Kama unafikiria Kuanzisha Blog yako leo, basi ni wazi kwamba utahitaji blog binafsi si ndio?. Watu wengi watakushauri kwamba ili uweze kusima kama Brand ni lazima uwekeze kwenye Blog binasfi yaani Self-Hosted.

Lakini ni Kwa nini Blog Binafsi(Self Hosted blog) ilhali unaweza tuu kuanzisha Blog yako ya Bure(Free Blog) na ukaendelea kutoa huduma kama kawaida pasipo na tatizo lolote? Hapo chini nimeelezea Tofauti kati ya Blog Binafsi(Self hosted blog) na Blog ya Bure(Free hosted blo), Faida na Hasara za Kila moja.

Blogu za Bure(Free hosted blog/platforms):

Maana ya Blog za Bure: Tunapozungumzia aina hii ya Blog ni kwamba tunamaanisha unajisajili na kuanzisha Blog yako Bure kabisa pasipo gharama yeyote huku Files(Majalada) picha na data zako zote zinahifadhiwa na Kampuni inayotoa huduma hiyo mfano kama google Kupitia program yao ya Blogger au WordPress. Ambapo Anwani ya Blog yako itakua inaambatana na Anwani ya Kampuni hiyo mfano Blogyako.blogspot.com au Blogyako.wordpress.com..

Faida zake:

 • Hakuna gharama yeyote itakayotumika wakati wa kuanzisha blog yako.
 • Hutohitaji ujuzi wowote ili kuitengeneza blog yako(Ni rahisi sana Kuitengeneza).

Hasara zake:

 • Labda uingie gharama ununue anwani ya Blog yako mfano jinalablogyako.com vinginevyo anwani ya blog yako itaambatana na anwani ya kampuni husika mfano jinalablogyako.blogspot.com au jinalablogyako.wordpress.com.
 • Mwonekano wa Free blog siku zote huonekana kama hakuna ufundi wowote jambo ambalo sio jema kwa branding.
 • Hakuna Umiliki kamali wa blog hiyo.Katika hili hutokua na umiliki kamili wa blog yako jambo ambalo litakukwamisha kuiendeleza blog hiyo kiufundi Zaidi.
 • Pia memory ya blog yako huwa ndogo hivyo kukunyima wewe uhuru wa kujaza mambo meengi katika blog yako

Je ni gharama zipi hujumuishwa katika Blog yako hiyo ya Bure?

Kwa kawaida unaweza kuamua kitumia blog hiyo kwa free bila kikomo cha muda lakini ikumbukwe Kamba kuna wakati utaamua kujikwamua kutoka katika Free hiyo na utalazimika kununua anwani yako binafsi ambayo itakugharimu kiasi cha dola za kimarekani zisizopungua ama zisizozidi 10. Na Zaidi ya yote utalazimika kumtafuta mtaalamu wa kurekebisha mambo kadhaa ya kiufundi katika blog yako hivyo unaona wazi kwamba Bure sio Bure kamwe.

Je ni nani anapaswa Kutumia aina hii ya Blog?

Blog hizi ni kwa wale ambao wanajaribu kuufahamu ulimwengu wa blogging ila hawako serious kuhusu blogging yaani wao hufanya blogging kwa hobi tuu na sio vinginevyo hivyo kwa namna moja ama nyingine inampasa kuanzisha blog ya aina hii.

Blog Binafsi(Self Hosted blogs):

Maana Ya Blog Binafsi: Tunapozungumzia aina hii ya Blog ni kwamba unakua na umiliki kamili wa blog yako japukua watu hulazimika kununua bundles kutoka katika Servers za makampuni binafsi yanayotoa huduma hiyo mfano OLEDOINYO(ambayo nakushauri uitumie),Bluehost,Hostgator nk.

Faida za kuwa na Blog Binafsi.

 • Unakua na Full control ya blog yako yaani utaweza kubadili ama kuongeza chochote kwenye Blog yako katika upande wa matengenezo hasa pale linapokuja swala la Coding.
 • Utaweza kubadilisha Muonekano(Theme) amabayo umeifanyia Marekebisho kulingana na mahitaji ya Brand yako.
 • Unakua na uwezo wa Kuyafikia majalada(Files) ya Blog yako na Kufanya mabadiliko kwa kadiri utakavyo.

Vikwazo/hasara zake.

 • Utahitaji kuwekeza fedha wakati unaanza. Ni gharama kuanzisha blog yako.
 • Huwa inachanganya sana kwa wale wanoa anaza ambao hawana ufahamu juu ya Blogging.

Je ni gharama zipi hutuhitajika ili kuanzisha blog binafsi?

Utahitaji kununua huduma ya hosting kutoka katika makampuni ambayo yanahusika na kutoa huduma za Hosting ambapo makampuni mengi yatakuuzia huduma hiyo kwa kiasi cha Dola za kimarekani kuanzia dola 2 mpaka dola 5 kwa mwezi. Wakati mwingine kama huna Ujuzi wowote wa Kutengeneza blog utamuhitaji mtu mwenye Ujuzi ili akusaidie jambo ambalo utalazimika kumlipa mtu huyo kwa huduma hiyo.

Je ni nani anapaswa kumiliki blog binafsi?

Muonekano wa blog binafsi siku zote ni muonekano ambao ni Professional hivyo ni bora kibiashara. Na ni kwa wale ambao huchukulia blogging kama Biashara ama sehemu ya Maisha yao.

kwa hayo machache ni matumaini yangu kwamba utakua umeweza kung’amua mambo hayo mawili japo kwa uchache. Je bado unachanganya Mambo? niachie ujumbe wako katika comments hapo chini tuzungumze.

 

 

ACHA JIBU

Tafadhali weka Maoni
Tafadhali weka Jina lako hapa