Utegemezi, dependant, DPD, Mtumwa
Tangazo

Utegemezi ni hali ya mtu kujiona hajitoshelezi mwenyewe na kujikuta akitaka/hitaji kuwezeshwa na watu wengine haswa kihisia,kifedha na hata kiakili.

VITU VINAVYOSABABISHA UTEGEMEZI

1.Kukosa maarifa na msukumo wa kujituma. . .Unakuta mtu hajasoma hivyo inakua ngumu kupata kazi inayohitaji kisomo. Za kawaida na ujasiriamali anapuuza maana hapendi kujituma.

2.Malezi na mazoea. . .Kuna watu katika kulelewa kwao walizoea kila kitu kinatoka kwa baba/mama mpaka umri ambao ni mkubwa sana. Yani wanaendekezwa. . . sasa ikitokea yule mzazi hayupo tena au hana uwezo wa kumpa mahitaji yake mtoto (ambae ni mtu mzima sasa) anatafuta pengine pa kutegemea maana hakufundishwa kujitegemea. Watu huwa wananyanyasika kweli kwa hii hali baadae wanapojikuta kwenye mazingira yanayowalazimu kujitegemea. Na ndio maana ni muhimu kuwafundisha watoto kujitegemea kihisia. . .  kimatendo na kimawazo.

3.Kutokujiamini. . .Hii inaweza kuwa ni matokeo ya #2 hapo juu au ikawa tu ni matokeo ya low-self esteem and morale.

4.And then there is the Dependent Personality Disorder. . .Unakuta mtu yeye kama yeye haamini kwamba anaweza kujitosheleza mwenyewe kwa namna yoyote ile (emotionally. . financially. . .au hata kimawazo) Yani lazima ategemee watu wengine. . . hivyo ndivyo alivyojengeka.

Binafsi naamini kwamba utegemezi ni ugonjwa mbaya zaidi ya ukoma. . . mbaya zaidi kwa kuwa tegemezi ni sawa na kujiweka mahabusu. Unakosa uhuru wa kufanya yale unayopenda na kuamini. . . unakosa kuheshimiwa. . . unakosa ujasiri wa kusimamia yale unayoona unastahili. . . unashindwa KUWA WEWE na kujikuta unakua yule watu wanaotaka uwe kwasababu unawategemea.

Kama wewe ni tegemezi basi hisia zako. . matumizi yako. . .mawazo yako na maisha yako kwa ujumla yanaendeshwa na mtu/watu wengine. Kwa ufupi wewe ni MTUMWA. Na njia pekee ya kuondokana na utumwa wa namna hii ni kuacha UTEGEMEZI.

Jinsi ya  kuondokana na UTEGEMEZI.

1.Anza kuwa na na mawazo yanayojitegemea. Usikubali kupelekeshwa na mawazo/imani za watu wengine. Kuwa tofauti na watu wengine sio kosa na wala sio vibaya as long you are not hurting anyone. Let people agree to disagree with you.

2.Jitume.Kama ni mama wa nyumbani anzisha bustani au kabiashara kako kadogo. Fuga kuku uza mayai. . .nunua mboga mboga za jumla uza mtaani kwako.Yani hakikisha chumvi ikiisha huendi kukopa na kusubiria baba nanii aje umuombe sh.300. Kwa wanaume vile vile. . . yawezekana mkeo ndio mwenye kazi/kipato kikubwa. . . wewe hakikisha tu unatoa mchango wako nyumbani. . . hata kama ni mdogo.

Kama ni binti. . .pangilia pesa ya matumizi unayopewa kama vile umetoka kuifanyia kazi na unaionea uchungu. Jifunze kujipa unayohitaji kabla ya unayotaka kukwepa mitego ya kuwa tegemezi.

3.Fanya wewe ndio uwe mwamuzi mkuu wa nini kinachoendelea maishani mwako.Kwepa kuwapa watu wengine fursa ya kukuendesha. . . wewe ndo unatakiwa uwe dereva. Ukikata kona unakata kwasababu ndicho ulichotaka na sio ulicholazimika kufanya.

Ushauri  kwa wazazi na walezi…

1.Jitahidi kumpa mwanao/nduguyo elimu ya darasani pia ya maisha. 

2.Mruhusu/mfundishe kujieleza pale mnapokua mmepishana badala ya kusema tu “mimi ndie mwamuzi”. Hata kama ni kweli, reason with him/her ili aelewe kwanini. Hii itamsaidia kuwa na mawazo yanayojitegemea badala ya kuwa bendera fuata upepo.

3.Mfundishe kusimamia kile anachoamini as long as hatendi kosa.

4.Mfundishe kujituma. . .mpe kazi ndogo ndogo hata kama mna mfanyakazi/ wafanyakazi. Badala ya kutengewa chakula mezani na kuondolewa nvyombo. . .kutandikiwa kitanda na kusafishiwa chumba chakulala anaweza akafanya hizi shughuli mwenyewe. It only takes a couple of minutes a day. . ila somo lake litadumu maisha.Nakumbuka sisi nyumbani tulikua na sheria. . .ukila/kunywa kitu bila watu wengine lazima usuuze vyombo utakavyochafua. Na Vyombo vya milo ya pamoja vilikua vinaoshwa na mtu mmoja baada ya chakula.

5.Mjengee kujiamini.

6.Mfundishe THAMANI YA PESA. Hii inashirikiana sana namba nne na ntaitolea mfano.Ndio inawezekana uwezo unao wa kumnunulia kila atakacho ila kwa kufanya hivyo hutokua unamsaidia maana mbeleni hayo mazoea yatakuja kumsumbua.

Mfano. . .Kila mwezi tulikua tunapewa pesa kidogo ya ALLOWANCE. . .bila masharti. Ila sasa ilikua mtu ukitaka vitu ambavyo sio neccessities (video games,CDs,sijui music players na vikorokoro vingine vya aina hiyo ) unaulizwa kwanza una sh. ngapi. Tulikuwa tunatakiwa tusave atleast nusu ya bei ya hicho tunachotaka alafu tuongezewe nusu. Au unakopa na kukatwa kwenye allowance inayofuata badala ya kununuliwa tu. Hii kitu ilitufanya tuwe tunaheshimu vitu vyetu na kujiuliza mara mbili mbili “do I really need/want this”  kabla ya kununua kitu. It helped. . .maana mpaka leo na kesho hua sinunui wala sitaki kitu nisicho na uwezo nacho hata kama nakitamani.

pale atakapokua hawezi kuridhisha tamaa yake maana kuidhibiti hawezi.

 

 

AdvertisementMtokambali 728x90