Tangazo

Wazo la kuwa na free blog ama Free web siku zote huwepo kichwani mwa mtu yeyote mwenye ndoto ya kuwa na blog ama Tuvuti. Siku hizi katika Internet kuna makampuni lukuki yanayotoa huduma ya Hosting hata kama ni WordPress. Unashangaa si ndio?? Je ni kwa nini watu wengine hawapendi kutumia free WordPress website? katika chapisho hili nita ainisha sababu 25 ni kwa nini kuwa na Free blog au website ni idea/wazo mbaya jambo ambalo unapaswa kuepuka hata kwa gharama yeyote ile.

Namaanisha nini naposema Free blogs ama free websites?

Wengi wa wale ambao ndio wanaanza mambo haya ambao wanaotaka kufungua Blog/web zao hupenda kutumia gharama ndogo kwa ajili ya kufanikisha jambo hili. Hivyo wao huenda Google nakuandika free website kisha zinajitokeza kampuni nyingi zinazotoa hudama za Hosting bure kabisa na kisha wanachagua moja kati ya kampuni hizo na kujiunga nao.

Wazo la wao kujiunga na Kampuni hizo ni kumiliki blog ama tuvuti zao pasipo kulipia hata shilingi moja ama kwa gharama ya chini kabisa ambacho ni sawa na Bure.

Ndio utajisajili na kampuni hizo na kisha utapata kumiliki Blog/ web yako lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda na kufahamu mambo mengi utajikuta unagundua kwamba Bure sio Bure wakati wote. Utakuta mashariti kibao na vizuizi vingi ambavyo ili uweze kuepuka vizuizi hivyo, utalazimika kuingia tena mfukuno na kuwalipa hao hao waliokupa Bure

1.Blog ama web za Free mara nyingi Huwa Slow sana.

Makampuni haya yanayotoa huduma hii ya Free hujikuta wakiweka mamia ya blogs na Websites kwenye Severs zao ambazo ni ndogo jambo ambalo hupelekea blogs hizo kuwa slow sana na matokeo yake hupelekea ufanyaji kazi wa blog/web hizo kuwa mbovu nakuathiri blog hizo katika SEO(Search Engine Optimazation).

2. Web address isiyokuwa ya kitaalamu(Unprofessional web address).

kuwa na domain name kama www.blogyangu.freewebsite.com sio jambo jema kabisa. watembeleaji wa blog hiyo wakiingia katika blog yako watajua kwamba hauko makini na kazi yako. Na wakati mwingine inawawia vigumu kuingia katika site yako hiyo kutokana na web Address yako kuwa ndefu na ngumu. Ni vyema ukachagua domain name yako peke yako ambayo itakua ni Fupi na inayoeleweka mfano www.jinalako.com. Na kibaya zaidi katika makampuni hayo ukiwaomba kutumia Domain yako watakuambia tumia Premium service zao ambazo watakuhitaji kulipia dola 20 -25 ambapo katika site kama BLUEHOST utachajiwa dola 8 Tu.

3.Wanaweza kuizima website/blog yako muda wowote pasipo na taarifa.

Site not found

Kuna wakati utashtukia kwamba web yako hiyo haipatikani tena na jambo hilo hutokea pasipo wewe kupewa taarifa yeyote na mbaya zaidi huwa hawakupi nafasi ya kuchukua Data zako na hivyo unakua umefanya kazi bure na kupoteza Muda wako.

4. Wanaweza kuuza taarifa zako.

Kumbuka kwamba na wao wanahitaji kutengeneza pesa kupitia huduma yao hiyo. Na mchongo ni kwamba wewe si hauto lipia chochote! sasa kama hautolipia chochote, wewe utakua moja kati ya bidhaa zao. Wanaweza wakauza taarifa kama vile email address yako na web address yako kwa makampuni mengine pasipo wewe kujua na mwisho wa siku ukajikuta umeangukia mikononi mwa Hackers bila hata kujijua.

5. Hakuna WordPess

Kamwe hutoweza ku-install wordpress kwenye site zao. Jambo ambalo itakuwia vigumu kutumia tools zao katika kujenga web/blog yako hiyo. Ukiwa na Hosting Provider kama BlueHost mambo haya ni Bure kabisa. Utaweza Kuinstall WordPress na kutengeneza Web/blog makini kabisa kuliko kutumia hizo free Sites.

6.Low disk storage

Siku zote hawa jamaa huwa hawakupi storage yakutosha kwa ajili ya web/blog yako. Mara nyingi wao huhifadhi web/blog kwenye sehemu ndogo ya servers zao na nyingine kwenye hard disk zao hivyo basi hulazimika kutoa storage ndogo ambayo ni limited na unapokua umefika ujazo huo waliokupa, utalazimika kulipia ili kupata storage kubwa zaidi

7. Hakuna msaada wala huduma kwa wateja.

Mara nyingi makampuni hayo hutoa huduma tuu lakini hawatoi msaada wowote na wala hawana vitengo vya huduma kwa wateja, hivyo basi unapokuwa umepata tatizo ama umekwama pahala hutoweza kusaidika kwa urahisi.

AdvertisementMtokambali 728x90