Tangazo

Rashid Yussuf Mchenga
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni
muungano wa mfano duniani. Ni dola mbili huru zilizoungana na kuunda
nchi moja yenye serikali mbili.

Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9/1961
na ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa Desemba 14, 1961. Namba ya
kiti hicho ni ‘GA resolution 1667 (XVI).’ Zanzibar nayo ikapata uhuru
wake Desemba 10, 1963 na ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa
Desemba 16, 1963; namba ya kiti hicho ni ‘GA resolution 1975 (XIII).’

Ilipofika Aprili 26, 1964, mataifa hayo mawili
huru yaliungana na hapo ndipo ilipozaliwa nchi iliyojulikana kwa jina
la Tanzania.

Novemba 2, 1964 kupitia Wizara wa Mambo ya
Nchi za Nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliuandikia
barua Umoja wa Mataifa na kutaka Zanzibar na Tanganyika ziondoshwe
katika orodha ya mataifa na iingizwe nchi inayojulikana kwa jina la
Tanzania.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na
muungano wa Siria na Misri walioungana mwaka 1958 na ni sawa na muungano
wa Yemen ya Kaskazini na Yemen ya Kusini walioungana mwaka 1990. Kwa
bahati mbaya muungano wa Siria na Misri ulivunjwa mwaka 1961 (ulidumu
kwa miaka 3).

AdvertisementMtokambali 728x90