Ninapo litaja jina la Lucky Dube ni wazi kwamba utakua unafahamu moja kwa moja namzungumzia nani. Ni moja kati ya wana harakati walio tetea haki za wanadamu hasa watu weusi walio kuwa wakibaguliwa na kuonewa kila siku kupitia sanaa ya Muziki. Kupigania Uhuru wa Africa kutoka mikononi mwa makaburu. Leo nitakupatia Historia kamili ya Mkali Huyo ikiwa ni pamoja na Historia ya maisha yake tangu kuzaliwa, safari yake ya Muziki, harakati za kupambana na Ubaguzi ulimwenguni….
Maisha yake ya Awali.
Jina lake kamili ni Lucky Philip Dude, na alizaliwa mnamo 3 August 1994 huko nchini Africa ya kusini katika eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama Mpumalanga, awali eneo hilo lilijulikana kama Eemelo. Wazazi wake walitengana kabla ya Luck Dube Kuzaliwa, hivyo Lucky alilelewa na mama yake. Mama yake alimuita jina la LUCKY baada ya kuteseka muda mrefu bila kupata ujauzito hivyo akampatia mwanae huyo jina la LUCK(Bahati).
Akiwa na ndugu zake Thand na Patricky, Dube alikua akiishi na Bibi yake ambae ni mzaa mama kipindi chote cha udogo wake wakati mama yake akiwa kazini. Moja kati ya interview aliyo fanyiwa mnamo mwaka 1999, alieleza kwamba bibi yake ndie Kipenzsi chake, ambae alipigania yeye kuwa yeye leo hii.
safari yake ya muziki ikaanza.
Akiwa bado mdogo, Lucky alikua akifanya kazi kama gardener ila alipo kuwa mkubwa aligundua kuwa kazi ile haikuwa ya kumpatia kipato ambacho kingewezsa kutosha kuilisha familia yake, na ndipo akaamua kuanza shule ambapo shuleni huko alijinga na Kwaya na kuanza kuimba katika kwaya.
Wakati akiwa shuleni huko pia alikutana na marafiki zake ambao kwa pamoja waliamua kuunda kundi lao la muziki ambalo waliliita skyway Band. Akiwa na umri wa miaka 18, alijiunga na Band ya Binamu zake iliyo julikana kwa jina la The Love Brothers ambalo lilikua likipiga muziki aina ya Zulu Pop music wakati huo wakifanya kazi katika machimbo ya Dhahabu huko Midrand wakiwa kama walinzi na wapishi wa eneo lile.
Kundi lile lilipata deal la kusign katika Record label ya “Teal Record Company” na hapo walipewa nafasi ya kurekodi ngoma zao ingawaje Lucky yeye bado alikua bado yupo shule ila alikua akiingia studio kipindi alipo pata likizo. Walifanikiwa kutoa Album yao ya kwanza iliyopewa jina la “Lucky Dube and the supersoul”. Na ikumbukwe kwamba wakati ule ule ndio mda ambao Luck Dube alianza kujifunza Kiingereza.
Lucky ana hamia kwenye Reggea.
Kipindi Album yake ya Tano ikitoka(Mbaqunga), Dave Saga ambaye badae alikuja kuwa sound Engineer wa lucky Dube alimshauri Luck Dube kuacha zile Element alizo toka nazo kule kwenye band aliyo kuwako na Kuanza kurekodi Album zake zote zilizo fuata kwa Jina la Lucky Dube. Wakati huo Dube aligundua kwamba mashabiki wake walikua wakionyesha muitikio pale alipo kuwa akiimba nyimbo za rege katika matamasha yake. Ambapo alikua akivutiwa sana na Wasanii kama vile Peter Tosh pamoja na Jimmy Cliff wote walikua wakicheza rege. Aliona kwamba zile socio-political messages zilizo kuwa zsikkimbwa katika Jamaican Rege zingefaa kabisa katika jamii ya kibaguzi aliyo kuwa akiishi yeye Lucky Dube.
Aliamua kuazisha aina nyingine ya muziki(Rege) na alifanikiwa kutoa album iliyopewa jina la Rasters Never Die na album hiyo haikuuza sana kama ilivyo tarajiwa kwani iliuza kopi 4000 ukilinganisha na ile ya Mbaqunga iliyo ulaza Kopi 30,000. Album hiyo ilifungiwa mnamo mwaka 1985 enzi za Ubaguzi kutokana na mashairi ya Nyimbo za Album(hasa katika ule wimbo ulio julikana kwa jina la “War and Crime”) hiyo kuchoma vikali serekali ya Makaburu walio kuwa wakiongoza Africa Kusini kwa kipindi kile.
Ingawaje hakukata tamaa ila aliendelea kutengeza ngoma za rege na baadae aliachilia Album ya pili iliyo pewa jina la “Think About the Childrean”, album iliyo vunja Rekodi ya mauzo na kumfanya Lucy Dube kuwa mwana muziki maarufu wa Rege Africa na Ulimwenguni kote.
Biashara na mafanikio katika muziki.
Lucky Dube aliendelea kutoa album kali zilizo uza kwa wingi, na mno mwaka 1989 alifanikiwa kushinda Tuzo Nne(4) tuzo zilizo julikana kwa jina La “OKTV awards” kupitia wimbo wake wa Prisoner na baadae tena kuchukua tena tuzo nyingine kupitia Cuptured life mwaka ulio fuatia na baadae kuchukua tena tuzo mbili kupitia ngoma yake ya House of Exile. Album yake ya Victims iliuzsa zaidi ya kopi milion moja ulimwenguni kote na mnamo mwaka 1995 alipata dili la kurekodi akiwa na Motown Records.
Mnamo mwaka 1996 aliachia Albu yake iliyo mfanya kuwa juu zaidi album iliyo pewa jina la “Serius Reggae Busness”, Album iliyo mfanya kujulikana kama Mwanamuziki aliyefanya mauzo Mengi ya Juu na msanii bora wa kimataifa. Album zake zote tatu zilizo fuatia zilifanikiwa kuchukua tuzo Huko Bondeni kwa Mzee Madiba.
Kifo na Mauti.
Mnamo tarehe 18,October-2007, Lucky Dube ali uawa kwa kupigwa Risasi akiwa njiani kuwapeleka wanawe wawili kwa mjomba wao. Taarifa zilizo toka kuhusiana na Kifo chake ni kwamba,, majambazi walikuwa wakitaka kumpora gari lake hilo la Kifari aina ya Chrysler 300C. Watu watano walikamatwa kwa kuhusishwa na kifo cha Dube na watatu kati yao walipatikana na hatia na Kuhukumiwa Kifungo cha maisha Gerezani.

Na huo ndio mwisho wa Makala yangu kwa leo tafadhali nitaomba unipatie maoni amba ushauri wako kupitia anwani yangu ya mtokambali2015@gmail.com ama namba yangu +255767322193(WhatsApp only).Pia nitoe shukrani zangu kwa WIKIPEDIA kwa kufanikisha kuandika Makala hii

ACHA JIBU

Tafadhali weka Maoni
Tafadhali weka Jina lako hapa