hivi ukiwa na hasira zilizokufika Hapaa hutolia??

Watu wote ambao hupuuza machangu na hasira hujidanganya nafsi zao juu ya ukweli wa maisha. Kukasirika ama Kulia sio ishara ya udhaifu ni ishara ya kwamba wewe ni mwanadamu na una hisia.

2.Wanafahamu uponyaji ulioko katika machozi.

Kama vile matone ya mate yatokavyo katika tarumbeta(Mbiu), ndivyo machozi yatiririkayo katika mboni zako huondoa msongo wa mawazo, Uoga, na kuchanganyikiwa katika akili yako na mwili wako. Machozi Husafisha moyo, hutuliza akili.

Zaidi ya yote hayo, kisayansi machozi yana sumu ambayo huua vimelea(Bacteria) walioko machoni kwa asilimia 90 hadi 95 hivyo kuoneza iwezo wakuona vizuri.

3.Wanafahamu matibabu ya kulia yalivyo.

Masomo mengi ya Kisaikolojia yameonyesha kwamba unapolia, Ubongo huruhusu homoni ijulikanayo kama endorphin kuachiliwa ambapo kazi kubwa ya Homoni hii ni kukufanya wewe ujisikie vizuri na kufanya kazi kama pain Killer mwilini mwako.

Hata kama tatizo litazidi kukusumbua baada ya kulia, hakuna ubishi kwamba kitendo cha wewe kuendelea kulia kitakusaidia kuondoa hisia mbaya zinazozidi kukuandama. Jambo hili litakurusu kufikiria zaidi tatizo lile na kupata ufumbuzi kuliko kukaa nalo na kuzidi kukuandama.

4.Hawajali majukumu ya Kijinsia na huwa hawajali matarajio ya jamii.

Katika jamii zetu wengi tuna amini kwamba wanawake ndio watu wanaopenda kulia lia kila mara eti kisa ni wadhaifu jambo ambalo tunakua tunakosea kwa kusema hivyo na kuamini hivyo. sio kwamba wanaume nao hawaliii, ila ukweli ni kwamba hata wao hulia kama ilivyo kwa wanawake sema tuu ni kwa vile tushajiwekea mipaka kwamba mwanaume halii.

Huu ni uwanja wa mapambano katika majukumu ya kijinsia yaani wanaume na wanawake hupambana. Wale wote wanao lia na kukasirika katika mhadhara sio wenye akili pekee bali hata wanaharakati kijinsia na Kiafya.

5.Hukaribisha wengine kutokukimbia hisia zao.

Yawezekana napenda kulia au kutokujiingiza katika hasira pale napoona nakaribia kukasirika. Kwa pamoja tunapambana na jinamizi linalo tuletea msongo wa mawazo na hasira na kututoa machozi kila kukicha.

Pale tunapo ruhusu hali ya maumivu kuwa nasi, tunakua tunawakaribisha na wengine kujiunga nasi katika machungu. Watu hao wanaweza kuwa ni wale ambao teyari tunafahamiana ama wale ambao hatujuani. Wale wote wanao kubali machungu na vulio katika jamii husababisha wengine nao kufanya hivyo.

Na hizo ni Sababu 5 ni kwa nini watu wano-lia sana wanakua vizuri kiakili.

Mpaka hapo nimefikia ukingoni ni Mimi swahiba wako Francis Mawere mti mkavu usochimwa Dawa, na hapa ni nyumbani kwangu, Nyumba ya Mambo na Burudani. Ungana nami Twitter @Mawere3 

AdvertisementMtokambali 728x90