Scandal in the family. Parents share child. Isolated on white background
Tangazo

Linapokuja swala la mahusiano/ndoa na watoto waliozaliwa kabla ya baba kuoa tena huwa hatuachi kuongelea mama wa kambo na malezi ya watoto. Jinsi walivyo wakorofi, wanyanyasaji, wakatili n.k Naongelea wamama tu maana wababa wengi huwa hawana matatizo wawe wazazi kabisa au walezi(wale wa kambo) linapokuja swala la mzazi mwenza kuwa na mahusiano mapya au wale wa kambo kulea watoto wa mwanaume mwenzie, tofauti na wakina  mama!

Mara nyingi wasiwasi huwa unakuwa kwa watoto zaidi na malezi/uwepo wa mama wa kambo.Tunasahau kwamba hata yule mwanamke mpya anaweza akanyanyasika na uwepo wa watoto wasio wake pamoja na mama yao bila kusahau ndoa yake kuyumbishwa kama mti usio na nguvu dhidi ya upepo. Kama tunavyojua wakati mwingine au niseme baadhi ya wanawake huwa na vinyongo..gubu..chuki kwa wazazi wenzao kwa kuachana nao…na kitendo cha mwanaume kupata mwanamke mwingine na kuoa hakiwi cha furaha kwa wote! Sasa wanawake wa aina hii wanaweza kutumia watoto wao kuyumbisha ndoa ya mwanaume aliyeachana nae pamoja na mke wake mpya, na  pia kusambaza chuki dhidi ya mwanamke mwenzie huyo.

Ila muhimu hapa ni hili la kuyumbisha ndoa…kuharibu au hata kuondoa kabisa amani ndani ya nyumba ya mwanamke mwingine kwa kutengeneza mazingira ya kuwachanganya wana ndoa hao! Unakuta mwanamke mwenye watoto anawatumia wanae kumuendesha mwanaume kama gari moshi kitu ambacho hakiwezi kumfurahisha mwenye mume. Yani kama aliyeolewa ni mwepesi wa kukasirika na kubugudhiwa ndoa inaweza ikaisha kabla hata utamu wa ndoa haujakolea.

Nakumbuka kuna mtu wangu wa karibu alipata shida sana kipindi cha mwanzo cha ndoa yake. Mama mwenye watoto alikuwa ni mkorofi sana na kila anachofanya anafanya kukomoa tu. Watoto amewahamishia shule ya kawaida ila ada anapokea ya shule ya international. Anawadanganya watoto wakubali kwamba wanaumwa ili amchune baba wa watu mpaka abaki mifupa tu. Ilikua kazi kweli maana unakuta mke alishataka/hitaji kitu akaambiwa pesa hamna bwana mwezi huu tufanye kitu flani alafu mwezi ujao tutafanya utakavyo…alafu mama watoto anapiga simu na kuagiza, wala sio anaomba awe amepata kiasi kikubwa cha hela  ndani ya masaa machache na anapata bila ubishi. Mwenye mume alilia mpaka baadae alipogundua kwamba sio kosa la mume wake…yeye tatizo lake ni mapenzi kwa wanawe na woga kwa yule mama watoto. Ikabidi aanze kumshauri mumewe asiwe mwepesi wa kukubali kuchezewa na yule mama watoto ndo mume nae akawa mgumu na kukataa kusukumwa sukumwa hovyo kama mkokoteni!

Kwahiyo naomba niwaulize wababa wenye mtoto/watoto tayari na hampo kwenye ndoa ila mnatarajia kuwa siku moja, mmejiandaa vipi kukabiliana na changamoto zitakazosababishwa na juhudi za wazazi wenzenu kutaka kuvuruga ndo zenu na kuwaondolea amani ndani ya nyumba????!

Binafsi naamini mwanaume akikataa kuchezewa na mzazi mwenzake basi haitatokea. Hivyo basi nawashauri muwe mnawapa wale mlio nao kipaumbele kwa kiwango cha kutosha. Kama akikutaarifu kuwa kuna matatizo yanayosababishwa na mzazi mwenzio hakikisha tu haitokani na chuki ya mke wako dhidi ya mzazi mwenzio kisha fanyia kazi. Usikubali kuharibiwa ndoa/mahusiano yako kwa kisingizio cha watoto ambao hata hawahusiki. Usikubali kutumiwa wala kuchezewa akili. Kwa wamama, ukijikuta kwenye situation kama hii jitahidi kuwa mvumilivu na mshauri wa mumeo badala ya kuwa mlalamishi tu. Pia jitahidi matatizo yatakayosababishwa na mama mtu yasizae chuki kwa mtoto!!Watoto huwa hawachagui wazazi wao kutengana na kulelewa na mama/baba wa kambo hivyo hawastahili kuadhibiwa na kunyanyaswa kwa hilo.

AdvertisementMtokambali 728x90