Support System – kuepuka depression!!

Tangazo

Kuna umuhimu mkubwa sana wa watu kuwa na SUPPORT SYSTEM (mtu maalum anaemumini ili kuzungumza nae kwa nia pale anapokuwa amezeidiwa na mawazo, matatizo na hofu ya jambo fulani.). Msongo wa mawazo (Stress) ukizidi huzaa depression. Depression huweza kupelekea mtu akafanya maamuzi ya kujidhuru ama kudhuru walio karibu nae kwa namna moja ama nyingine. Kipindi cha nyuma kidogo kuna tukio la kusikitisha lilitokea hata kunisukuma kuongelea jambo hili.

Kwa ufupi ni kwamba kuna dada wa kiKenya aliyekuwa  akiishi Sweden alishukiwa  kuua watoto wake wawili, mmoja wa miaka nane na mwingine miaka mine kwa kuwatupa kwenye ziwa dogo lililokuwepo jirani na alipokuwa akiishi. Kutokana na maelezo ya watu waliomfahamu kwa karibu ni kwamba huyu dada alipoteza kazi yake kipindi cha summer baada ya kuondoka kazini na kwenda nyumbani kwao  (Kenya) bila ya kupata ruhusa kazini, hivyo aliporudi akakuta kazi sio yake tena, wamemuondoa na kumpa mtu mwingine nafasi yake. Akaomba msaada serikalini ili aweze kujikimu na wanae kwakuwa hakuwa na kipato kwa wakati ule ila for whatever reason social hawakumsaidia. Ikafikia hatua mpaka akakatiwa umeme kwenye apartment yake kwa kushindwa kulipa bili, akajifungia ndani na wanawe kwa zaidi ya wiki moja huku chakula chao kikiwa pizza (nchi za wenzetu pizza sio chakula cha gaharama!!). Mwisho wa siku ndio watoto wakakutwa ziwani.

Hii story nzima imenifanya nifikirie kwamba kuna uwezekano mkubwa huyu dada alipata depression kutokana na matatizo yake na kitendo cha kukosa msaada mpaka akafikiria kwamba ni bora wanawe wafe kuliko waishi katika hali waliyokua nayo. Inawezekana jibu likawa ndio au sio…either way mambo kama haya yanawatokea watu wengi tu kwakuwa na limbikizo la mawazo, hofu, kukosa msaada n.k.

Wengine huwa wanachagua kujiua, wengine kujiweka mbali na watu wengine mpaka wanachanganyikiwa na kujikuta wakiua familia zao (mke/mume/watoto) wakiamini kwamba wanawapunguzia uchungu na mateso kwasababu wanaona hawana namna ya kutatua matatizo yao au ama nguvu ya kushinda kinachomsumbua hivyo kuchagua kifo badala ya kuishi.

Yote hii inatokana na watu kukosa ama kutojua pa kukimbilia.

Unakuta mtu amepoteza kazi ila anashindwa kutegemea ndugu/marafiki zake kwasababu wao wanamtegemea yeye, kwasababu hawako tayari kumsaidia, kwasababu haamini kwamba watamsaidia, woga wa kuonekana ameshindwa n.k. Kitu hicho hicho kinaweza kusababishwa na mtu kukutwa na janga ambalo hata kama halihitaji pesa m.f kubakwa/manyanyaso mtu anahitaji kushea matatizo yake na mtu mwingine ili asije akazama peke yake. Mtu anapokosa support akazama kwenye matatizo/mawazo/hofu peke yake ndipo depression inapogonga hodi na kujikaribisha yenyewe. Na inapomtawala mtu ndo unashangaa kusikia fulani kakutwa amejinyonga unabaki kujiuliza ilikuwaje mbona alikuwepo kazini jana .

Ni muhimu kila mtu akawa na mtu anaemwamini kiasi cha kutosha kumweleza pale anapokuwa matatizoni kwa sababu yoyote ile. Inawezekana mtu huyo asiwe na msaada unaouhitaji kwa wakati ule ila mawazo yake ukichanganya na yako yanaweza kukupa solution na pia kumueleza mtu anaekujali kinachokusumbua kutakupunguzia mzigo wa mawazo/maumivu kwasababu unakuwa na mtu mwingine sharing your worries. Yaweza kuwa rafiki au ndugu…mkubwa au mdogo kwako it doesn’t matter.

Create your own support system and make a habit of talkin to them whenever you feel overwhelmed  na ikiwezekana, be someone else’s support system.

Ukihisi mtu wako wa karibu ana kitu kinachomsumbua jaribu kuwa karibu nae ili baadae usije ukabaki kufikiria ”Ningejua ningeweza kumsaidia”.

AdvertisementMtokambali 728x90