Watu wanaopenda kufanya mambo peke yao na kutumia muda mwingi faragha huwa werevu na imara

Tangazo

Jamii zetu za leo zinasisitiza kwamba tupende kutumia muda wetu mwingi tukiwa pamoja na wenzetu kwa kadiri tuwezavyo, hata pale tunapokua wapweke, tunatumiana ujumbe mfupi wa maandishi, ama kupigiana simu n.k. Lakini katika hali ya uhalisia kuna faida nyingi sana kwa kutumia muda wako mwingi ukiwa pekee.

Hali ya kujitenga sio hali ya kawaida sana katika ulimwengu huu ulio unganishwa kwa pamoja, na bado watu wanaojitenga huenekana kwamba ni watu ambao wako katika hali ya Upweke na machungu mioyoni mwao. Ingawaje jambo hili ni tofauti kati ya wanadamu, kuna watu hupenda kukaa peke yao nakufanya mambo peke yao maana hali hii huwasaidia kisaikolojia na kuwapatia uhuru kamili wa kufanya mambo yao. Kutumia muda wetu kukaa pekee ni jambo nzuri sana kwetu sis maana tunapata nafasi ya kupumzika na Kufikiri kwa kina zaidi.

1.Kutumia muda wetu tukiwa pekee hutufanya sisi kuwa na hali ya kujiamini zaidi.

Watu wote ambao hawajiamini hutegemea watu wengine kuwasaidia kufanya maamuzi, lakini kutumia muda wako ukiwa peke yako kutakufanya wewe kufanya maamuzi peke yako. Ukiwa peke yako, unaweza kutupilia maoni na idea za watu na kuwekeza zaidi katika maoni na mitazamo yako binafsi. Utapata nafasi yakupima faida na hasara ili uweze kufanya maamuzi sahihi ambayo yatakupelekea wewe kuwa na Ujasiri na kujiamini.

2. Kutumia muda wako ukiwa pekee itakusaidia kuongeza uzalishaji.

Tunapokua tumezungukwa na watu mara nyingi tunakua tukiingiliwa katika malengo yetu na Fursa tulizo nazo, ila tunapokuwa pekee tunapata nafasi yakufikiri zaidi katika malengo na fursa tulizo nazo jambo ambalo litatuweka sawa katika Kazi zetu, familia zetu na hata katika Fedha zetu. Hali hii hutufanya huongeza ufanisi na bidii katika kile tunachokifanya.

3. Kutumia Muda wetu tukiwa pekee hutufanya kuwa wabunifu.

Kila mtu ni mbunifu katika njia tofauti tofauti, lakini tunapokua katika kundi moja tunajikuta tukifanya kile ambacho kundi nzima linafanya. Lakini tunapokua wenyewe, ile misukumo itokayo kwa watu wengine na kutufanya mambo ambayo wanatakao wao hupotea kabisa na kutufanya sisi kufanya zaidi yale tuyapendayo zaidi. Baashi yetu tunapenda kuchora, Kupika, na wengine hupenda kuimba na kufanya muziki, ama Kucheza. Kuna njia nyingi za kuwa wabunifu na tunapokuwa wenyewe inatusaidia sisi kuweza kugundua ubunifu tofauti na pia itatuwezesha sisi kufahamu uwezo wetu binafsi katika yale tunayopenda kufanya.

4. Kutumia muda wako ukiwa pekee itakusaidia kutatua matatizo yako.

Suluisho sahihi huja pale tuu tunapokuwa pekee na kuakisi matatizo yetu, Kutumia muda wetu tukiwa pekee hutusaidia kupata suluhu ya matatizo yetu maana tunapata nafasi ya kufikiri zaidi matatizo hayo. Tunaweza kufikiri ni nini hasa chanzo na kiini cha matatizo hayo na kutengeneza njia za kutoka katika matatizo hayo.

5.Zaidi ya yote, inatupelekea kufanya mambo na kuishi katika hali kujitegemea.

Faida kuu yakutumia muda tukiwa pekee ni kuhamasika kufanya kazi zaidi pasipo utegemezi, unajua hata

. kufanya kazi independent kutakufanya uwe mbunifu, mzalishaji na zaidi ya yote mambo yako yataenda na kufanyika kama ulivyopanga.

Yawezekana nikawa nimeongea sana juu ya mtazamo wangu sasa ni wakati wako Kunieleza maoni yako juu ya Mada hii, naiandikie katika comment box hapo chini kisha tuendeleze mjadala wenye tija. Karibu na hili ni darasa huru.


Je Ungependa Kupokea Makala Zetu? Jiunge sasa ili kuweza kuzipata makala Zetu kila Mwisho wa Wiki moja kwa moja kwenye simu yako!

* inahitajika 


 

AdvertisementMtokambali 728x90
SHARE
Previous articleHealth eating – faida za CABBAGE
Next articleFahari ya Mwanaume!!
Ukiniita Mtokambali bado utakua sahihi, karibu na Hili ndilo chimbo langu, Utajifunza Mengi yahusianayo na Maisha. Kwa pamoja tuikuze mtokambali.com. Ungana nami twitter@mawere3. Siku zote "Haja ya Mja hunena na Uungwana ni vitendo"