Je umeawahi kufikiri kumiliki ama Kufungua Blog yako? Huu ni mwongo kamili ulio andaliwa ili kukuwezesha wewe ulie na nai ya dhati kabisa ya Kufungua na Kuimiliki blog yako kwa mwaka 2018 na Kufanikiwa. Mwongozo huu ni marekebisho ya Mwongo ulio tolewa mwaka jana ambao ulisaidia wengi kufungua Blog zao na Kuziendesha kwa mafanikio Zaidi. Hivyo Mwongozo huu umekua ukiboreshwa Kila muda kutokana na Mawazo na mchango unaotoka kwa Rafiki waotoa Comments zao juu ya mwongozo uliopita.

Hadithi ya mimi kufungua Blog na kuiendesha Blog yangu ilianza mwaka 2012 kipindi ambacho nikiwa chuoni amabapo sikua napenda sana vipindi darasani hivyo nilikua nikitumia muda mwingi katika vyumba vya Computer chuoni ambapo pia kulikua na Free internet ambayo iliniwezesha mimi kupitia tuvuti mbali mbali ambazo zilikua zinatoa mafunzo mbali mbali yahusuyo Teknolojia,Biashara na Burudani. Huko nilijifunza mengi ambapo nilipata Shauku ya Kufungua Blog yangu na mimi ili niweze kutoa mchango kwa Kile nilichokua nacho. Nilifanikiwa Kufungua Blog hii lakini ilikua ni Free yaani Sikua na Personal Domain name wala Hosting mpaka leo nipo Na hii ndio MTOKAMBALI.

Leo nitakunyesha ni kwa namna gani utaweza kufungua blog yako ambayo sio zile za bure yaani Free domain mfano jinalako.blogspot.com au jinalako.wordpress.com n.k. Hapa ntakuonyesha ni wapi ununue Domain yako na hosting yako ili uweze kumiliki blog yako ambayo utakua na umiliki kamili wa blog yako hiyo. Na ndani ya mwongozo huu nitakupatia Njia mbali mbali za kuikuza blog yako hiyo na kufanikiwa. Upo teyari?

Muhtasari:

Yafuatayo ni Mahitaji muhimu ya kuanzia safari yako.

  1. Nunua domain na bundle(Kifurushi) kwa ajili ya hosting
  2. Install(Weka) WordPress kwenye cPanell yako
  3. Chagua theme(Muonekano) mzuri kwa ajili ya Blog yako
  4. Andika Chapisho(Post) lako la kwanza.

Sasa tuchambue kwa kina hatua tajwa hapo juu.

1.Nunua Domain name na bundle(Kifurushi) kwa ajili ya hosting

Jambo la kwanza la kufanya ni kununua Domain name na kifurushi/bundle kwa ajili ya hosting ambapo ndipo mahali files zote za blog yako zitahifadhiwa, napozungumzia domain ni anuani(Adress) ya kimtandao ambayo itakua ikiwapeleka watu kwenye tuvuti/blog yako mfano jinalako.com au jinalako.co.tz au jinalako.tv. Na pia napozungumzia HOSTING namaanisha mahali Blog yako na Vitu vyake vyote ikiwa ni pamoja na picha, video n.k.  Hapa mara nyingi huchanganya watu kwamba ni wapi watapata vitu hivyo likini leo nakuonyesha utavinunua wapi.

Kipekee napendekeza OLEDOINYO WEB SERVICES wawe nisuluhisho la Bundle bora kwa ajili yako. Kwa Muda mrefu binafsi nimekua nikihamisha hamisha blog yangu hii kutoka huku kwenda kule ama kule kwenda kwingine yaani kama vile mtu anavyokua akibadili mitandao ya simu na hii ilitokana na huduma Mbovu na gharama kubwa walizokua wakinipa hao wengine ila nilikuja kukutana na OLEDOINYO WEB SERVICES ambapo walinipatia suluhisho la tatizo langu kwa bei nafuu kabisa na huduma Bora kwa hali ya juu kabisa, najivunia kuwa nao.

Bofya maneno yaliyo narangi tofauti(OLEDOINYO WEB SERVICES) hapo juu uwatembelee kisha fuata malekezo yafuatayo.Jinsi ya Kufungua Blog kwa mwaka 2018Picha hiyo hapo juu ni sehemu ya kwanza utakayo anzia pindi utakapo ingia OLEDOINYO kisha utabonyeza Get yours now ili uanza manunuzi ya Domain name yako pamoja na Hosting kwa ajili ya blog yako. Moja kwa moja utapelekwa hatua ya pili ambayo ni kukuonyeha Vifurushi(Hosting plans zao) kwa mwaka mzima kama Inavyoonekana katika picha hapo chini.

Utachagua Kifurishi kimoja kulingana na uwezo wako wa kifedha na mahitaji yako ambapo uzuri ni kwamba kwa kila kifurushi utapewa Domain Name Bure Kabisa(Hii ni nzuri si ndio). Baada ya kuchagua Kivurushi utabofya ORDER NOW ambapo utapelekwa hatua inayofuata ambapo itaonekana kama inavyoonekana katika picha hapo chini.

Baada ya kuchagua Domain yako, utabofya CLICK TO CONTINUE ili uende hatua inayofuata. baada ya hapo utapewa taarafa kwamba Domain name yako inapatikana Kisha Utendelea ambapo utapatiwa Order Summury ya Kifurushi ulicho nunua Kisha utabofya CHECKOUT ili kulipia ambapo utachagua Njia ya malipo mfano M-Pesa nk  na baada ya hapo utalipia kisha utaruhusiwa kuendelea na Hatua ifuatayo ambayo ni Install WordPress kwenye cPannel yako.

2.Weka/install WordPress kwenye cPanel yako.

Baada ya Kufanya malipo, Utapatiwa accsess ya Control Pannel(cPannel) yako. Napozungumzia cPannel namaanisha uwanja ambao una mpangilio wa mambo mengi ikiwa ni pamoja na software mbali mbali kama vile WordPress(Mfumo utakao kuwezesha wewe kupata nafasi ya Kuandika na kuchapisha machapisho ya Blog yako), Emails nk. Sasa kazi ya Pili ni kuiweka WrdPress kwenye cPannel yako na hapa OLEDOINYO wamekurahisishia kiasi kwamba utabonyeza Kitufe cha wordpress mara chache tuu kisha mambo yanakamilika.

Baada ya Kuingia kwa cPannel yako, utakutana na mambo mengi ambayo kwa sasa hayatakua na umuhimu ssana kwako kwa wakati huu, hivo utashuka mpaka chini pale na kukutana na “WORDPRESS MANAGER” utachotakiwa hapo ni Kubofya kitufe hicho na Kisha Kujaza Details zako mfano Jina la blog yako, Email utakayotumia, na PassWord zako kisha Utabofya “Continue” sasa hapo WordPress Itakua instilled na Kukamilika Kisha Utatumiwa “User Name” na “PassWord” kwenye Email yako. Ili kuingia sasa kwenye blog yako, utatumia domain name yako mfano www.jinalablogyako.com/wp-admin kisha utaweka User name na Password ulizotumiwa na hapo hatua ya Pili itakua imekamilika.

3.Chagua theme(Muonekano) mzuri kwa ajili ya Blog yako.

Mara nyingi watu wengi hupenda kutumia kwanza themes zilizoko teyari ndani ya WordPress ili waandike machapisho mengi kisha wabadili mionekano ya Blog zao baadae, lakini napenda ufanye kwanza kuweka theme mpya na kuifanyia kazi ndipo uanze kuandika. Utakachotakiwa kukifanya hapo ni Kubofya Changa Theme Completely na hapo utapata nafasi ya Kubadili theme na kuifanyia Customizations ikiwa ni pamoja na kubadili rangi, logo nk.

Baada ya kufanya vyote hivyo, teyari utakua umekwisha kumaliza kazi na Blog yako inakua imekamilika na Upo teyari sasa kuandika machapisho yako na Kufurahia Blogging.

Mpaka hapo nimefika mwisho, tafadhali kama utakua na swali lolote ama kama kuna jambo nitakua nimesahau, tafadhali nijuze kwa kuweka Comment yako hapo chini na mimi nitazifanyia kazi. Aksante.

ACHA JIBU

Tafadhali weka Maoni
Tafadhali weka Jina lako hapa