Uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ya kubadili laini: Vitu muhimu vya kufahamu

Uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ya kubadili laini: Vitu muhimu vya kufahamu
Tangazo

Nadhani hadi sasa utakuwa umekwishapata taarifa ya uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ata ya kubadili laini/namba ya simu kama ilivyokuwa kwa muda mrefu kabla. Na tunaamini maswali yatakuwa mengi tayari.

Fahamu hapa mambo muhimu ya kujua;

Utaratibu wa kuhama mtandao huku ukibakia na namba ya simu ileile

Itakubidi ufike kwenye mtandao wa simu yako na ujazo fomu ya kuomba uhamisho, hatua ya pili itakuhusisha kuandika neno HAMA kwenye huduma ya SMS na kutuma kwenye namba 15080. Na utapata majibu kuhusu zoezi lako la kuhama mtandao.

Huwezi kuhama mtandao kama una deni kwenye mtandao unaouacha.

Hili limesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, hautaweza hamisha namba yako ya simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kama una deni la aina yeyote kwenye mtandao wa simu uliopo. Hii inamaanisha deni la vocha, au la huduma za pesa kama vile mkopo kwenye huduma ya TIMIZA Airtel na nyinginezo kama hizo.

Hakuna kuhama mtandao mara mbili ndani ya siku 30.

Ni lazima ukae kwenye mtandao uliopo kwa siku si chini ya 30 kabla ya kuomba tena kuhama mtandao wa simu.

Wakati unahama

Kipindi cha muda ambao namba yako inafanyiwa kazi kuhamishiwa mtandao mwingine huduma za kipesa za mtandao uliopo kama vile Airtel Money, MPesa, n.k zitasitishwa kwa muda huo na kurudishwa ukiwa tayari umehamia mtandao mpya. – ila huduma zingine zote kama vile kupiga na kupokea simu na sms zitafanya kazi kama kawaida.

 

CREDITS TO: http://teknokona.com
AdvertisementMtokambali 728x90