Tangazo

Magufuli

Kampuni inayotarajiwa kufanikisha
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda
imesema iko tayari kuanza ujenzi huo.

Makamu wa Rais wa kampuni ya
Total Afrika Mashariki Bw Javier Rielo amemwambia Rais wa Tanzania John
Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi huo haraka iwezekanavyo, kwa
kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Mradi huo utahusisha
ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha
mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Bw Javier, akikutana na Rais Magufuli ikulu ya Dar es salaam, amesema
kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4
ambazo tayari zimeshaandaliwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais
Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa
mradi, na kupendekeza muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi
huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, Tanzania pia inatarajia
kunufaika zaidi na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta
zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania.
Amesema zikikamilika kwa mafanikio, inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Makubaliano
ya kujengwa kwa bomba hilo yaliafikiwa wakati wa mkutano kati ya Rais
Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mapema mwezi huu.

AdvertisementMtokambali 728x90