Tangazo

Tatizo la madawa ya kulevya ni tatizo la kijamii na kitaifa. Tatizo hili hushirkisha makundi mawili ambayo ni..

A. Watumiaji (waathirika) wa madawa ya kulevya.

B. Wauzaji a.k.a wasambazaji wa madawa ya kulevya.

Kwa bahati mbaya, kwenye jamii yetu tumekalia zaidi kusema ”hawa wanatuharibia watoto/ hawa wanatuharibia ndugu zetu/wauzaji ni mashetani/ni wauji ”. Tunaweka nguvu nyingi kwenye kulaumu wasambazaji na wauzaji wa madawa ya kulevya badala ya kuangalia sisi kama jamii tunawezaje kuwaepusha vijana wetu/ vijana wenzetu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Swala la usambazaji ni la kibiashara zaidi, HARAMU, lakini bado biashara. Binadamu ni wabinafsi na muda mwingi watu hufanya vitu kwa faida binafsi na sio kwa faida ya wengine. Ndio maana sumu ipo na inauzwa, bunduki na mabomu nayo vile vile, pombe na aina nyingine za vilevi navyo ni kwa madhumuni hayo hayo, ya kumteka mtu mwingine kifikra/ki-utu na kumtajirisha mtengenezaji/muuzaji wa bidhaa hiyo. Kukubali kushawishika na kujiingiza kwenye kitu ambacho kina madhara kwa mtu ni kosa kwa mtu mwenyewe kwanza kabla ya mwingine yeyote yule kwasababu kila mmoja wetu ana uhuru wa kujiamulia lipi afanya na lipi asifanye..

Sio vyema lawama zote wakatupiwa hao wauzaji na kusahau kujikosoa sisi wwenyewe kama  wazazi, ndugu, jamaa na marafiki  wa muathirika wa madawa ya kulevya kwa kushindwa kwa namna moja ama nyingine kumuweka mtu huyo wa karibu kwenye mstari ili asiingie kwenye janga hilo la madawa ya kulevya on the first place.

Jiulize ulikuwa wapi usiweze kumsaidia mtu wako kabla hajaanza kutumia? Ulitumia nafasi yako vizuri kumuelimisha na kumsaidia kama alikuwa na matatizo binafsi ili yasimsukume kwenye ulimwengu huo wa madawa ya kulevya? Ulim-support alipokuhitaji? Ulimuelimisha kama ni kijana mdogo aliyehitaji muongozo wako? Na kama ni kijana aliyejifunza kutumia madawa ya kulevya kwa kufuata mkumbo na ushawishi wa marafiki tumje umewahi kukaa nae chini ukamfundisha umuhimu wa kuwa na maamuzi binafsi bila kukubali kusombwa na makundi hata kama ataonekana sio mjanja? Fikiria, kama mtu alishawishiwa tu (that means anashawishika) kwanini wewe kama ndugu/jamaa/rafiki hukutumia nafasi yako na kumshawishi kutokujiingiza kwenye mambo kama hayo??

Ninachomaanisha ni kwamba, hao wote wanaolalamikiwa wameharibiwa wauzaji, je  walilazimishwa kutumia madawa ama walijiingiza kwa hiari na matakwa na matatizo yao binafsi?? Chukulia mfano wa msanii Ray C aliyekuwa akimlaumu mpenzi wake wa zamani Lord Eyez kwa kumshawishi atumie madawa ya kulevya , mwisho wa siku aliyefanya maamuzi ya kutumia alikuwa ni yeye au ni mpenzi wake? Watu wengi wanashawishiwa kufanya vitu wasivyovifanya ila mwisho wa siku maamuzi ni ya Yule anayeshawishiwa na sio mshawishi. Ndio maana mpaka leo kuna watu wasiokunywa pombe japo wamezungukwa na watumiaji kila upande kwa miaka nenda rudi, bila kusahau ushawishi wa kutosha kutoka kwa wale wanaowazunguka.

Kwahiyo tuache kumlaumu anayetengeneza sumu, kisha anaeuza sumu na kuangalia je aliyekunywa sumu alisukumwa na nini?? Na sisi kama ndugu/jamaa na marafiki tulichangia kwa kiasi gani kumuacha/kumsukuma (kwa kushindwa kuwa nae pale alipotuhitaji) ndugu/jamaa ama rafiki yetu anywe sumu? Ukweli ni kwamba mwisho wa siku hao drug dealers ni wafanyabiashara. Wanachojali wao ni kuuza mzigo wao tu, hawachagui wa kumuuzia ili mradi apate hela. Wanaotakiwa kuleta mabadiliko ni sisi na sio wao kwasababu ushawishi wao ni mahsusi kuongeza victims ili biashara ikue na sio kupunguza.

Wewe kama mwana jamii, mwana familia, rafiki do your part. Muepushe rafiki, jirani,ndugu na jamaa yako na madawa ya kulevya. Usikae kutegemea ”drug dealer” mwenye uchu wa pesa atakusaidia kwa hilo, kamwe haitotokea.

Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe!

AdvertisementMtokambali 728x90