Ifahamu historia ya Gyptian mkali wa muziki kutoka Jamaica

0
317

Kwa majina kamili anajulika kama Windel Beneto Edwards a.k.a Gyptian na alizaliwa tarehe 25 October 1983 huko nchini Jamaica. Ni mwimbaji wa Muziki aina ya Raggae (Dancehall).

Alizaliwa katika familia yakidini yaani mama yake alikua ni mfuasi wa Dini ya Kisabato(Seventh-day Adventist) na baba yake alikua ni Rastafarian. Alianza kuimba katika kwaya kanisani ambapo huko ndipo kipaji chake kilionekana.

Kwa kukitambua kipaji chake, Wazazi wake walimtambulisha Kwa mwalimu wa Muziki aliye julikana kwa jina la Mr. Wong ambaye pia Alikua Producer wa studio moja yenye jina la  Portmore, St. Catherine.

Sikulitilia jambo lile maanani, familia yetu ilikua ikinisihi kukaa katika studio za  Mr. Wong lakini mara nyingi nilikua nikitoroka. Siku moja waliniacha katika Studio zile na kuondoka na ndipo Safari yangu ilipo anzia – Gyptian.

Safari yake ya Muziki ikaanza…

Akiwa chini ya Uongozi wa Mr.Wong, Gyptian aliweza kuonekana katika Ulimwengu wa Muziki kwa Kishindo mara baada ya Kuibuka mshindi katika shindano moja la kusaka Vipaji huko nchini Jamaica mnamo mwaka 2004.

Alijipatia jina la Gyptian mtaani kwao kutokana na tabia yake ya Kufunga T-Shirt Shingoni kisha kutisa kidevu chake kama walivyokua wakifanya wafalme wa Egypt(Misri) Mafaraoh ndipo watu wa mtaani kwake wakampatia jina Egyptian ambapo yeye alilifupisha na Kujiita Gyptian..

Ikumbukwe kwamba jamaa huyu aliachia album yake ya kwanza mwaka Huo huo 2004 VP Records. Na ilipofika 12 December 2007, akiwa New York nchini Marekani alifanikiwa kutengeneza Video yake ya kwanza ambayo iliongozwa na Director Rhona Fox, video ilikua ni ile ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la “I Can Feel Your Pain” ambapo nyimbo hiyo ilikuja kuthibitishwa itakuepo kwenye album yake ya pili iliyo pewa jina hilo hilo la I Can Feel Your Pain” ambayo ilitoka rasmi mwaka 2008.

Mafanikio yake kimataifa…

Ilipofika mwaka 2010, ngoma yake ya “HOLD YUH” ilifanikiwa kuingia katika chart za Billbord( Billboard Hot 100) nakufanikiwa kushika nafasi ya 91, namba 33 katika chart za Billboard R&B/Hip-Hop na namba 6 katika chati za  Billboard Heatseekers Songs na aliwahi kukaa kileleni katika chati za Reggae Digital Songs kwa wiki Tisa(9) mfululizo.

Nyimbo hiyo ya Hold Yu ilifanyiwa Remix ambapo ndani alishirikishwa Nick-Minaj na ikafanikiwa kuingia tena katika chati za Billboard Heatseekers Songs ambapo ilikaa katika chart hizo kwa muda wa wiki 29, na wiki 15 katika chati za Billboard Hot 100.

Mnao mwaka 2013 alifanikiwa kuachia album yake ya Tatu ambayo aliipa jina la Sex, Love & Reggae na album hiyo ilifanikiwa kuingia katika chart za Billboard Top Reggae Albums na kuchukua nafasi ya Kwanza. Album yake ya mwisho aliitoa mwaka jana 2015 na aliipatia jina la Nothing to Lose.

Uandishi wake na aina ya Muziki anao-fanya…

Reggae music ni aina ya muziki anoafanya na umekua ukichukiliwa kama  lovers rock na  roots reggae muziki unao husika na Mapenzi pamoja na siasa. Na mara nyingi aina yake ya muziki na uandishi wa Mashairi unafananishwa na Ule wa msanii  Sizzla, Luciano na  Beres Hammond wote ni wasanii walio wahi kuwika vilivyo huko nchini Jamaica.

Baadhi ya ngoma ambazo zilimuweka Gyptian kileleni ni…

Nah let Go
Hold yuh
all on me
Mama Dont Cry.

Mpaka hapo nimefika mwisho wa makala hii ambayo ilikua ikimzungumzia mwanamuziki maarufu ulimwenguni kutokea Jamaica sii mwingine bali ni Windel Beneto Edwards almaarufu kama Gyptian.

ACHA JIBU

Tafadhali weka Maoni
Tafadhali weka Jina lako hapa