Tangazo

Samsung Galaxy S8 na S8 Plus? Yes nina habari njema kwako ewe mpenzi wa Samsung…

Tetesi zilizoko mitandaoni na maeneo mengine ni kwamba kampuni ya utengenezaji wa Vifaa vya kielekroniki Samsung wanapanga kuachilia Toleo lao jipya la Simu janja aina ya Samsung Galaxy S8 na S8 plus mara tuu itakapofika tarehe 18 April mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba mnamo mwaka 2016 kampuni hiyo iliangukia pua mara baada ya toleo la S7 kuondolewa sokoni kutokana na Simu hizo Kulipuka. Jambo ambalo liliifanya kampuni hiyo kupata hasara na kupoteza mabilioni ya Fedha licha ya takwimu kuonyesha kampuni hiyo ilifanya vyema kibiashara mwaka jana.

Teyari mtandao wa uchambuzi wa maswala ya Teknolojia hususani Vifaa kama vile simu, tablets GSMArena umeweza kunasa michoro mbali mbali kutoka kwa watengenezaji wa Housing za simu hizo ikionyesha Size kamili ya simu hizo yaani S8 na S8 Plus.#Tetesi: Samsung Galaxy S8 na S8 Plus kuachiliwa mwezi Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa GSMArena, size(urefu na upana) ya simu hizo itakua ni 140.14 x 72.20 x 7.30mm kwa S8 na 152.38 x 78.51 x 7.94 mm kwa S8 Plus. Kama kweli tetesi hizi zitakua ni za kweli, basi S8 plus itakua ndefu kuliko S8 na S8 itakua ni pana kidogo kuliko S8 Plus.

Tetesi hizi zinaendena na zile zilizokuwako hapo awali kwamba simu hizi zitakua na Vipimo vya Inc 5.7 kwa inch 6.2.

Kulingana na Vipimo hivi, ni wazi kwamba ile Home Button ambayo tulikua tumezoe kuiona katika simu za Samsung nyingi haitakuepo na badala yake itakua pembeni pamoja na zile Button za Sauti.

Ni wazi kwamba Samsung teyari walikwisha kuweka mambo sawa katika upande wa Camera za simu zao hasa katika kizazi hichi cha SAMSUNG EDGE hivyo hakuna wasiwasi juu ya Ubora wa camera katika toleo lao hili Jipya.

Nadhani huu ni wakati mwafaka kwa Samsung kuachilia Kitu hichi kipya ili kuongeza Ushindani ambao upo kati yake na iPhone ukizingatia tena baba karudi NOKIA 6, bofya >hapa< Kusoma zaini juu ya NOKIA 6.

AdvertisementMtokambali 728x90